Chadema haitafuti haki, haki ipi mnayoitafuta na mlionyimwa? mmedai katiba, hewala. Mnauza vibinti chini ya umri pale Bili, hewala. Mnapora wake za watu, hewala.
Sasa, mnaiba na kuharibu mali za raia na kuhatarisha maisha ya wananchi na wageni hapo Arusha, halafu mnasema historia ya kutaka haki? Hivi mnajuwa mnachokifanya? Hakuna mTanzania mwenye akili timamu atae-waunga mkono kwa hili.
Nyie mnafikiri mkikaliwa kimya na Serikali ni kuwa inawaogopa? Sasa mtakiona.
Labda kama umeanza kufuatilia siasa 2006, hii hali sio mpya na haijavunja bado record ya matukio makubwa zaidi yaliyopata kutokea, na Chadema wanawajibika pia kwa upotevu wa mali za raia wema na usumbufu usio wa lazima uliotokea leo.
huo ni mwanzo wa safari wandugu... ukishakuwa mpinzani basi hicho ni kitu cha kawaida. Kuna watu wameshauawa nchi hii na kutiwa kizuizini kwa muda mrefu sababu ya siasa, kuna watu wamelemaa na wengine walivunjwa mikono, sababu ni wapinzani.
Leo hii watu wamesahau yote hayo.... Hii ni kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu tulionao tunalichukulia kwamba ni suala kubwa sana.. je mwadhani ni halali kukiuka amri ya serikali hata kama ni ovu na hatua isichukuliwe? lazima tukubali kuheshimu utawala na watawala wake huku tukitumia busara za ziada kutatua matatizo tuliyonayo. napenda kuwakumbusha tena Serikali yoyote ile iwayo HAITISHWI bali HUTISHA. Je ikiwa hivyo ndivyo ni wangapi wanabaki nyuma ya Laptop zao kuwahamasisha wapumbavu wachache wafanye ujinga? Na mwisho wa siku wanaumia waliomo na wasiokuwamo.
Kesho mtu aende hospitali ya Mawezi na atajionea majeruhi wangapi watakuwa na pingu! (hali yenyewe ndio hii, kisha mtiwe vilema na hali wenye akili zao wanatanua na kusalimiana na hao mnaowaona kuwa ni adui zao!) Siasa za nchi hii.....:embarrassed: