Maandamano ya CHADEMA Mara

Duh, hapa patachimbika. Polisi Mara wana kazi nzito. Wataua wengi huko, maana wale jamaa hawaogopi kitu wala polisi wa IGP na JK.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, kimeitisha maandamano makubwa utakaohusisha mkoa mzima kupinga kile walichokiita vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za raia vilivyofanywa na Jeshi la Polisi mjini Arusha.

Kwa mujibu wa Chadema Mkoa wa Mara, maandamano hayo yatalenga kupeleka ujumbe kwa taifa na dunia kulaani vikali hatua ya jeshi hilo kutumia nguvu kubwa, ikiwamo risasi za moto na mabomu ya machozi kuzima maandamano yaliotishwa na chama hicho hivi karibuni mjini humo.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Nyanza Sibitali, aliliambia Nipashe mjini hapa kuwa maandamano hayo yatafanyika Jumamosi wiki hii yatakayohusisha majimbo saba ya uchaguzi ya mkoa wa Mara na kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kupeleka ujumbe huo.

Alisema Mkuu wa Mkoa ndiye anayetarajia kupokea maandamano hayo kisha kupokea ujumbe huo ingawa alisema bado hawajampata mkuu huyo wa mkoa kumweleza uamuzi huo.

Chanzo: Nipashe

I hope this time the Police force will allow common sense and wisdom rather than force and thurgery to prevail.
 
Dar Mpo? Moro Mpo? Mbeya Mpo? Iringa Mpo, Mwanza Mpo? Kigoma Mpo, Dodoma Mpo? Kweli Tuonyeshe Mapenzi kwa Taifa Letu. Wakati Umefika na Nguvu Tunazo. Twendeni Pamoja Tukawaunge Wote Waliopigwa Risasi Sasa ni Arusha, Mbeya na Shinyanga. "Mashujaa Waliouliwa ni Kupigania Haki ya Watanzania Wenzao ya Katiba, Ukweli wa Dowans, EPA, Uchaguzi na Mengi" Twendeni Pamoja Kuibadisha Nchi Yetu ...
 
Riziki haivutwi kwa kamba ndugu!!!. Hata hivyo sie hatumo kwa sasa, zamu yetu ikifika nasi tutakuwemo!!!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi.

Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya.

Katika madai hayo, Mbowe alitangaza msimamo mkali wa kutaka mashitaka yote yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa chama hicho - wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi - yafutwe bila masharti yoyote, vinginevyo hawatahudhuria mahakamani tena, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani.

TUTAFIKA?

KWANI KATIBA MCHAKATO SI UMEANZA NA UNAENDELEA?

KUTOFIKA MAHAKAMANI: WAPI UTAWALA WA SHERIA?

HII SIO KUTAFUTA SHARI?

Wow, So Mara people don't value their lives?! Oh, never mind , I forgot they always mutilate(circumcise) girls, beat to death their wives and girl friends.

They do, thats why they are able to fight for it. But for you coward, you dont thats why everybody can play with you. The goverment who let corrupted figures steal everything which could be used to supply medicine, water, and reduce death tolls through diseases beats everybody to death.
 
Mwema chondechonde zile taarifa za kiinteligensia zipuuze kwani hazitofautiani na umbea. Waache waandamane tushuhudia wanachokifanya.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi.

Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya.

Katika madai hayo, Mbowe alitangaza msimamo mkali wa kutaka mashitaka yote yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa chama hicho - wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi - yafutwe bila masharti yoyote, vinginevyo hawatahudhuria mahakamani tena, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani.

TUTAFIKA?

KWANI KATIBA MCHAKATO SI UMEANZA NA UNAENDELEA?

KUTOFIKA MAHAKAMANI: WAPI UTAWALA WA SHERIA?

HII SIO KUTAFUTA SHARI?

Acha kudanganya umma wewe, hawakusema hawataenda mahakamani sana sana ni waliwaomba wananchi wa Arusha kufika siku kesi yao itakaposomwa yaani tarehe 21-1-2011
 
Acha kudanganya umma wewe, hawakusema hawataenda mahakamani sana sana ni waliwaomba wananchi wa Arusha kufika siku kesi yao itakaposomwa yaani tarehe 21-1-2011

Crashwise, kuna mtu alichakachua lile tangazo lililotoka kwenye gazeti ndivyo linabyosema kwamba hawatakwenda mahakani tofauti na lile tamko alilotusomea mbowe kwenye mkutano.
 
Mpaka sasa naamini serikali imejua kuwa huwezi kuwanyima watu haki ya kujieleza,,mda umafika wa watu kujua kuwa polisi au jeshi si kitu mbele ya sauti ya umma,hiki kinachotokea kilishatabiliwa siku nyingi na hayati Nyerere bt CCM ni viburi 2,nw its payback time..
 
Back
Top Bottom