Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa

Haiwezekani wanasiasa tu kwa sababu wanatetea haki ya wote kuwekwa lupango and this source is apparently true. Moshi arusha na tanzania kwa ujumla amkeni kwani sasa hivi we know our rights and democracy is getting spread all over. Mbowe, Selasini na Lema piganieni haki za wote na sio haki za chama cha chadema............ Lakini mbona wote wachaga tu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Leo nilisikiliza radio asubuhi, MAONI ya Watanzania wengi ni kuwa CHADEMA wamekosea kufanya maandamano na Watanzania wengi wamewalaumu viongozi wa chadema kutokuwa makini na kumwaga damu.

redio gani? Redio uhuru?
 
haya sasa kuna kikao kufikiria kuifuta chadema au kuisimamisha kwa muda usiopungua miaka mitano au nane !kifutwe tu,wanataka kutuletea rwanda hapa ?ustaarabu umewashinda !!:confused2:

taahira mwingine
 
Haya sasa kuna kikao kufikiria kuifuta Chadema au kuisimamisha kwa muda usiopungua miaka mitano au nane !Kifutwe tu,wanataka kutuletea Rwanda hapa ?Ustaarabu umewashinda !!:confused2:

Crap! Ths is poverty of thoughts, psychosis! What a shameful coment!
 
Kwanza ninalaani jeshi lka polisi arusha kwa kuwapiga watanzania wenzao waliokuwa wakiandamana kwa amani. Lakini watanzania tutambue kuwa hakuna kitu kizuri kisicho na gharama, tunasikitika kwa kuuawa na kujeruhiwa kwa watanzania wenzetu lakini hii pia ni dalili njema ya watanzania kuondokana na woga na kupigania haki zetu kwa nguvu zote.

Ukiona mateso yanazidi tambua ukombozi umekaribia. Ninaamini muda si mrefu watanzania tutayaondoa mafisadi ya madaraka hapa nchini. Wito wangu kwa watanzania wote kuungana katika vita hii safi, maana matokeo yake ni uhuru na haki
 
Hii inaonyesha na yeye alitumwa kwa sababu
  1. polisi walitoa kibali cha maandamano siku kadhaa kabla kwa maandishi
  2. Yakiwa yamebaki si zaidi ya masaa 12, IGP anafuta kibali hicho kupitia vyombo vya habari
  3. Alishindwaje kuwatafuta viongozi wa chadema na kukaa nao kikao kujadili dharula ya kiiteligensia iliyopo? Kwa sababu wenye uwezo wa kusitisha maandamano kwa ufanisi walikuwa ni viongozi wa chadema ambao ndio waliyaitisha. IGP kwenda kusitisha maandamano ambayo hakuitisha yeye ilikuwa ni kuwachanganya wananchi, na matokeo yake ni kuitia hasara serikali kwa nguvu kubwa iliyotumika kudhibiti raia wasio na hatia wala siraha
 
Hali hii haiwezi kuvumilika. Raia watanzania wanathamani kubwa sana. Si busara kwa viongozi wa siasa kuwashawishi raia kuvunja amri za serikali iliyo madarakani kisheria. Watanzania tuwe MAKINI na viongozi wachanga wasio na huruma na raia. Si kila kitu POLISI wanakosea. Kuna mengine watu wanataka wenyewe hasa kama busara haitumiki katika maamuzi.

Mbona sijawahi kusikia unawaonea watanzania wanaopoteza masha kwa uzembe, wizi,uonevu, kutojali kwa serekali,,,,,,Umeshakaa chini ukajiuliza ni Watanzania wangapi wanaopoteza maisha kwa kuuwawa na majambazi,,,,,,Hao polisi wako wapi,,,,,,,,Ni watanzania wangapi wanapoteza masiha kwa siku kwa ajali za barabarani,,,ili khali polisi wapo,,,,,,,,,,Umejiuliza ni watanzania wangapi wamepoteza maisha kwa kuuwawa na polisi haohao kwa kisingizio cha kwamba ni majambazi,,,,,,,,,,,,,,,,,,Ni wakinamama wangapi wanakufa kila siku kwa matatizo ya uzazi ambayo kwa nchi yenye umri wa miaka 50 ni laana,,,,,watoto wanaokufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 2 kwa uzembe wa serekali hiyohiyo ni wangapi,,,,,,,,,,,,watu wanaokufa kwa kukosa huduma za afya,,,,,,,,,,,,,ukiendelea ni idadi kubwa tena saana ya watu wenye hatia wanapoteza maisha kwa uzembe na kutojali kwa serekali hiyohiyo unayoitetea

