Maandamano ya CHADEMA Jiji la Mbeya-Picha na Matukio

@Mlengo wa Kati, Assume for the sake of this argument that CDM is indeed Chama cha Demokrasia na Maandamano. Labda nikuulize, nani hasa ni CHADEMA? Mbowe?, Slaa?, Lema au mtu mmoja mmoja? Ni kwanini watanzania vijana kwa wazee, wake kwa waume, wanaacha shughuli zao na kufuatana na hiki Chama cha Demokrasia na Maandamano, tena kwa maelfu? wamepagawa? ni wajinga hawa watanzania?

CCM wanaweza kuwa na monopoly ya DOLA lakini kamwe hawawezi kuwa na monopoly ya wisdom. Chadema is not just a political party, it is a movement to put an end to all the lies, mass failures, looting,nightmares created by a group of individuals who thought they had the title deed to do as they wish! In short Chadema is vision of what Tanzania should be and what it can be. Watu wanaojitekeza kwenye hayo maandamo (bila fuso) wanajitekeza kwa jambo moja tu - nalo ni, mubadala:)

Well said JFM and message sent !
 
Wakuu,

Hivi sasa ndio tunajipanga ili kuanza Maandamano yetu. Mji umejaa hamasa kubwa kila ukipita bendera za CHADEMA na ishara ya vidole viwili ndio vimetawala.

Watu wamependeza sana na Kombati na Sare nyingine za Chama. Tunatarajia kuanza Maandamano mida ya saa sita. Magari yote ya msafara yako hapa Forest yakipiga nyimbo mbalimbali za chama. Maandamano yanatarajiwa kuanza maeneo ya Mafiat njia ya Uwanja wa Ndege yataelekea Viwanja vya Ruandanzovwe Mwanjelwa.

Leo tutatembea Kilomita Mbili tu.

Pata picha za Awali.

Umati.jpg

mabango-mbeya.jpg

maandalizi.jpg

gamba.jpg

nyomi.jpg


Aluta Continua
Kutoka Mbeya Forest

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Asante Waziri Kivuri kwa kutujuza nakupa BIG-up
 
Yaani inatia hata RAHA. Yuko jamaa yangu mmoja aligombea uraisi pale CBA kwa kivuli cha CCM aligarazwa vibaya sana na mwenzie aliyeshindana naye kwa kivuli cha CHADEMA. Safi sana CHADEMA. CCM inachukiwa na kila mtu... hata mtoto aliyezaliwa leo.
 
1. Watu wamelimika.(kidarasa na kujua haki na wajibu wao)
2. Ccm ya leo sio ile
3. Chadema wapo makini.
4. 75% ya wapiga kura ni vijana na wengi hawakupiga kura 1995 walkikuwa hawa jazaliwa au hawajafikisha umri wakupiga kura
5. Hakuna kijana anayeshabikia ccm.
6. Ufisadi upo wazi hta ccm wanakiri hadharani.
7. Alipa kodi mulikuwa wachache leoi tupo wengi na tuna uchungu na kodi zetu!
8. Shule za kata.
9......
utandawazi unao unachangia sana kujua machafu yanayo fanyika tofauti na miaka ya 1995 leo hii tunajua kinachoendela mbeya hata kuliko walio mbeya kwa kutumia vi mchina vyetu kitu ambacho kama kilikuwepo 1995 basi waliofaidika walikuwa wachache....vyombo vya habari pamoja na kwamba vinabana lakini angalau tofauti na 95...kifupi anae jaribu kulinganisha 1995 na 2010 basi anapaswa kupimwa akili....
 
Wakuu,

Hivi sasa ndio tunajipanga ili kuanza Maandamano yetu. Mji umejaa hamasa kubwa kila ukipita bendera za CHADEMA na ishara ya vidole viwili ndio vimetawala.

Watu wamependeza sana na Kombati na Sare nyingine za Chama. Tunatarajia kuanza Maandamano mida ya saa sita. Magari yote ya msafara yako hapa Forest yakipiga nyimbo mbalimbali za chama. Maandamano yanatarajiwa kuanza maeneo ya Mafiat njia ya Uwanja wa Ndege yataelekea Viwanja vya Ruandanzovwe Mwanjelwa.

Leo tutatembea Kilomita Mbili tu.

Pata picha za Awali.

Umati.jpg

mabango-mbeya.jpg

maandalizi.jpg

gamba.jpg

nyomi.jpg


Aluta Continua
Kutoka Mbeya Forest

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Inatakiwa kuwepo na Elimu kwa umati huu wa kupiga kura kama tunavyoandamana,vinginevyo hakitafanyika kitu.
 
Namsikitikia mtu au watu ambao wanamaliza mda wao kwa kujenga hoja za kuitetea au kuisafisha CCM......ukweli ni kwamba mnabishana
na wakati na hamuangalii alama za nyakati....ccm haiwezi safishika hata kwa dodoki la chuma. Tukubali tukatae CCM inaumwa na iko mahututi ICU....wananchi wameshachimba kaburi la mgonjwa huyo na tunasubiri akate roho tuende kumzika. Mtaongeaweeee,mtaiteteaweeee,mtaisafishaweee,lakini mwishowe mtashindwa na mtachoka! Hakuna mtu wa kuzuia kifo cha CCM. Acha niitemee mate ccm....twuuuuuuuh....
 
