Maandamano ya mabucha ya Nguruwe 1993

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
Mwaka wa 1993 ulikuwa mwaka mzuri sana kwangu kwani katika miezi 12 nilikuwa nimesafiri mara tatu tena ukichukulia kuwa mwaka wa 1991/92 nilikuwa Uingereza.

Nilikwenda Harare na ulikuwa mwezi wa Ramadhani.

Nilikaa Harare kwa majuma matatu na nikafika hadi Bulawayo.

Nikaenda Lusaka Zambia.

Niliporudi nikaenda Ufaransa nikawa Le Havre na Paris na safari ya kurudi nikapita London nikasali Eid Kubwa Regent Park Mosque hapo London kisha nikaenda Cardiff nikarudi Dar es Salaam.

Wakati huo Bunge liko Karimjee linaunguruma na sakata la Rais Mwinyi kuruhusu Zanzibar kuingia Organisation of Islamic Conference (OIC) na aliyehusika alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ahmed Hassan Diria.

Barua za Kiuchungaji zinashambulia serikali ya Rais Mwinyi pamoja na magazeti yote hata yale ya Chama na Serikali.

Rais Mwinyi akajikuta hana wa kumtetea ila Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro Mwinyi Mangara na ndani ya serikali akifarajiwa na Prof. Kighoma Ali Malima.

Hotuba za Ijumaa za Sheikh Kassim kwenye membar ya Mtoro zilitikisa nyoyo za Waislam na serikali nzima.

Siku ya Ijumaa msikiti unajaa hadi nje kufikia Mtaa wa Livingstone.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu alikuwa Augustine Mrema.

Kulikuwa na makaratasi ya "uchochezi," yakimwagwa misikiti yote ya Dar es Salaam yaliyokuwa yakiandikwa na "waandishi wasiojulikana," yakijibu Barua za Kiuchungaji.

Wachina wana msemo, "May you live in interesting times."

Hizi nyakati zilikuwa za kipekee kabisa hazikupata kutokea hata wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika.

Hii safari yangu ya Ufaransa ilikuwa imenifanya nipitwe na mengi ya mjini.

Niliporudi nikaenda Zanzibar kushughulikia mambo fulani kuhusu OIC mimi na mwenzangu mmoja.

Tulipokuwa ndani ya chombo tunarejea ndiyo tukapata taarifa kuwa Waislam wamevunja mabucha ya nguruwe baada ya sala ya Ijumaa.

Rais Mwinyi kwa hofu akasema wale waliovunja mabucha ya nguruwe "nguvu za dola ziwaangukie."

Hiki ndicho kilichokuwa kinasubiriwa.

Usiku mmoja hadi kufika asubuhi masheikh na wahadhiri wa Kiislam wakakamatwa.

Waislam wakahamaki taarifa ikatoka kuwa wakutane Msikiti wa Mtoro kujadili kuwatoa masheikh walipokuwa wamewekwa rumande Central Police.

Katika kikao kile cha Mtoro siku ya Jumapili asubuhi msikiti ulijaa vijana hakuna sheikh hata mmoja aliyehudhuria.

Allah amenijaalia kuona kwa macho yangu matukio makubwa katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Mjadala ulikuwa mkali vijana ndani ya msikiti wakidai kuwa uamuzi wowote utakaofikiwa siku ile utoke kwenye Qur'an na Sunna hapatakiwi rai ya mtu binafsi.

Kikao hiki bila kuuma maneno kilikuwa kikao cha vita.

Sijapata kuona hamaki kwa Waislam kama niliyoshuhudia siku ile.

Ndipo Sheikh Waziri Ramadhani akasimama na kusema, "Ndugu zangu Allah leo ametuletea mtihani kutuangalia kama tunaweza kusimama kuipigania dini yake.

Kama dhulma tumeshafanyiwa sana ifike mahali tuseme basi kwa kukamatwa viongozi wa Waislam ni dharau ya juu kabisa dhidi yetu.

Kila unachokiona duniani kinamtumikia Allah basi ndugu zangu tutokeni twendeni Central Police tukawatoe masheikh zetu."

Hapo ndipo yalipotokea maandamano ya kwanza ya Waislam na yalipofika Mnazi Mmoja katika hali ya jua kali ghafla wingu likatanda na mvua ikaanza kunyesha.

Maandamano yalipofika Clock Tower askari wa FFU walikuwa wanawasubiri waandamanaji hapo mapambano yakaanza.

Mabomu mengi yaliyopigwa pale moshi wake ulipeperushwa na ule upepo wa mvua.

Milango ya Central Police ambayo daima haifungwi ikafungwa kwa kuhofu ule umma ungeweza kuingia hadi ndani ya selo za polisi.

Waislam wengi walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Nahitimisha kwa kusema kuwa wakati haya yanatendeka Sheikh Kassim alikuwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu.

Hii ilikuwa "turning point," katika maisha yake kwani yeye alikuwa karibu sana na serikali na iliwashangaza wengi kumuona ameigeukia.

Kama si yeye kufanya vile na kusimamia haki Sheikh Kassim Jums angepita dunia hii kama walivyopita masheikh wengi wengine kabla yake.

Ndugu zanguni msimuone ndugu yenu kakataa kuitambua haki na akawa upande wa dhulma mkamkatia tamaa.

Muombeeni dua.

Kile kibri chake cha yeye kuwa upande wa wenye mamlaka na nguvu kisituvunje moyo.

Picha ambayo hainitoki kichwani mwangu ni picha ya Sheikh Kassim Juma mwaka wa 1979 anamkaribisha Nyerere ndani ya Msikiti wa Mtoro kwenye khitma ya aliyekuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.
 
Halafu ikawaje baada ya vurugu hizo? Iliingia kwenye maandishi jinsi watu wenye nia zao mbovu wanavyotaka kutumia dini kuleta mgawanyiko.

Muda mwalimu mzuri. Baada ya miaka kadhaa, Shekhe hebu tupe tathmini....mafanikio na kushindwa kwake kukoje
 
Ndahani,
Una "assume."

Kabla ya kuandika inahitaji ufanye utafiti kwanza.
 
Wala si assume. Kuna mambo yanafeli kabla hayajashika kasi. Mtu mwenye akili wala haimsumbui.

Nakuuliza, hebu toa mchanganuo wa mafanikio na kushindwa kwa move hii ya kuvunja bucha Manzese mwaka 1993
 
Hongera. Katika hadith yako umejitanabahisha kwa kuzitembelea nchi zenye Maduka ya Kitimoto karibia kila mtaa!

Sijaona ulipotembelea nchi za ndugu zetu katika imaan!

Kumbe, hawa makafiri ni wazuri hata ukawa kiguu na njia kila mwaka katika nchi za walipa kodi wala Nguruwe!
 
Mabucha mengi mlioharibu ya pale mzimbazi center walijenga tena na mdudu analiwa kama kawa. Najua lengo lako si suala la nguruwe.
 
Hongera. Katika hadith yako umejitanabahisha kwa kuzitembelea nchi zenye Maduka ya Kitimoto karibia kila mtaa!

Sijaona ulipotembelea nchi za ndugu zetu katika imaan!

Kumbe, hawa makafiri ni wazuri hata ukawa kiguu na njia kila mwaka katika nchi za walipa kodi wala Nguruwe!

Kesho asubuhi kama utakumbuka kuamka,soma hii comment yako.
 
Wala si assume. Kuna mambo yanafeli kabla hayajashika kasi. Mtu mwenye akili wala haimsumbui.
Nakuuliza, hebu toa mchanganuo wa mafanikio na kushindwa kwa move hii ya kuvunja bucha Manzese mwaka 1993
Ndahani,
Umezungumzia mgawanyiko ndiyo nasema ume- "assume."

Fanya utafiti ili ujue ukweli.
 
Hongera. Katika hadith yako umejitanabahisha kwa kuzitembelea nchi zenye Maduka ya Kitimoto karibia kila mtaa!

Sijaona ulipotembelea nchi za ndugu zetu katika imaan!

Kumbe, hawa makafiri ni wazuri hata ukawa kiguu na njia kila mwaka katika nchi za walipa kodi wala Nguruwe!
Mhadzabe,
Nimefika kwingi huko pia - Sudan, Misri, Saudia, Yemen, Muscat, UAE na Abu Dhabi.
 
Tanganyika haina waislamu tena ina watu wenye majina ya kiarabu.
Uislamu bila haki ya mwenyezi Mungu ni kutwanga maji kwenye kinu
 
Ina maana huu uzi hawauoni wakongwe wa JF kina Chige . Mimi nataka waje waongeze nyama ila naona kimya.
Ahsante kwa kunikaribisha kwenye mjadala ingawaje sina mengi sana ya kuchangia kwa sababu wakati ule bado nilikuwa kijana mdogo tu... ndo kwanza nilikuwa nimeanza Form I.

Hata hivyo, si kwamba nilikuwa kijana mdogo kama walivyo vijana wadogo wengi wasiopenda kufuatilia kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla, manake, moja ya mambo ambayo nilikuwa nawashangaza sana watu pale nyumbani na mtaani ilikuwa ni tabia yangu ya kupenda kusikiliza BBC, station ambayo ilionekana kama ni ya watu wazima na sio watu wa rika langu!

Lakini kwa upande mwingine, nimekulia kwenye kota za polisi... kwa maana nyingine, ingawaje sikuwa mkubwa sana lakini sikutoka kapa moja kwa moja kuhusu kilichokuwa kinaendelea kwa sababu kwa upande mmoja nilikuwa mtoto wa BBC, na kwa upande mwingine, nilikuwa nashuhudia kwa macho yangu harakati za polisi baada ya lile tukio!!!