Ni vema ungejiuliza kama nchi ni ya demokrasia watu kuandamana kwa amani ni kosa,,,,,,,kwanini haohao polisi hawatumii nguvu kama walizotumia jana kuzuia ujambazi au hata ajali za barabarani

Ulaaniwe mjinga wewe pamoja na kizazi chako chote
 
IGP Mwema alisema wamepata taarifa za kiintelijensia kuwa chadema wameazimia kuleta uvunjifu wa amani hivyo wamepiga marufuku maandamano! siku hizi wakitaka kufanya mambo ya kipuuzi kama waliyoyafanya Arusha wanasingizia 'eti taarifa za kiintelijensia'! Hivi hizo taarifa za kiintelijensia hazipatikani kwa majambazi na mafisadi ila kwa chadema tu?

Ni jambo la kushangaza sana kuwa polisi waliweza kupeleka askari wengi sana pamoja mabomu, siraha za moto na magari ya maji washa yakiwa yameenea mji wote Arusha hata kabla ya maandamano hayo kufanyika ili wayazuie!

Bwana mwema hivi huoni kuwa nguvu hiyo hiyo ingetumika kulinda hayo maandamano na yakamalizika kwa amani badala ya kuuwa ndugu zetu wasio na hatia? Are you really effective and efficient?

Kumbuka damu ya wasio na hatia huzungumza na sauti yake husikika. Hiyo damu utadaiwa mikononi mwako kama ile damu ya Habili ilivyomlilia Kaini mpaka ulipe wewe mwenyewe na waliokutuma.
Mkuu
CCM haijiamini kabisa. Kikwete anajua aliiba kura kuingia madarakani, hivyo wakiruhusu maandamano utawala wao dhalimu utangolewa kwani Watanzania kwa mamilioni wameshawachoka. Hii mambo ya taafarifa za liintelijensia ni uongo wao kama walivyokwisha zoea. Laana ya milele na iwaangukie na familia za kwa kumwaga damu ya watu wasio na hatia baada ya kushindwa kutawala kwa haki.
 
Hali hii haiwezi kuvumilika. Raia watanzania wanathamani kubwa sana. Si busara kwa viongozi wa siasa kuwashawishi raia kuvunja amri za serikali iliyo madarakani kisheria. Watanzania tuwe MAKINI na viongozi wachanga wasio na huruma na raia. Si kila kitu POLISI wanakosea. Kuna mengine watu wanataka wenyewe hasa kama busara haitumiki katika maamuzi.
HIVI WEWE UNAPOSEMA RAIA WA TANZANIA ..................... Slaa ni RAIA wa wapi.....??? ........... AU uraia wa Slaa umempa nani...........??? Mbowe ni raia wa wapi..........??? naye uraia wake umempa nani..........??? Tatizo lako unapoambiwa upeleke matokeo ya kipimo cha akili yako...utakuwa umepeleka matokeo ya choo kubwa
 
Kwanza ninalaani jeshi lka polisi arusha kwa kuwapiga watanzania wenzao waliokuwa wakiandamana kwa amani. Lakini watanzania tutambue kuwa hakuna kitu kizuri kisicho na gharama, tunasikitika kwa kuuawa na kujeruhiwa kwa watanzania wenzetu lakini hii pia ni dalili njema ya watanzania kuondokana na woga na kupigania haki zetu kwa nguvu zote.

Ukiona mateso yanazidi tambua ukombozi umekaribia. Ninaamini muda si mrefu watanzania tutayaondoa mafisadi ya madaraka hapa nchini. Wito wangu kwa watanzania wote kuungana katika vita hii safi, maana matokeo yake ni uhuru na haki

Tuendelee kutoa elimu ya uraia kama tulivyofanya kuhimiza uchaguzi 2010. Peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzz powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Ukombozi wa kweli hauji kwa kukaa na kuongea kwenye luninga na maredioni tu bali kwa kuonyesha vitendo. Hongera wanaArusha kwa kuonyesha njia nasi tu pamoja nanyi katika vita hivi.
 
Viongozi wa Chadema msifanye mzaha kwa yaliyo tokea Arusha kwani Ccm walisha sema wata tawala kwa gharama yoyote ile na sasa kauli yao ime dhihirika ,aliye jipachika umeya lazima atoke na hili hali hitaji majadiliano, swali la kujiuliza ikiwa wana diriki kumwaga dam kwa nafasi ndogo ya umeya je Slaa ange amua kudai ushindi wake alio porwa na JK nini kinge tokea? Kama kuna uwezekano walio husika wote wapelekwe ICC ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Gaza usijali huu ndio mwanzo mzima wa shughuli ya kuwaamsha watanzania.... sasa tunasonga mbele....
 
Jeshi la Polisi sasa linaipeleka nchi pabaya Wednesday, 05 January 2011 20:37
Mwananchi

igp-mwema.jpg

Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema.

Kwa mara nyingine katika kipindi cha wiki moja, polisi wamefanya vitendo vya kinyama na kihuni, zamu hii wamewashambulia na kuwajeruhi kwa silaha za kivita wafuasi wa Chadema waliokuwa wanaandamana kwa amani kuelekea katika Viwanja vya Unga Limited, mjini Arusha kwa ajili ya mkutano wa hadhara ambao viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa wahutubie.

Maandamano hayo, ambayo yalikuwa yahitimishwe na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ilikuwa ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa ushindi CCM kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni. Chadema pia ilikuwa itumie mkutano huo kutoa msimamo wake kuhusu madai yake ya katiba mpya yaliyoanzishwa na chama hicho kabla na baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika miezi miwili iliyopita.

Itakumbukwa kwamba Alhamisi iliyopita, polisi waliwashambulia kwa mabomu ya machozi, risasi za moto, virungu na maji ya kuwasha wafuasi wa Cuf waliokuwa wanaandamana kwa amani kuwasilisha rasimu ya katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani. Wakati wakifanyiwa unyama huo wa kutisha na polisi, waandamanaji hao wa Cuf waliendelea kuwa watulivu pasipo kujibu mapigo.

Katika vurugu zilizoanzishwa na polisi jana mjini Arusha kwa kujeruhi vibaya baadhi ya waandamanaji na kuwasweka rumande baadhi ya wabunge, akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wananchi katika Jiji la Arusha walipata hofu kubwa, huku wakikimbia hovyo bila kujua la kufanya kutokana na polisi kuonekana kudhamiria kuwakomoa waandamanaji.

Polisi hao walitumia nguvu kubwa kupita kiasi na hawakutilia maanani ukweli kwamba licha ya waandamanaji hao kutokuwa na silaha yoyote, pia walikuwa katika hali ya utulivu mkubwa. Kinyume na kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema aliyedai juzi kuwa jeshi lake lilikuwa na taarifa za intelijensia zilizodai kwamba iwapo maandamano ya Chadema yangeruhusiwa waandamanaji wangefanya vurugu, badala yake ni polisi ambao walianzisha vurugu kwa kumwaga damu ya watu wasiokuwa na hatia.

Ni jambo la kushangaza kwamba ingawa awali maandamano hayo yalikuwa yameruhusiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye ambaye alisema alitoa kibali hicho baada ya Chadema kufuata taratibu zote zilizotakiwa, kitendo cha IGP Mwema kujitokeza ghafla na kupiga marufuku maandamano hayo katika dakika za lala salama kinatia shaka na kuibua hisia kwamba pengine alifanya hivyo kwa amri na shinikizo la chama tawala. Vinginevyo, haiingii akilini kuona mkuu wa jeshi hilo kitaifa akiingilia taratibu zilizo ndani ya mamlaka ya kamanda wa polisi wa mkoa bila sababu za msingi.

