Maandamano ya CHADEMA Mara

Hii safi, sasa wandugu tusiseme Mara ndo wanajua kupigana na polisi hivyo tuache hii vita kwao. Huu moto unatakiwa ukue nchi nzima. Viongozi wa Chadema mikoani jipangeni maana tunataka mkwere aanguke tena
 
Its time for a change, Chadema nchi nzima itisheni maandamano kupinga hayo ya arusha, bei za vyakula, bei za umeme, malipo feki ya Downs na migomo vyuoni kumtaka JK aachie ngazi kwa kushindwa kazi. Tusilale muda ndo huu wa kuiokoa nchi.
 
tunahitaji na mikoa mingine iitishe au angalau itoe tamko maana an injury to one is an injury to all
 
Vijana wa Chadema wataka maandamano nchi nzima Tuesday, 11 January 2011 20:41

Salim Said
SIKU chache baada ya kutokea vurugu huko Arusha na kugharimu maisha ya watu na uharibifu wa mali, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limekiomba chama hicho taifa kutangaza maandamano ya nchi nzima kupinga na kudai mambo mbalimbali kwa maslahi ya umma.

“Tunakiomba Chadema taifa kitoe tamko zito ili kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wote waliohusika na pia uchaguzi huo wa Arusha unarudiwa,” alisema Katibu wa Kamati ya Taifa wa Bavicha, Ally Chitanda katika taarifa yao kwa vyombo vya habari.

Chitanda aliongeza kuwa, “Sisi tuko tayari kushajihisha vijana nchini kushiriki katika maandamano yatayoitishwa na chama nchi nzima, kwa ajili ya suala hili na kuunganisha nguvu ya umma katika mambo mengine yanayoligusa taifa,” alisema Chitanda.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kupandishwa kwa bei ya umeme, jaribio la kutaka kuilipa kifisadi kampuni ya Dowans, maslahi ya wanafunzi na madai ya katiba mpya.

Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) taifa limelitupia lawama jeshi la polisi nchini kwamba limefanya vurugu na mauaji mjini Arusha kwa maelekezo ya serikali ya CCM, chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

Wakati huohuo Bavicha ililaani mauaji na vurugu za Arusha sambamba na kueleza kusikitishwa kwao na tamko la Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) kwa vyombo vya habari lenye mwelekeo kuunga mkono vitendo vya mauji na vurugu hizo.

Chitanda alisema hajashangazwa na kauli hiyo ya UVCCM kwa kuwa lilitolewa na Ridhwan Kikwete ambaye pia ni mtoto wa Rais Kikwete.

“Vurugu na mauji hayo yamefanywa kwa ajili ya manufaa ya CCM na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa Desemba 31 mwaka jana,” alituhumu Chitanda.

Chitanda alisema Rais Kikwete alionyesha kukwerwa na migomo na maandamano yanayofanywa na vyama vya siasa na wadau wengine nchini kupinga au kudai mambo mbalimbali.

Rais Kikwete aliyasema hayo siku chache baada ya vijana wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kufanya maandamano ya kudai haki zao za msingi, Chadema na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) nao kutangaza maandamano ya kupinga matokeo ya umeya Arusha na ongezeko la bei ya umeme.

“Hivyo UVCCM wametoa tamko kwa lengo la kukisafisha chama chao na mwenyikiti wao wa taifa ambaye pia ni mzazi wa mmoja wa waliotoa tamko hilo,” alisema Chitanda na kuongeza:

“Hata hivyo imetulazimu kutoa tamko kutokana na lugha ya utovu wa maadili waliyoitumia ambayo imepingana na kauli za viongozi wa dini ambao wametoa kauli za wazi za kukemea matukio ya Arusha yaliyofanywa na jeshi la polisi.”

Chitanda alisema wamefadhaishwa na UVCCM kuupotosha umma wa Watanzania kwa kueleza kuwa, viongozi wa Chadema wamefanya vurugu wakati ushahidi unaonyesha wazi kwamba polisi kwa manufaa ya CCM ndio waliofanya vurugu hizo.

“Ushahidi wa mikanda mbalimbali ya vituo vya ndani ya nchi yetu vya televisheni umeonyesha wazi kuwa, polisi walikuwa wakiharibu mali kwa kuvunja vioo vya magari na lipo jengo lililochomwa moto kutokana na kutupiwa bomu la machozi,” alisema Chitanda.

Alisema Bavicha inafahamu kuwa viongozi wa Chadema hawafanyi maandamano kujitafutia umaarufu kama ambavyo UVCCM imewatuhumu kwenye tamko lao; bali wanatimiza wajibu wa kidemokrasia wa kudai haki na kutetea maendeleo kwa kutumia nguvu ya umma.
 
Kampeni za uchaguzi wa 2015 ndiyo zimeanza rasmi...........kwa sababu washindi wa uchaguzi wa 2010 ni wezi wa kura na hatukuwachagua kwa hiyo inabidi tuanze mapema mikakati ya kulikomboa taifa hili kwenye ukoloni mambo leo wa CCM.............
 
Wapinge na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kupewa kifuta jasho cha 40 milioni kila mmoja kwenye mafao yao ya hitimisho la kazi.
 
kuisha kwa uchaguzi ni mwanzo wa kampeni za uchaguzi ujao. CDM 2015 kidedea
 
Huyo ally chitanda ni ndugu ya yule ***** kule arusha?
mary chitanda au?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, kimeitisha maandamano makubwa utakaohusisha mkoa mzima kupinga kile walichokiita vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za raia vilivyofanywa na Jeshi la Polisi mjini Arusha.

Kwa mujibu wa Chadema Mkoa wa Mara, maandamano hayo yatalenga kupeleka ujumbe kwa taifa na dunia kulaani vikali hatua ya jeshi hilo kutumia nguvu kubwa, ikiwamo risasi za moto na mabomu ya machozi kuzima maandamano yaliotishwa na chama hicho hivi karibuni mjini humo.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Nyanza Sibitali, aliliambia Nipashe mjini hapa kuwa maandamano hayo yatafanyika Jumamosi wiki hii yatakayohusisha majimbo saba ya uchaguzi ya mkoa wa Mara na kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kupeleka ujumbe huo.

Alisema Mkuu wa Mkoa ndiye anayetarajia kupokea maandamano hayo kisha kupokea ujumbe huo ingawa alisema bado hawajampata mkuu huyo wa mkoa kumweleza uamuzi huo.

Chanzo: Nipashe
 
ninawaunga mkono MARA na nawatakia maandamano mema na ya amani.
MUNGU ibariki TANZANIA,MUNGU ibariki CHADEMA na watu wake AMEN.....
 
aiseee,so this year ni maandamano tu yani!
Anyway,ndo njia pekee ya serikali kuwasikiliza wananchi
 
Moto waliouanzisha CCM sijui watuweza kuuzima, unaweza kuanzisha moto ukitegemea utachoma magugu ya shamba lako tu lakini ghafula upepo ukaja na moto kurukia shamba la jirani patashika hapo.
 
Kama itawezekana kuaanda ya Nchi Nzima - Natumaini watawala watafahamu fika kuwa Watawaliwa wamechoka -

Refer Signature ya Dark City:

WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE........

 
Huko kwa kina mura soksi itavuka kiatu kitabaki wakishasema mang'ana gasarikire pitia mbali kabisa.
 
Dah mwaka huu JK analo. Jana alikuwa kanuna kapoza hata lile tabasamu lake. Akiisikia na hii ndio kabisaa atazidi kukonda!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom