Maandamano kupinga posho za Wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano kupinga posho za Wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jan 31, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  MAANDAMANO NDIYO DAWA YA KUPINGA ONGEZEKO LA POSHO ZAWABUNGE

  Inasikitisha na ni huzuni kubwa kwa jamii ya Watanzaniakusikia kwamba Rais Jakaya Kiwete amebariki na kuridhia ongezeko la Posho kwaWabunge kutoka Tshs .70,000/= mpaka Tshs.200,000/=. Kwa ongezeko hili kilaMbunge sasa ataondoka na kitita cha jumla ya Tshs.330,000/= kwa kila sikuanayokuwepo Bungeni. Hii ni pamoja na kujumlisha Tshs.80,000/=kama posho yakujikimu(perdiem)na Tshs.50,000/= pesa ya mafuta(fuel allowance)inayolipwa kilasiku kwa kila Mbunge aliyeko Bungeni.

  Kitendo hiki cha Rais kinaonyesha jinsi Rais Kiweteasivyokuwa na upeo wa kuongoza. Lakini pia kinaonyesha udhaifu wa Serikali yaCCM ambavyo imeshindwa kuongoza nchi hii. Rais Kiwete na Serikali yakewameonyesha DHARAU kubwa sana kwa Watanzania. Kwamba pamoja na malalamiko nakelele za Wananchi na Wanaharakati mbalimbali kupinga posho hizi Kiwete na Serikaliyake wameamua kuridhia ongezeko hilo!

  Sasa basi Watanzaniatufanye nini kutokana na kitendo hiki cha dharau, kihuni,kidikteta nakinyonyaji kilichoridhiwa na Rais Kiwete? Jibu nimoja tu: MAANDAMANO.

  Haiwezekani kwa namna yoyote ile kudharau na kupuuza maoniya Watanzania ambao ndio wameiweka hii serikali madarakani kwa matumaini kwambaingelikuwa sikivu na kuweza kuwaletea maendeleo Watanzania.
  Kuna matukio mengi sana ya kuonyesha kuwa vipato vyaWatanzania walio wengi ni vidogo sana kuanzia Wakulima mpaka Wafanyakazi wataasisi na idara mbalimbali. TUCTA walishaiomba serikali kuongeza Mshahara waKCC (Kima Cha Chini) toka Tshs. 135,000/= mpaka 315,000/kwa mwezi . Badoserikali hii imekataa katakata kwa madai kuwa mshahara huo ni mkubwa sana nahauwezi kulipwa!
  Let's use our common sense. Kama kuna mtu anaweza kulipwaTshs. 330,000/= kwa siku kwa maana ya Mbunge,vipi kwa Mfanyakazi anayedaiTshs.315,000/=kwa mwezi siyo kwa siku ishindikane?Kulipa Tshs.330,000/=kwa sikuPESA IPO. Lakini kulipa Tshs.315,000/= kwa mwezi PESA HAIPO!!!!!

  Kwa sasa kuna MGOMOWA MADAKTARI nchi nzima wakidai kuboreshewa maslahi yao serikali imekataa kwamaneno kwamba madai yao ni makubwa mno kiasi kwamba seriakli haiwezi kuyamudu. Madaktari bila shaka wamesikia kuwa Rais Kiwete amekubaliWabunge walipwe Tshs 330,000/=kwa siku ilhali madai yao(Madaktari) wanaambiwaserikali haina pesa ya kulipa viwango wanavyodai . Hivi Kiwete na Pinda na serikali yao ya Chama Cha Majambaziwanatarajia nini kutoka kwa Madaktari hawa?
  Nahitimisha kwa kusema kuwa sasa ni wakti wa Watanzania KUAMKANA KUPINGA UJINGA HUU WA SERIKALI YA CCM KWA MAANDAMANO MAKUBWA YA NCHI NZIMAMPAKA KIELEWEKE. Naomba Wabunge makini wa CHADEMA waanze kuwasha motohuko Bungeni kuhusiana na Posho hizi za KIFISADI ili Watanzaia wajue kuwawamechoka kuongozwa na Serikali ya majuha!
  Nawasilisha.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  tatizo ni uthubutu wa walio wengi kupinga udhalimu huu na ufedhuli haupo
   
 3. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulishapata matangangazo mengi ya maandamano huko nyuma sasa hatutaki mnatusumbua . Tukijitokeza hatuoni kitu.
   
 4. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kibaya kama kusumbua waandamanaji kila tukijitokeza waandaaji mnaingia mitini. Mnacheza na muda wetu. Mimi natangaza rasmi hakuna maandamano.
   
 5. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini pia sikubaliana na maandamano ya chama kimoja cha siasa hayana sura ya utaifa.
   