Inatia moyo sana kuona watanzania wanaamka kwa kiasi hiki. kweli watanzania wa sasa hawadanganyiki.
 
Hata aliyemwapisha Gbagbo Ivory Coast, ndo amekiri jana kuwa aliyemwapisha mara ya kwanza hakuwa mshindi. jana ndo tena kashiriki kumwapisha mshindi halali. Naamini nawewe time will tell
 
MH chama sio serikali mbona unachanganya mambo.Hivi umesikia CDM inakusanya kodi wapi? Imesaini mkataba na mchimba mgodi gani? Halafu sheria ya manunuzi imetungwa na bunge kwa ajili ya serikali na ina maana yake haikutungwa kwa ajili ya watu binafsi wala vyama vya siasa, kwa hapo kila chama kina namna kinavyo nunua mali zake na matumizi ya hela zake.
 
Wewe ni hasara tupu. Kila hoja uliyoitaja CDM wana maelezo yake, wewe ulichoongea ni defence yako na CCM, kwanini usichallenge arguments zao unajichallenge mwenyewe?
 
Jana tarehe 06.05.2011 CHADEMA walifanya maandamano yao Mbeya yaliyoanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanja vya shule ya msingi ya Luanda – Nzovwe.

Maandamano hayo yalikuwa na nia ya kuishinikiza serikali mambo yafuatayo:
  1. Kuachana na muswada wa sheria ya ununuzi wa vitu chakavu
  2. Mchakato wa katiba uondolowe mikononi mwa CCM
  3. Kupinga upangaji vitu bei
  4. Uchaguzi meya wa arusha ufanyike upya

My take:

  • Kuhusu kupinga muswada wa sheria ya ununuzi vitu chakavu huku ni kuwahadaa wananchi, wao wenyewe CDM ndio vinara wa ununuzi vitu chakavu, kwa hiyo wanasema wasilo litenda, hii ni alama kubwa sana ya watu wanafiki. Mifano ipo, rejea mtafaruku wa kikao cha kamati kuu 30.04.2011
  • Mchakato wa katiba hauko mikononi mwa CCM, uko bungeni hivi sasa. Na watu wamepewa fursa ya kusoma muswada wa marekebisho ya katiba na watoe maoni yao. Sasa kusema uko kwa CCM huku ni kuwahadaa wananchi. Na bunge ni la wananchi, sasa kama CDM wabunge wake ni wachache hilo ni shauri lao kwani wananchi waliwachagua wachache kwa vile hawakukubalika, na wakaipa CCM ushindi wa kishindo wa urais na wabunge, wajipange 2015
  • Suala la upandaji vitu bei, hilo haliihusu Tanzania tu kwani sio kisiwa. Tunaona sehemu mbali mbali na nchi nyingi vitu vimepanda bei. Sasa ukisema ushuru ushushwe, serikali itapata wapi mapato ya kutekeleza majukumu yake ?. Hili laonyesha CDM wanataka serikali itekeleze sera yao ya kuwapa watu vitu vya bure bure bila kufanya kazi, hili halitekelezeki
  • Uchaguzi wa meya wa arusha ulitolewa maelezo ya kirefu na ufasaha na Mh. Waziri mkuu pale bungeni, kuwa ulikuwa ni huru, haki na wa halali. Kama CDM wanapinga waende mahakamani. CDM wakaanza kurudi kinyuma nyuma na kuipigia magoti serikali kwa kutaka mazungumzo. Mazungumzo yamefanywa na yanafikia ukingoni ambapo CDM wameomba wapewe nafasi ya unaibu meya kwa miaka 4, na TLP wapewe nafasi hiyo kwa mwaka 1. Suala la umeya , CDM wao wenyewe wamekubaliana nalo kuwa ni la CCM. Sasa kelele za nini , na mmeomba mmepewa

Kama dhumuni la maandamano lenyewe lilikuwa ni kuzungumzia mambo hayo ambayo , basi CDM wamepotoka na inaonekana si watu wa kuwaamini kabisa, na wanapoteza pesa wanazo pewa za kodi ya wananchi kama ruzuku kwa vitu tayari vinafanyiwa kazi na wao wakiwa ni sehemu ya utekelezaji. CDM tumieni ruzuku vizuri, kwani mikoani na wilayani ofisi hazina vitendea kazi, watu hawana mishahara na ofisi zinaendeshwa kwa pesa za mifukoni za viongozi, hamtofika kiivyo. Na mie naanza kuamini sasa kuwa ' SAA YA UKOMBOZI KUMBE SI SASA , BADO IKO MBALI SANA KWA MTINDO HUU'.

thrown to recycle bin....
 
Back
Top Bottom