Maandamano kupinga posho za Wabunge

Ili suala la posho linashangaza sana,kuna watu wanalidandia kiushabiki tu...ningeunga mkono kama yangeitishwa maandamano ya kuongezwa maslahi kwa tasnia zingine kama mishahara ya walimu,polisi,manesi nk sio wengine wasiongezewe,maisha yamepanda sana kiukweri kwa mbunge anaetegemea kipato cha ubunge wake pekee,iyo elfu 70 apange hoteli,ale chakula,aweke mafuta gari,dereva wake nae anamuangalia..tuandamane posho ziongezwe kwa wote ndio suluisho.
 
Ili suala la posho linashangaza sana,kuna watu wanalidandia kiushabiki tu...ningeunga mkono kama yangeitishwa maandamano ya kuongezwa maslahi kwa tasnia zingine kama mishahara ya walimu,polisi,manesi nk sio wengine wasiongezewe,maisha yamepanda sana kiukweri kwa mbunge anaetegemea kipato cha ubunge wake pekee,iyo elfu 70 apange hoteli,ale chakula,aweke mafuta gari,dereva wake nae anamuangalia..tuandamane posho ziongezwe kwa wote ndio suluisho.
wewe vipi! Kwani nani asiyetegemea kipato kutokana na kazi anayofanya!!! kwani walimu hawategemei mshahara kutokana na kazi yao ya ualimu? ningekuwa na uwezo ningetandika bakora wabunge woteee! na kuwanyang'anya walichojiongezea!
 
Napenda kuandamana lakini naogopa.
Naogopa mkono mrefu wa serikali.
Naogopa kupigwa na polisi na kuswekwa lupango
Naogopa kufa

Akilini kwangu napiga picha jamaa fulani mashujaa.
Mashujaa wasio ogopa kitu chochote
Vijana wenye ujasiri
Wasioogopa virungu vya polisi
Wenye hoja za mvuto midomoni mwao
Wenye upeo na uelewa.
Wazalendo.
Wzalendo hawa waandamane kwa niaba yangu na waoga wenzangu
Ikibidi nianamane basi nijichanganye humo huku nikificha sura yangu wasije wakaniona
bango langu lenye maneno mazito mfukoni
naficha sura yangu kwa sababu naogopa kisasi cha serikali mmbo yakienda mrama
Najificha ficha ili wenye nchi na wenye neema wasinione.
Nipo lakini natakiwa nisionekane, naogopa mwenzenu
Ushujaa wangu ni huko mafichoni au nikiwa na wa ubani wangu chumbani
Ushujaa wangu mpaka nipige kilita cha ulanzi
Ushujaa wangu unategemea neema ya wanao ninyanyasa.

Napenda kuandamana ili niibane pummbu serikali ya CCM
Lakini tatizo langu pummbu zangu zinanywea pale tu nikikumbuka kipigo cha FFU
Mkwara wa FFU unanifanya nilegee kaa choko
Usicheze na virungu vya FFU
Wale jamaa wanatandika mwana koma.

Napenda ningejaliwa moyo na ujasiri wa Nelson Mandela
Napenda ningejaliwa Ari ya Martin Luther King
Napenda ningekuwa na moyo hata nusu tu wa wale mashujaa vijana wa Misri
Napenda ningekuwa Mkurya wa Tarime
apenda ningekuwa Marusha au Msafwa wa kule Mbeya

Nahisi zile nyimbo za kuwaimba viongozi wakati wa gwaride enzi zile zimenitengua nguvu zangu
Nahisi mwenge wa CCM lile tochi la BAALI unazidisha unyonge wa Mtzanzania na kuwapa nguvu MAFISADI

Napenda kuandamana kupinga uonevu lakini ushujaa huo sina
Napenda kuandamana kupinga kuongozwa na vilaza kama baba Riz lakini naogopa kipigo