Tumekuwa tukilikumbusha jeshi la polisi mara kwa mara kupitia safu hii kwamba jeshi hilo halina mamlaka kisheria kutoa ruhusa kwa vyama vya siasa kufanya kazi za siasa kwa njia zozote zile, zikiwamo maandamano au mikutano ya hadhara. Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992 inaeleza bayana kwamba vyama hivyo vikitaka kufanya shughuli hizo vinalijulisha tu rasmi jeshi hilo ndani ya saa 48 ili liweze kuwapa ulinzi. Tulisema kuwa kitendo cha jeshi hilo kujipachika mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama hivyo ni kuvunja sheria.

Tunarudia kusema leo kwamba ukatili wa kutisha unaofanywa na polisi dhidi ya wananchi wanaotimiza haki zao za kidemokrasia kwa amani utaipeleka nchi yetu pabaya. Polisi waache ubaguzi katika kuhudumia vyama vya siasa, kwani kama sheria hiyo ya vyama vya siasa inavyosema, vyama vyote viko sawa mbele ya sheria.

Tunawashauri wahanga wote wa vitendo viovu na ukatili wa polisi unaoendelea kwa kasi nchini kwamba sasa waanze kufikiria hatua za kisheria za kukomesha vitendo hivyo, hata ikibidi kulishtaki jeshi hilo katika Mahakama ya Kimataifa iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.
 
Jamani wandugu Arusha bado hakujatulia, polisi wamekuwa wakiwatisha watu kwa defender na landcruiser zilizojaa askari na kupita kila mtaa. Kwa taarifa za uhakika ni kwamba viongozi wa juu wa CHADEMA bado wanashikiliwa na polisi kati

Hawa ni kuwaandalia maandamano ya nchi nzima kama alivyosema mkuu Dr. Slaa, nchi hii siyo ya ccm ni ya watanzania wote. Wengine tunatamani tuwepo Arusha ili tuongeze nguvu ya kudai haki hiyo inayokandamizwa huko.

Wana Arusha tuko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwenu. Mungu awajalie moyo wa uvumilivu, kazeni tu kamba, hakuna kulala, kitaeleweka tu!
 
Mambo bado ,silaha za kivita zilitumika Zenji ,huko ni vibastola ila zenji ni rocket louncher vifaru na smg ,ak47 bila ya kusahau maguruneti.mkituambia tuna uchu wa madaraka au sio ??? mkuki kwa nguruwe.
 
Viongozi wa Chadema msifanye mzaha kwa yaliyo tokea Arusha kwani Ccm walisha sema wata tawala kwa gharama yoyote ile na sasa kauli yao ime dhihirika ,aliye jipachika umeya lazima atoke na hili hali hitaji majadiliano, swali la kujiuliza ikiwa wana diriki kumwaga dam kwa nafasi ndogo ya umeya je Slaa ange amua kudai ushindi wake alio porwa na JK nini kinge tokea? Kama kuna uwezekano walio husika wote wapelekwe ICC ili iwe fundisho kwa wengine.

tatizo lenu mnafikiri wachaga na wamasai wa arusha wanawakilisha tanzania nzima! fundisho liwe kwenu nyinyi mkome kulazimisha fujo ebo!
 
Kwa hakika ni dalili njema, lakini Tanzania tulikuwa tuna nafasi ya kuleta mabadiliko ya Chama cha kushika hatamu kwa njia ya utulivu kabisa. Kinachosikitisha ni kundi la watu wachache sana wanaotupeleka huko ktk machafuko haya. Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa nasoma UDSM, Mchungaji Mtikila alikuja pale Chuoni na kutukusanya pale Revolution Square, na alitoa mfano mmoja mdogo tu, akasema " Hivi huyo Askari anayelinda hapo Bank akiwa na SMG yenye risasi 60, ataua wangapi kabla hajanyang'anywa hiyo silaha yake"? akamalizia kwa kusema Saa ya Ukombozi ni Sasa.

Tukio la Arusha jana, limepeleka hisia zangu kwa mfano huo wa Mchungaji Mtikila alioutoa miaka karibu 20 iliyopita. Hembu hawa polisi wajaribu kujiuliza kwa mfano, watu wa Arusha wangedhamilia kukiteka kituo cha Polisi jana wangeshindwa? Nadhani polisi inabidi wajiulize haya maswali, kwani ndiko wanakotaka kutupeleka.
 
Back
Top Bottom