It's a mess!!!

Sifahamu ni nini hasa kiliwapelekea baadhi ya Waislamu kuvamia mabucha ya nguruwe ingawaje utetezi ulikuwa kwamba, wao kama wao hawakuwa wakipinga uwepo wa hizo bucha bali walikuwa wakipinga uwepo wa bucha hizo kwenye maeneo yenye mchanganyiko wa watu, huku mengi yake yakiwa kwenye maeneo yanayokaliwa na Waislamu wengi hapo Magomeni na Manzese, huku wakidai hiyo ilikuwa ni kinyume hata na sheria zenyewe (bila shaka za mipango mji), na wakazi wa huko walipojaribu kulalamika, serikali iliwapuuza na ndipo watu wakachukua sheria mkononi!

Nakumbuka siku anayoisema Mohammed Said hapo juu, nilikuwa naenda pale Central alipokuwa Bi Mkubwa hata hivyo kufika Posta ya Zamani nililazimika kugeuza manake Posta yote ilikuwa imetanda magari ya polisi waliobeba silaha za kivita!

Uzoefu wangu wa kuishi Kota za Polisi haukusaidia kunipa ujasiri wa kutowaogopa polisi wale manake ilikuwa ni kama Uwanja wa Vita!!

Huyo Sheikh Kassim Bin Juma sie wengine ndo tulianza kumfahamu kupitia tukio hili! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, movement mzima ilikuwa inaendeshwa na BALKUTA iliyokuwa chini ya Sheikh Yahya Hussein.

Sina uhakika wa uhusiano wa Sheikh Kassim na BALKUTA lakini nisicho na shaka nacho ni ushawishi wake mkubwa aliokuwa nao pale Msikitini kwa Mtoro!

Hii BALKUTA ilikuwa mwiba mkali kwa serikali... cjui ilifia wapi lakini nadhani ilipigwa ban na serikali, manake kwa jinsi ambavyo ilikuwa na ufuasi mkubwa hususani wa vijana, I doubt kama ingeweza kufa yenyewe!

Bila shaka Mohamed Said atakuwa analifahamu vizuri hili suala na kuweka kumbukumbu isiyo shaka sawa! Na kama kweli ilifutwa na serikali basi sina shaka moja ya taasisi ambazo zilifanya sherehe kutokana na kufutwa huko basi ni BAKWATA ambayo wakati ule ilikuwa chini ya Sheikh Hemed bin Juma bin Hemed!!

BAKWATA ilikuwa inanyimwa sana usingizi na BALKUTA!!

Hizi movements za Sheikh Ponda si lolote si chochote mbele ya BALKUTA manake hata mapinduzi kwenye misikiti ili kuondoa ma-Imam wa BAKWATA, kama sikosei movement za aina hiyo ziliasisiwa na BALKUTA, na kufutwa kwa BALKUTA ndiko kukaja kuibua akina Sheikh Ponda!!

Anyway, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Tanzania, hususani Dar es salaam!!!
 
Mhenga mwenzangu umeeleza vizuri sana, naomba kuongezea kidogo sana ili nisiharibu uliyasema; Sheikh Kasim alikua member wa Balkuta na hata kile kikundi kilichokua kinasema Yesu sio mwana wa Mungu nadhani na chenyewe kilikua ni zao la hao hao Balkuta, kiliwahi kumsilimisha kijana mmoja wa Kiluteli ambaye wao walikua wanamwita "askofu Mwaipopo", huyo dogo aliishiwaga ada ya shule alikua akisoma siminari moja kule Tukuyu; anyway back to the topic; baada ya hilo tukio, vijana kadhaa waliongoza uvunjaji wa mabucha yale walikamatwa na kuwekwa lock up, kesi ikawa inaunguruma Kisutu, wakili wao alikua Musa Kwikima (nadhani kafariki mwaka hu mwezi April, habari zake zipo humu jukwaani ). Namkumbuka kijana mmoja (ki umri nadhani alikua ananizidi mimi so ni makosa kumwita kijana ) anaitwa Rashid Idd Athuman Njeja, vijana wa sheikh Kassimu aliyehitimu elimu nyingi za dini, huyu "dogo" ndiye aliyeongoza hasa uvunjaji ule wa yale mabucha. Kwasasa wengi wa hao watu ni RIP. Well, kilikua kipindi kigumu sana kwa Tanzania hasa jiji la Dar kama ulivyo sema.
 
Asante sana mkuu Chige hapo juu. Mimi JF inanieleimsiha nina list ya watu wa kuita kulingana na uzi. Wakitaja magari, historia, vita, ndege, Zanzibar, mahusiano, habari za mjini, wizi na utapeli kote uko najua nani aje kuongezea na mara nyingi hakosi neno.

Sasa nikajua mambo ya VPN tena umekosa maana nimezoea kwenye nyuzi hizi unatinga bila kuitwa, tena mapema sana.
 
Back
Top Bottom