.
Al-qaeda ni wabaya kweli kweli lakini hata hivyo ubaya wao haujafikia ubaya wa tawala nyingi za kiafrika.
Hebu fikiria nchi kama Tz miaka 50 ya uhuru haijaweza kujenga uwezo wa umeme wa kutosha asilimia 13 ya watumiaji wake. Maji watumiaji ni chini ya asilimia 40 kwa maana ya safi na salama na hawayapati. Shule mpaka leo wanafunzi wanakaa chini tena mjini mithili ya enzi za kina Abraham na Yakobo, vijijini sijui ndo itakuwa vipi. Hospital mama mzazi anatakiwa aende na syrange mpaka na makarai ya kuogesha mtoto. Mambo yaliyo katika hali ya kibaribaiki ni mengi mno. Huku kwa upande wa pili wa shilingi serikali ikijitapa kukusanya mapato ya billion 500+.
Lakini wamekuwa wahubiri wakuu wakuwataka wale watoa kodi kibinafsi kuchangia huduma za jamii. Swali ni wapi makusanyo ya taifa(budget) kwa kila sector zinapotelea?
Watendaji wa namna hii na Osama ni nani mbaya zaidi?
Nasema Osama kwa hawa watu ni malaika wa nuru!!.
Mkuu hapo umenigusa kabisaa. Yaani umepigilia msumari wa moto kwenye hii topicNakuunga mkono asilimia mia! Ebu fikiria mtu hana uwezo wa kupata mlo mmoja kwa siku akiuza mazao yake anakatwa kodi; akinunua mafuta ya taa anakatwa kodi; akisafiri anakatwa kodi; akinunua nguo ya krismas kila baada ya miaka mitano baada ya kuhongwa kwaajili ya kadi yake ya kupigia kura anakatwa kodi; etc etc then huyo huyo anatakiwa achangie eti maendeleo....Ya kweli hayo? Wizi wa mchana and a very bad public sin commited by all professionals in Tanzania. Bora tusiende makanisani na misikitini...Hakuna anasema neno wote kimya tena wengine ndiyo wahamasishaji wakubwa wa hiyo michango. Maana ya kodi ni nini? Matumizi yake ni nini?
Kwa tunayoyafanya watanzania Osama ni malaika wa nuru. Yes hatuna uwezo wa kuwafunga; je midomo ya kuongea nakupinga ambayo tumepewa bure hatuna? Wengine ni washauri eti wa viongozi mna shauri nini kama siyo unafiki, mna wapa hizi facts viongozi? Eti tunaogopa kuwajibishwa uwongo mkubwa wote wako traped into opportunism kwamba nisipoongea vibaya basi nitapandishwa cheo; what a shame?
Damu inayomwagika kila siku kwa watoto kufa mahospitalini; vibaka kunyongwa na kulawitiwa mitaani kwa kukosa malezi ya kifamilia; ndoa zilizovunjika kwa kukosa cash na kusababisha watoto wa mtaani; mabinti waliobakwa na hatimae kutoa mimba na kuua vichanga kwa sababu ya kukosa jinsi ya kujisaidia; vijana wanaokufa kwa UKIMWI kwa sababu ya kutaka kujipatia mahitaji ipo juu ya kila mtanzania alieamua kunyamazia hali hii!
Mmmh..... mkuu hii imekwenda shule. yaani ccm wakipita hapa na kuiona hii,waweza wasilale wala kulaTunakuja Mpwa, tunakuja, subiri, tumeshajifunza, utaniambia, I can even predict nchi ya weusi itakayoanza hili vuguvugu, and am convinced itakua ni nchi fulani ya ukanda fulani unaosifiwa kwa kitu fulani cha kijinga sana ambacho in reality hakipo..., We are coming, we are coming the sons and daughters of the Oppressed we are coming, yes we are coming with a common determination, we are coming, we gona shed no more tears, we gona fear no more,
wanakuja, Wamachinga, wakulima kwa wafanyakazi, wanakuja, sichochei bali wanakuja, subiri uone, Kama jua angavu wakati wa asubuhi, ili kuleta nuru ya matumaini, wanakuja, si kizazi tena cha uongo na manyanyaso, hawatamwaga damu tena, bali vilio vyao na sauti zao ndio silaha yao kubwa, Wanakuja, wakubwa kwa wadogo, wale waliorundikwa kwenye madarasa kama kuku, wasiijue kesho yo itakuaje, wanakuja, wameshaunda na bomu, wanakuja, wasio na elimu, wasio na imani, wanakuja.
lakini, wakati wakija, Mimi na wewe tutakua wapi? je si wakati wa sisi kujiunga nao, tusimwage damu, tumwage chozi, chozi litakaloijaza bahari, bahari itakayounda mawimbi, mawimbi yatakayokuja kwa nguvu kuliko Tsunami, Yes, Tsunami itakayondoa uonevu wote, Tunakuja, Na Jina langu likiitwa, na MIMI nitakuwepo. Karibu twende wote.
Mmmh..... mkuu hii imekwenda shule. yaani ccm wakipita hapa na kuiona hii,waweza wasilale wala kula
wakimwaga 30elf polis mtaani je watashindana na watu milion 150 wa algeria?mkuu usifanye mchezo na peoples power ya ukweli ya waarabu hawaogopi kufahao,mwisho wa mwezi huu rais wa algeria ataachia madaraka,inafatia maandamano yemen,jordan,syria,ktk nchi za kiarabu ni qatar.uae,na kuwait ndio zitabaki salama,ila wengine wote watang'olewa ktk madaraka.mamemwagwa kama 30,000 police mtaani, unafikiri maandamano yatafanikiwa?
Nguvu ya ummaYES,YES,YES.Kama baba zetu walimwondoa mkoloni hatutashindwa kwa mkwere.Tupaze sauti.PEOPLE'S VOICE,PEOPLE'S POWER.