 6. bona

  bona JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  tufanye kama walichofanya wenzetu wa naijeria ndo kitaeleweka vinginevyo ni upuuzi tu!
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  zimekuwa kama verses za bongo flava hazina mashiko, maneno yale yale "mpenzi nakupenda" kwa kila mwimbaji na single zao
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kibali ndo itakuwa tatizo. Lakini hata polisi nadhani hata kama viongozi wao watakataa kuruhusu, nadhani polisi hawatapiga mtu, kwani nao inawahusu sana
   
 9. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maandamano sasa basi, silaha haramu ziingizwa hasa mabomu ya kurusha tuilipue bunge. Sasa ni kujitoa mhanga.
   
 10. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  wako wapi wana jf waliokuwa wanamponda Dr.Ulimboka kwa kitendo chake cha kuongea na vyombo vya habari akitokea mafichoni kuwa si cha kishujaa ila ni woga? naomba sasa wao wawe mstari wa mbele ktk kufanya hayo maandamano ili tujue kuwa wao ndio mashujaa wa ukweli
   
 11. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  watanzania tumebaki kuwa washadadiaji huku taifa letu linaangamia,na hata watawala wanalielewa ilo ndio maana wanapitisha mambo wanayotaka wao,vijana watanzania wengi hatujitambui na hatuna uthubutu kabisa,tunashindwa kuelewa kua athari hizi zinatugsa sisi moja kwa moja na familia zetu pia,tumebaki kukaa pembeni na kulalamika na kua watumwa wa kushadadia mambo bila kuchukua hatua kuiamsha serikali,hii haitatusaidia kabisa,mbaya zaidi wengine bongo zetu zimeathiriwa vibaya mno hata mambo ya kijinga tunashabaikia na yale ya maana tunayapuuzia,utakuta mtu msomi kabisa anabakia kushadadia siasa kama vile ni simba na yanga,hizi siasa za usimba na yanga zitatufikisha wapi sisi kama taifa?tunashindwa elewa kuwa siasa ni zaidi ya upigaji kelele majukwaani au vijiweni,sias ni maisha.....kwa kweli ili ni taifa linalparaganyika,vijana hatujitambui kabisa.....hii kitu ya wabunge ilitakiwa kupingwa kwa nguvu zote,uwe mfuasi wa tlp,cuf,ccm,udp,cck,cdm au usiwe mfuasi wa chama chochote ili sio jambo la kuliacha na kukaa pembeni kushadadia tu
   
 12. K

  Konya JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hizi story za udhalimu wa hii serikali sasa zinatia kichefuchefu..na kila siku ni tuandamane mara tugome mwisho wa siku hakuna cha mgomo wala maandamano...zinachosha sasa!!
   
 13. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Masikini, Kikwete! Sikulaumu sana kwa sababu tangu awali ulionesha udhaifu wa kimaamzi, halafu mbaya zaidi washauri wako nao hawakutakii mema wamekuwa wakikupotosha kila mara.
   
 14. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hakuna mwandamanaji Bongo...na hata ukiandamana peke yako au wachache kuonyesha msimamo, waBongo watakuona kichaa na kukudhiaki! Ona yanayotokea kwa madaktari...Bongo ingekuwa nchi ya mwamko, angalau hata ndugu/rafiki au wagonjwa wenye testimonies za dhati jinsi walivyowahi kusaidiwa na madaktari basi wangekuja toa support!
   
 15. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Maandamano hayawezekaniki maaana Alshabaab watakuwepo.

  Kujitoa muhanga ndio mpango. Lipua V8 zote
   
 16. k

  kiche JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maandamano nchi hii ni porojo tu,la msingi kila mtu adai nyongeza ya posho kwenye eneo lake la kazi kama walivyoanza madokta,viongozi hawana uzalendo,pia tatizo ni sisi wananchi kwani zadi ya 75% ya hawa wabunge watarudi tena mjengoni kwanini maandamano yetu tusiyafanye 2015 kwenda kwenye box ka kupigia kura kwa lengo la kuwaondoa ambapo hakuna virungu wala maji ya kuwasha??kwa kufanya hivi watakaoingia watakuwa wamepata somo hivyo watajua umuhimu wa kuwajali wananchi
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Na hicho ndicho kinachokatisha tamaa kuhusu watu wetu, hata unapojaribu kuonyesha njia ya kwenda wataiacha serikali na kukugeukia wewe kwa hoja za kijuha oh mdini mara mkabila.....
  Watanzania ni umma wa ajabu sana hapa duniani.
  Hivi? Sawa vyama vya siasa (upinzani) hatutaki vizungumzie mustakabali wetu kisa "eti vina jichukulia umaarufu (hoja ya kipuuzi sijawahi ona)"
  je hizo trade unions ziko wapi??
  Maandamano hata ya umma unaojitambua lazima yaongozwe na vyama vya umma.....
  Mambo hapa kwetu yanakatisha tamaa sana.
   
 18. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu hakuna maandamano yanayopangwa, labda yenye ruksa na serikali!
   
 19. Mutta

  Mutta Senior Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ongeza mshahara wake 1,750,000/=Mimi sielewi tumewachagua wa nini?
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Kardinari Policarp Pengo alisema " maandamano sio njia sahihi ya kuwasilisha malalamiko yenu kwa Serikali "

  Kazi kwenu.
   
Loading...