Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 189
Mbona leo unakwenda kinyume nyume?
Nafikiri weye ndio umebehave hivi hapa!
Hapa JF wazo likianikwa, linachangiwa kutokea kona mbalimbali.
Walioko kinyume na mada hawalazishwi kukaa kimya.Hata kuonyesha tofauti ya mawazo ni mawazo.
Cha msingi acha tuipeleke mada vyovyote, kwani kuna wanaotuelewa.
Tukiendeleza kubishana, tutapoteza lengo la uwanja huu.
Hakuna mtu anakataza kuijadili hoja kwa mtazamo hasi, lakini kama unaweza kufanya hivyo basi utoe hoja za msingi za kukisupport unachokisema.....! Kwa mfano,hao wanaompinga JK wanasababu zao....sasa na wewe kama unamuunga mkono basi toa sababu za kufanya hivyo ili na wengine waweze kupima na kuamua either kumpinga au kumuunga mkono muungwana!
Nafikiri weye ndio umebehave hivi hapa!
!
NEXT LEVEL,
Mawazo yako ni mazuri sana mkuu,
Nakubali.
Kaniki ndugu yangu, unakuwa kama ile nguo ya zamani bana.Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.
Hivi huoni kuwa wewe ndiyo unaongea tu na hufanyi vitendo?
ulitakiwa uje hapa na ushahidi kuwa umeandamana kupinga utawala wa JK, don't waste your time kwa kubishana hapa kwenye forum, nenda ukaombe kibali kwa Kova haraka tu.
Kwani Kova wa Kigoma kwa sasa ni nani?Aende huko.Jamaa yuko Kigoma. akaombe kibali kwa Kova!!!!
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ...
Huoni kama maandamano pia yaweza kuwa njia nzuri ya kuhamasisha asipigiwe kura 2010? i...
Mapema mno kuandamana.Ukiitisha maandamano ya wana JF, trust me utajikuta wewe, Invisible, Zitto, Slaa, Mbowe, Mkumbo, Mnyika, Kahangwa, Mrema, Lipumba, Seif, Halisi, Mpita Njia, Uwiano Maalum na wengine wachache.
Afadhali uite maandamo ya wananchi wote; kama ni ya wanaJF pekee hiyo haitatimia, hata tukibeba mawili mawili, kuna baadhi ya mabango yatakakosa wabebaji.
Samahani kwa niliowataja hapa, kwani nimewataja kwa mfano tu; hawajanipa idhini wala ishara kwamba wataandamana.
Aliyeko tayari kuandamana ajitaje, na orodha apewe bwana Kaniki, aiweke kwenye post yake ya kwanza, then maandamano yaandaliwe.
Unakumbuka nini kilitokea South Africa last year kuhusiana na Thabo Mbeki? Unataka kuniambia wao hawakujua kuwa mwaka huu kuna Uchaguzi huko bondeni?
Kama maandamano ni ya humu ndani ya nyumba sawa kabisa!Hayo ya huko katika miji na majiji sijui kama kutapatikana waandamanaji.Kaniki & Co.haya...ongoza njia!
Mapema mno kuandamana.
Elimu tunayoitoa hapa inapaswa kwanza kupenya ktk mioyo ya Watanzania then hayo maandamano yataaandamana kila baada ya muda mfupi kwani sasa hivi hata polisi nao wanapaswa kuelimishwa.
Ops mawazo ya kilevi haya
Mbeki aliondolewa na maandamano au chama chake? South Africa hakuna uchaguzi wa kumpigia kura mtu mmoja kupewa uraisi. Chama kina piga kampeni kikishinda wana pendekeza raisi bungeni then wabunge wanampigia kura. Kisa cha Mbeki kuondoka ilikua chama chake kumuondoa katika nafasi hiyo na wala siyo kweli kuwa wananchi waliandamana kumuondoa madarakani. Anyway siyo kuwa napinga maandamano ya JK ila nakupa facts the SA kuwa hawakuandamana kumuondoa Mbeki.
Najua hivyo ndivyo ilivyokuwa, hoja yangu ni kuwa; Kama ANC walijua kuwa waliweza kumshinikiza Mbeki kuresign 1 year kabla ya term yake ya urais kuisha na wakijua wangeweza kufanya hivyo this year, kwa nini sisi tusubiri uchaguzi?
Hata kama chama chake cha sisiemu, hakitaki kufanya yaliyofanywa na ANC, sisi wananchi tunaweza kufanya yaliyofanywa na ANC kwa njia nyingine mkuu kama vile kuandamana etc!
I still believe in the revolution of the vote. Kama tukiandamana bure halafu bado CCM mwakani inaingia madarakani tuta faidika vipi? Ufisadi ule ule si utaendelea tu chini ya mwingine? Cha kufanya ni kung'oa madarakani chama cha mafisadi kabisa. Tukimuondoa JK simply kumuondoa JK tu hao mafisadi ndani ya chama wata chagua tu mwanasesere mwingine kutuongoza. Ndiyo maana nikasema nguvu tuiwekeze katika kuondoa chama tawala madarakani mwakani. If Kenya na ukabila wote could do it so can we.
I still believe in the revolution of the vote. Kama tukiandamana bure halafu bado CCM mwakani inaingia madarakani tuta faidika vipi? Ufisadi ule ule si utaendelea tu chini ya mwingine? Cha kufanya ni kung'oa madarakani chama cha mafisadi kabisa. Tukimuondoa JK simply kumuondoa JK tu hao mafisadi ndani ya chama wata chagua tu mwanasesere mwingine kutuongoza. Ndiyo maana nikasema nguvu tuiwekeze katika kuondoa chama tawala madarakani mwakani. If Kenya na ukabila wote could do it so can we.