Maandamano makubwa Songea!

Mkuu wa Mkoa Bw Mwambungu alipata kuwa meneja wa bendi ya Vijana Jazz......kumpa ukuu wa mkoa ni dhihaka kubwa wakati wako wengi wenye uwezo wa kuwa ma RC.....




Hapa yuko kushoto kwa mwenye shati jeupe......juu ya hayo madole gumba


 
mkuu mawe siyo silaha??
 
Nilisema polisi ni anti CDM, wanazidi kujidhihirisha. Mpaka lini wataendelea kutuua nasi tumekaa pembeni tu tukiangalia. Tuungane pamoja tupiganie nchi yetu. Hawa makaburu weusi hawawezi kushinda vita hii.
 
Nadhani watakuwa hawana, inasikitisha kwa askari wetu kutumia nguvu mpaka kusababisha mauaji kwa raia.
Hawa askari wetu hasa wakubwa wanatakiwa kuacha kutumia sheria za kikoloni wajue watu wako huru ndani ya nchi yao, sheria za kikoloni hata bungeni waziri mhusika azipeleke zibadilishwe, watu waheshimiwe sio kuku ni watu!!!!!Waheshimiwa wabunge waangalie sheria mbovu zifanyiwe marekebisho kuzuia askari kuuwa raia wasio na silaha, kwa kisingizio eti wanatawanya maandamano!!!! Vinginevyo hata nyinyi wabunge sheria hizo zitawarudi hata kabla ya katiba mpya kupitishwa mziangalie upya kifo hakichagui!!!!!! Iweje maandamano ya amani uyatawanye kwa risasi za moto hao ni al kaida au El shabab ?????

 
Ukweli ni kwamba polisi wanatangaza vita na wananchi, ipo siku watapata wanachokitaka. wasijisahau pia kwamba hata wao ni sehemu ya wananchi.
 
Ukweli ni kwamba polisi wanatangaza vita na wananchi, ipo siku watapata wanachokitaka. wasijisahau pia kwamba hata wao ni sehemu ya wananchi.

Na mbaya zaidi tuko nao mitaani na familia zao,watakuja kusaga meno hawa wahusika
 
Ushauri wako wa ulinzi shirikishi ni mzuri kaka, lakini naona kuna jambo hujaliona hapa. Hatua ya kufikia ku-shoot waandamanaji inaashiria kuwa polisi waliona wamezidiwa sana kiasi kwamba hata tear gas au njia nyingine za kudhibiti waandamanaji zimeshindikana, and I don't believe that it reached that extent!!
 
Kwa maana hiyo nani amfuate mwenzie kuanzisha huu ulinzi shirikishi? Waendesha pikipiki wawafuate polisi au polisi wawafuate waendesha pikipiki? Nini kazi ya jeshi la polisi? Usalama wa raia wanaouongelea ni kitu gani hasa?
Polisi wanalipwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia, na wana mtandao hadi huko kanda ya ziwa unakodanganyia, kwa hiyo hatutegemei hadi mwendesha pikipiki wa tisa anakufa hawajaja na hiyo prototype ya kanda ya ziwa na bodaboda guys wabakie wanaangalia tu. Ngoja siku auwawe ndugu yako ndo utajua kuwa AN INJURY FOR ONE IS AN INJURY FOR ALL
 
RPC anasahau ukweli kwamba ukiwa mwongo lazima usiwe msahaulifu!!!
 
Mkanganyiko wa aina yake uko kwenye taarifa zenyewe kuhusu idadi sahihi ya majeruhi na wale waliokufa huko mkoani Songea.Kulingana na gazeti la Mwananchi:
1.Polisi inasema waliokufa ni wawili na majeruhi ni 10.
2.Uongozi wa hospitali ya mkoa umesema umepokea maiti 4 na majeruhi 41 wawili kati ya hawa majeruhi wakipelekwa chumba cha upasuaji kutokana na kuwa na majeraha ya risasi.
3.Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inasema waliokufa ni wawili na majeruhi 20.
Kwa kawaida ukipata taarifa za ''casualties'' kwenye maafa yeyote hasa yanayoweza kuitia serikali matatani(RC ndiye mwakilishi wa serikali hapo) zidisha mara 2 angalau utakuwa umefikia kwenye idadi kamili.

My take:
Mfumo wa kushughulikia maandamano ya wananchi na namna ya utoaji taarifa juu ya maafa yanayojitokeza unahatarisha the so called ''amani nchini''.
Yaliyotokea Zanzibar kipindi cha Mkapa hasa ule wakati wa uchaguzi yana nafasi kubwa ya kujirudia tena lakini sasa kwa kiwango kikubwa hapa Tanzania Bara kwenye uchaguzi ujao.
Kama Jeshi la Polisi limeshindwa kushughulika vizuri na idadi ndogo ya watu katika sehemu tu ya mkoa wa Songea pata picha machafuko yakiwa katika kiwango cha kitaifa.
''Massacre in the making''
 
kujikomba kwa wakuu ili ionekana ni sahihi walichofanya kwa vile walikua wanalinda ofisi za chama zisidhurike!ila angekuwepo julius k nyerere ndio kiongozi wa nchi nafikiri sasa hv wahusika wote wangekua wamewajibishwa na wapo lupango!

next time mwende na vipaza sauti (mmesahau arusha ) mtoe maoni yenu mita mia tatu ndo wata waelewa msife wengi tuna hitaji makamanda 2015;mtumie news jk yuko london ana hangaika na wasomali wakati kwake kuna ungua
 
Ningependa sana kusikia kauli ya Rais wetu lakini najua hataongea kamwe...

