Maandamano ya kupinga dowans na ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya kupinga dowans na ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tanganyika2, Oct 26, 2011.

 1. T

  Tanganyika2 Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimehudhuria kikao cha haraka cha Waandishi Habari na wawakilishi wa Asasi za kiraia, Serikali za wanafunzi wa Vyuo Vikuu, wawakilishi wa wananchi wa kawaida na wadau wengine kutangaza rasmi maandamano ya nchi nzima jumamosi hii 29 oktoba 2011 kuanzia Ubungo mbele ya ofisi za Tanesco hadi viwanja vya Jangwani. Waliokuwepo kuwasilisha taarifa ni pamoja na viongozi wa DARUSO, Chuo Kikuu cha IMTU, CBE, Bw. Kahoho (raia binafsi), NGOs kadhaa na Harold Sungusia na Marcossy Albanie wa Kituo. Hii hapa ndo Taarifa rasmi::
  ========================
  [FONT=&quot]AP 2000[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot][/FONT]

  DARUSO DATA

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
  MAANDAMANO YA KUPINGA SERIKALI KUILIPA DOWANS Sh. BILIONI 112.67
  [FONT=&quot]Novemba, 2010 Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishiya Migogoro ya Kibiashara (ICC) ilitoa tuzo dhidi ya Tanesco kuilipa Dowans shillingi billion 94. Jambo hili liliibua hisia na hasira miongoni mwa wananchi kwa kulalamika na kupinga ulipaji huo wa fedha za umma kwa kampuni tata - kutokana na taarifa za kamati teule ya Bunge.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Baada ya tuzo hiyo watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mawakili wa Tanesco walipinga mahakama kuu kusajili tuzo hiyo. Mnamo Septemba 28, 2011 Mahakama kuu ilitoa uamuzi wa kusajili tuzo hiyo na kuamuru Tanesco ilipe shillingi billion 94 na asilimia 7.5 ya gharama hizo. Hata hivyo kabla ya usajili wa tuzo hiyo, Dowans iliuza mitambo husika kwa kampuni ya Symbion Powers kinyume cha taratibu kwa kuwa kulikuwa na amri ya mahakama ya kuacha hali ya mitambo ibaki kama ilivyo. Cha kushangaza ni jinsi ambavyo Serikali ilikuwa mstari wa mbele katika kuingia mkataba wa uzalishaji wa umeme na Symbion Powers kwa gharama ya watanzania hali ikijua mitambo hiyo iko kwenye mgogoro uliopo mahakamani.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Kwa kuzingatia haya, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Asasi kadhaa za Kiraia na Wanaharakati wa Haki za binadamu tulitoa tamko tarehe 11 Oktoba 2011 kuitaka serikali kuchukua hatua ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa bila mafanikio. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Kwa kuwa serikali imeamua kudharau maoni yetu, na kwa kuwa kuna kila dalili za serikali kuilipa Dowans fedha za wananchi, sisi, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, serikali wakilishi za wanafunzi wa Vyuo Vikuu na raia wa kawaida wa Dar es salaam tunaitisha maandamano kwa kratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu siku ya Jumamosi tarehe 29/10/2011. Kwa hapa Dar es salaam, maandamano yataanzia Ubungo, mbele ya zilipo ofisi za Makao makuu ya TANESCO hadi Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 2:30 asubuhi.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Maandamano haya yanalenga kuitaka serikali kufanya yafuatayo:-[/FONT]
  1. [FONT=&quot]Kutokuilipa kabisa Dowans kwa kutumia hela za walipa kodi wa Tanzania. [/FONT]
  2. [FONT=&quot]Itoe maelezo ya kina kwanini ilipuuza ushauri wa kisheria wa kuvunja mkataba na Richmond toka awali kwani kwa mujibu wa washauri wa kimarekani [/FONT][FONT=&quot]Hunton & Williams LLP wakati Tanesco inaingia mkataba na Richmond Dev’t Co. Kampuni hiyo haikuwa imesajiliwa achilia mbali kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake chini ya mkataba huo.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  3. [FONT=&quot]Itekeleze kwa dhati maazimio 23 yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mlolongo mzima unaopelekea mpaka sasa tutakiwe kulipa Shilingi 112,671,222,611.36. Kwa kufanya hili Serikali pia ituthibitishie kuwa itaacha kabisa kukikosea heshima chombo ambacho ni kisemaji na wakilishi wa wananchi kupitia wabunge.[/FONT]
  4. [FONT=&quot]Kama sheria za kimataifa zinatubana kulipa deni hili basi malipo haya yafanyike kwa kuuza mali za wale waliotusababishia kadhia hii na kwamba malipo ya kuilipa dowans yafanyike pale tu serikali itakuwa imeshawachukulia hatua kali wahusika wa kadhia hii. Umma ni lazima ujiridhishe kwa kuona hatua hizo zinachukuliwa.[/FONT]
  5. [FONT=&quot]Kuchukuwa hatua ya kinidhamu kwa wale wote walioshiriki katika kuingiza serikali katika mkataba huu hata mawakili waliotoa ushauri huu.[/FONT]
  6. [FONT=&quot]Serikali ipeleke Bungeni muswada wa utaratibu mzuri na sahihi wa kushirikisha wananchi na hata wabunge katika kuingia mikataba ya kimataifa na serikali ili kuepusha hali kama hii kutokea.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Kwa hiyo tunatoa wito kwa watanzania wote tuadhimishe kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kutenda yafuatayo:-[/FONT]
  1. [FONT=&quot]Tujitokeze kwenye maandamano ya amani na kupinga ufisadi na malipo ya kifisadi ya Dowans siku ya Jumamosi, tarehe 29 Oktoba 2011.[/FONT]
  2. [FONT=&quot]Kuvaa nguo za maombolezo, nyeusi, kama ishara ya maombolezo tukikumbuka msimamo wake wa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, [/FONT]
  3. [FONT=&quot]Tuzitumie siku za ibada za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili zote ndani ya muda huu, kumuomba Mungu atujalie Uzalendo na Ujasiri wa kuitetea nchi yetu, kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mwisho, tunaomba walipa kodi (wananchi) wote ambao hawajapendezwa na mlolongo huu unaopelekea ulipaji wa deni hilo la Dowans na ufisadi mwingine wote kuwa na uthubutu na kujitokeza kwa wingi kusimamia kile ambacho wanaona ni haki na stahili ya wananchi wote na taifa letu kwa ujumla. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa niaba ya asasi za kiraia nchini Tanzania zinazopigania haki na kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za Umma.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  he he hatukosi
   
