Tuko njiani kwa baadhi ya makamanda tunaenda kukutania tulipokubaliana
KUZUIA MAANDAMANO KWA KUPIGA WANAHABARI,NA KUTUMIA MBWA NI SOWETO STYLE
Wakati baadhi ya mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuanza kutekeleza agizo la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, agizo alilolitoa kama maadhimio ya mkutano mkuu, kuandamana nchi nzima pasipo kikomo, Jimbo la Musoma maandamano hayo yalianza kufanyia tangu ukawa walipotoka bungeni kabla hata viongozi wa juu kutoa tamko hilo.
Hayo yamesemwana na Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini, Vicent Nyerere alipokuwa akizungumza na Kwanza jamii/Mjengwablog kwa njia ya simu.
"Tumekemea wao (askari) kutumika kwa maslahi ya ccm, ila wanatakiwa kulinda raia wote wa vyama vyote na wasio na vyama, hata wasio raia wanaoishi kisheria" Alisema Nyerere
Nyerere alisema kuwa Dhamira ya mikutano imelifanya jeshi la polisi kutozuia mikutano ya CHADEMA mkoani Mara kwa kuwa hujadili mustakabali wa nchi hivyo hakuna maandamano ambayo yamewahi kuzuiwa lakini pia alieleza kuwa tangu maandamano hayo yalipoanza hakuna fujo iliyowahikutokea.
Nyerere alisema kuwa jana ulifanyika mkutano katika Kata ya Nyamatare, Jimboni Musoma mjini, ambapo Askari waliruhusu kuendelea kwa mkutano huo kwa Amani, kwani hata wao wanajua dhamira sio fujo ila kupeleka ujumbe.
Hata hivyo amesikitishwa na kuzuia maandamano ya amani badala ya kulaani uhalifu, mauaji, uporaji hivyo kulaani wanaodai haki jeshi hilo litakuwa limetoka nje ya mstari.
Sambamba na hayo Pia amelaani vikali kuendelea kupigwa kwa waandishi Wa Habari, huku akitolea mfabo wa tukio lililotokea hivi karibuni na kusema kuwa waandishi hao walikuwa kazini kutimiza wajibu wao.
"Kikubwa zaidi hawakuwa na silaha zinazoashiria hatari kwa raia Mali wala askari, hivyo kitendo cha kutumia mbwa kwa raia ni Soweto style iliyotumiwa na makaburu, Kwa nchi inayoyawala ni aibu kwa raia wake hasa wenye imani ambayo mbwa si rafiki wa Imani Yao.
Nyerere aliongeza kuwa Busara, Hali halisi ya elimu, weledi ndo kiwe Kigezo cha kupanda cheo, sio ukakamavu kama unavyofanywa na jeshi la polisi hii leo.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua kuwa wataandamana kuelekea wapi, Nyerere alisema kuwa "Maandamano yanafanyika lakini hapa hatuna mkuu Wa mkoa alifariki na hawajateua, hivyo hatuna wa kumpelekea ujumbe kwa sasa kwahiyo Hilo bado ni changamoto kwetu na lipo kwenye mijadala na Viongozi" Alisema Nyerere
Hakuna asiyetambua kwamba hivi sasa kuna chama kipya cha ACT hapa nchini, Nyerere alisema kuwa hakijui hicho chama anasikia tu radioni na Musoma chama hicho hakipo, hivyo kwa baadhi ya mikoa ambapo kipo kipimo halisi kitaonekana kwenye chaguzi.
"Hivi mwandishi hicho chama kwani kipo wapi maana hapa Musoma hakipo sasa kwa mikoa mingine nasikia tu redioni, hivyo kipimo kizuri itakuwa katika uchaguzi mkuu, hivi umetumia kigezo kipi kinachoonyesha kwamba chama hicho kipo na kinaungwa mkono" Alihoji Nyerere.