Naogopa kwa sababu ya uoga utokanao na woga wa kuogopwa kila kiogofyacho.
Woga wangu unatokana na woga wala sina sababu nyingine
woga wangu unatokana na utii bila udadisi
Woga wangu ni mazoea ya kuishi katika lindi la woga
woga wangu uko kwenye damu nisipo ogopa nahisi uhai unanitoka
woga wangu ni sehemu ya utamaduni wangu
Kiongozimwandamizi wa serikaali hata adanganye vipi ni lazima awe anasema ukweli
atanganya vipi hali yeye ni kiongozi wa serikali?
Eti tunaambiwa;
TBC siku zote wanasema ukweli
Redio ya serikali kamwe haiwezi kuongea uongo
Mimi na wananchi wenzangu ndiyo wenye akili finyu
Hatuelewi namna serikali inavyoendeshwa
Hatuna uvumilivu wala adabu
Pili hatuna uzalendo na heshima kwa viongozi wetu.
Viongozi wa serikali ni waadilifu na ni watu waliotosheka.
Kuandamana ni ukosefu wa fadhira na utovu mkuu wa nidhamu.


kunguru mwoga hukimbiza bawa lake
Mimi sina bawa nakimbiza Mioro na kwato zangu ili FFU wasizibanange.

Napenda kuandamana
sababu za kuandamana ninazo akini woga umenijaa kibao
Nipeni ushujaa hata kesho nitaandama

Haki ya nani! Ningekuwa na ushujaa wa Dr Slaa hata kesho ningeandamana.

Mwnezenu niliumbwa na moyo wa kuku, yaani kuku mkubwa
siku zote najua Hatima ya kuku ni kisu
Mimi ni wa kisu tu
Sipendi kuwa na moyo wa kuku
sipendi kuwa mwoga
Nataka kuwa shujaa
Ushujaa niliuacha kule kwa marehemu JKT
Enzi zangu walini hara wakati wa uchaka
Nilikuwa mtaalamu wa Mbinu Za Medani, leo hii naogopa hata kumwuua nzi

Napenda kuandamana lakini,lakini,lakini...... we acha tu.
 
Nakumbuka Kardinari Policarp Pengo alisema " maandamano sio njia sahihi ya kuwasilisha malalamiko yenu kwa Serikali "

Kazi kwenu.
Quotation yako siyo "Kharam" kweli?
How can you quote an infidel?
Acha unafiki!
 
Mi ntayaongoza arusha japo mi mgeni jf.ila sitawakaribish Zitto na Makamba coz wantafuta cheap popularity,a heat dhat guyz wana tamaa,ni sawa na MUUAJI MSIBANI ANALIA SANA KUMBE ANAFURAHI.malaria sugu na faiza foxy sasa nipo na nyie ana kwa ana na buku zenu mbili mnazopewa na Nape
 
Tulishapata matangangazo mengi ya maandamano huko nyuma sasa hatutaki mnatusumbua . Tukijitokeza hatuoni kitu.

unasema kweli mkuu hata mimi nashangaa wanaongea tu Kova akikohoa wote wanaingia mitini
 
Mi ntayaongoza arusha japo mi mgeni jf.ila sitawakaribish Zitto na Makamba coz wantafuta cheap popularity,a heat dhat guyz wana tamaa,ni sawa na MUUAJI MSIBANI ANALIA SANA KUMBE ANAFURAHI.malaria sugu na faiza foxy sasa nipo na nyie ana kwa ana na buku zenu mbili mnazopewa na Nape
 
kweli imefika wakati wa wananchi kuandamana kupinga ongezeko la posho
 
Watu wanazidi kulalamika kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari juu hali ngumu ya maisha lakini Rais na serikali wameziba pamba kwenye masikio.kwenye posho za wabunge akasign bila kusita na kuwaharumia wapiga kura wake.Naomba Mungu aliponye taifa letu na kama ni mapenzi yake hapendi tuteseke wabunge wote waliopigia debe ya increase ya posho zao wapate hali ngumu na washindwe kwenye uchaguzi ujao 2015 pamoja na ccm ile mweleka kwenye post ya rais.
 
Mi ntayaongoza arusha japo mi mgeni jf.ila sitawakaribish Zitto na Makamba coz wantafuta cheap popularity,a heat dhat guyz wana tamaa,ni sawa na MUUAJI MSIBANI ANALIA SANA KUMBE ANAFURAHI.malaria sugu na faiza foxy sasa nipo na nyie ana kwa ana na buku zenu mbili mnazopewa na Nape
Hawa nao walipaswa waandamane mpaka pale Lumumba kupinga hizo buku mbili ili ziongezwa maana ukali wa maisha sii Dodoma tuu hata Dar na wao ni watendaji waaminifu kwa Nape. Wako kazini usiku na mchana mara itokeapo hoja ya kukibomoa chama chetu twawala.
 