Shida sasa ni jinsi nchi yetu inavyozidi kukosa mwelekeo.. Ukienda kwa undani matatizo ni mengi sana na ya msingi...

Mfumo Mbovu wa Elimu
Viongozi wasio wazalendo
Katiba Mbovu
Kushuka kwa thamani ya Shilingi..

Haya yote ni matunda ya serikali na utawala mbovu usio na ruya ya kuona mbele...
 
Haya ndiyo maneno ingawa muda si mrefu utaambiwa unaombea vita ije.
Wakati mwingine lazima uwe na maamuzi yanayoweka woga pembeni..vita kwa ajili ya jambo jema ni utukufu mbele za mungu, Hata Yesu(nabii issa) alipoona hekalu la Mungu limegeuzwa pango la wanyang'anyi aliamua kuingilia kati na kumwaga vitu chini ili kurudisha hadhi ya nyumba ya bwana..kazi ni kwetu Watanzania.
 
hii yote inatokana na utendaji mbovu wa vyombo vyetu vya dora ukiangalia sababu zao na ukaenda kulinganisha na tukio halisi ndo unapata picha ni kwa jinsi gani vyombo vyetu vinatumika kukandamiza haki ya wananchi hatuwezi kuwa taifa la mauaji kila kukicha ukiangalia polisi wetu wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kuliko hata kwenye maandamano,katiba imeweka wazi ni ruksa kwa watu kukutana na kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na manufaa kwao kwa hyo kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na wala siyo kuua na kujeruhi raia hatuwezi kuwa na taifa ambalo alijari haki ya kikatiba ya kuishi ni lazima tuchukue hatua ambazo zitatufanya tushi kwenye nchi yetu kwa amani hatuwezi kuwa waoga pale tunapodai haki ndugu zetu wanaangamia kisa wanadai haki yao ya msingi ya kikatiba ya kulindwa wao pamoja na mali zao hamna kitu kinachouma kama risasi tunazonunua kwa kodi zetu ndo zinatumika kutuua walipa kodi,mbona askari wanaohusika na mauaji haya hawachukuliwi hatua angalia zanzibar mwaka 2001,angalia Arusha mwaka jana,angalia songea kwanini wasifikishwe kwenye vyombo vya haki ili waweze kujibu tuhuma ni kwanini wanawanyang'anya haki yao ya kuishi kwa mujibu wa katiba,ni lazima haki itendeke
 
Naamini polisi ni binadamu na wanaowaua ni binadamu na kwamba Mungu aliwaumba kama wao. Hii tabia ya polisi kujidai wanatetea sana CCM itawageuka wamesahau kuna leo na kesho. wanasahau pia kwamba lazima kuna watu wanaona kila wanapoua na hilo jicho ndo litakalo wafuata mpaka kufa kwao halafu wanasahau kwamba hiyo jamii wanayoiua ni jamii wanayoishi nayo, na kwamba wanajenga chuki mbaya ambayo naamini itawahukumu baadaye. Wasijisahau sana na tumewachoka, wanaifanya nchi hii iwe ngumu kusihi haina utu hata kidogo bali imejaa ubabe na dhuluma tu.
 
Every tanzanian has a right to live and to be protected according to the constitution.Its a pity that the ones we have entrusted to protect us are the ones killing us.Where are we going?when will all these end?and how did we even get here?
Immediate measures should be taken to stop this.
 

Hivi nyinyi mnalalamika nini? Mnafikiri TZ kuna jeshi la polisi, wengi wao ni genge la wahuni na majambazi. Poleni sana kama mtakasirika. Nimeshasikia kwenye taarifa ya habari wananchi wanalalamika baada ya kituo cha polisi kujengwa ujambazi ndio umeongezeka. Alafu we haushangai mtu mzima na akili zake analipwa sh laki mbili na anakubali kufanya hiyo kazi we unadhani ni wazima kichwani hao...poleni sana ndugu zangu mliokumbwa na hili jambo.
 

ungefahamu ukaribu wa mkuu wa mkoa wa ruvuma na mkuu wa nchi-ungeshangaa,hawa mabwana ni maswahiba wa karibu sana.Hii ndo inayotucost maana kiongozi anampromote rafiki yake kuwa mkuu wa mkoa,bila kujali competency yake,matokea yake RC hata ku-settle quarrels kama hizi anashidnwa-watu wanauliwa pasipo sababu ya msingi.
hawa viongozi wetu ni janga la taifa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…