 3. e

  emrema JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  soildarity forever.................................!
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jamani, hawa asasi za kiraia walitangaza tuvae nguo nyeusi siku ya 'Nyerere Day' kupinga malipo kwa Dowans, mimi nikavaa kwenda kazini, matokeo yake nikajikuta ni 'black' peke yangu kuanzia nyumbani, njiani hadi kazini. Tunaomba J'mosi wasitutose, nitaandamana pia.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hayo maandamano yasishie Dar tu, ni vizuri yangefanyika nchi nzima.
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kibali kimeshapatikana?
   
 7. T

  Tanganyika2 Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi unataraji kibali toka kwa nani?? Hawa Polisi wanatumwa na wale waliotuibia, halafu wao watoe kibali cha kupinga mambo ya mgao??
   
 8. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  sheria inasema toa taarifa nt kibali
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Kwa vile kila maandamano yaliyoanzishwa na cdm, cuf, tawla, nk yameonekana kama aina ya uchochezi wa kisiasa, napendekeza hizi taasisi zitumie maandamano haya ya TANESCO (kwa kuwaunga mkono) kuhamasisha wananchi kuwasupport ili yawe na matokeo mazuri. Ninachojua, endapo Watanzania (Waliochoshwa na ufisadi tu) watajitokeza kwa wingi kuwaunga mkono TANESCO nchi nzima inaweza kuwa na mwangwi mzuri kwa hawa watawala waliojisahau.

  Pia waandaaji wa maandamano haya (TANESCO) wachukulie hili wazo kama lenye nia nzuri na wafanye maandalizi mazuri tu kwa kuto mawasiliano (instant communication) mazuri kwa watakaotaka kuwaunga mkono. Wanaweza kufungua internet blog (facebook, jf, twiter nk) na kutoa namba za simu kwa ajili ya instructions ya je yatakuwa lini, sehemu tutakazo kusanyika, njia, ajenda nk

  Endapo hili likifanikiwa litasaidia Watanzania kuacha kulalamika lalamika bila kufanya chochote kutatua matatizo yao. Mwenye mawazo tofauti, tafadhali yalete.
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 5,361
  Trophy Points: 280
  mimi siandamani,.waandamane sitta na mwakyembe walioficha ukweli eti kuinusuru serikali yote isianguke...
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nimekusoma mkuu, points kama hizi tunazisahau katika kutafuta suluhu ya matatizo yetu na matokeo yake tunaishia 'kuzunguka mbuyu'
   
Loading...