Kama hili ni kweli, basi kuna ujuha huko kwenye watoa maamuzi. Wamekunywa bia wamelewa au hawajui wanalolifanya. Double standard
 
Mzaha Mzaha mwishowe jibu hutumbuka.

Serikali inachezea amani ya nchi kwa kuwapokonya wananchi haki

Sasa watanzania tujipange kimkoa kwa maandamano.

Tunawaomba maaskari na waalimu muungane na watanzania ili kupinga wabunge kujiongezea posho badala ya kuboresha huduma za afya.

Je kwani yeye mbunge ni muhimu kuliko wewe mwalimu au askari?

Sasa tuweke kamati za kimkoa. watu wajitolee kwa kazi hii ya kuwa kiongozi kila mkoa.

Katika kila mkoa, wanaojitolea kuongoza na kutoa maelekezo wajiandikishe.

Mwanza....

Dodoma..

Morogoro...

Dar es salaam--

Pwani...

Mtwara...

Lindi...

Rukwa...

Ruvuma..

iringa..

-Mbeya..

Kigoma...

kagera...

shinyanga..

mara...

kilimanjaro...

tabora.

arusha..

manyara..

Sasa ni wakati wa kwenda mbele. na kuchukua hatua

tukishapata viongozi kila mkoa, tunaandaa ujumbe ambao tutakutana na kuutuma kwa sms kwa watu wote Tanzania.

JWTZ na usalama wa Taifa mtusaidie kuikomboa Tanzania.

Hapa simaanishi wale JWTZ na usalama wa taifa wanaoitetea Xicmmm!!!!
 
Tujiunge na kama tukishindwa kuandamana basi tuunde kundi kama Boko Haramu.

Tutashirikiana na polisi, JWTZ na tutaikomboa Tanzania.

Namaanisha polisi na JWTZ walioichoka XCMM
 
Hahahahah halkaf Makinda anatufundisha namna ya kuhesabu hizo posho. Eti tusiumie kwani si miaka yote bali watalipwa pale tu watakapokuwa wanakaa vikao vyao. Hahahahah kaazi kwelikweli

Bado Kikwete anatai Tanania itagharamia ujenzi wa mahakama ya haki za binaadamu itakayojengwa Arusha. Kwa haki zip[i??
 
NAKUBALIANA NA MEMBERS WALIOCHANGIA HOJA HII KWA KUSEMA ,
"MUANDAMANAJI NANI?"

Hii ni sawa na ile hadithi ya panya na paka, Panya Mwerevu kwa wenzie, "Jamani eeeeh huyu paka tumfunge kengele ili kila apitapo kengele itapiga tutajua yuko wapi na hivyo kusalimisha maisha yetu" Panya Mwerevu zaidi akauliza huyo wa kumfunga Paka kengele katika sisi ni naniiiiiiiiii? wooooote KIMYAAAAAAAAAAAAA!!!!!!! Haya na sisi muandamanani nani??????
Jamani tuishie humu humu kwenye forum kwa kupiga mayoe lakini MTENDAJI HAKUNA, wa kwanza nikiwa mimi mwenyewe. NIMEKUBALI YAISHE.
 
Dear SEM, mie narudi pale pale muandamanaji hapa HAKUNA, tena HAKUNA kwa herufi KUBWA, iwe kwa posho za wabunge au kwa sanda za Maiti, ona Madaktari, kwanza wanavyodharauliwa kwa kuachwa hapa Muhumbili na watu kwenda kutibiwa India USA na UK and whereever, wanavyo nyanyaswa kwa kudai haki zao, wenginge waburuzwa kazini na FFU, kisha wao ndio wanalaumiwa kuwa wanaacha watu wanakufa hovyo, kana kwamba wao ni washika roho, basi hamuwezi kuwaongeza Posho , wapeni Kauli nzuri, kwani maneno matamu yalimtoa nyoka pangoni, lakini kwa kuwa serikali yetu ya mabavu wanaona wakiongea nao taratibu wataonekana wanawambembeleza.
JAMANI EEH MAANDAMANO HAKUNA, tusijifananishe hata kwa theluthi na hao WAANDAMANANI wa kweli.
 
Back
Top Bottom