Maandamano dhidi ya sheria mpya ya uraia India

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Maelfu ya watu wameteremka majiani katika miji kadhaa ya India , masaa machache tu baada ya dazeni kadhaa za waandamanaji na maafisa wa polisi kujeruhiwa, machafuko yaliporipuka katika viwanja vinavyozunguka vyuo vikuu.

Sheria ya uraia iliyoidhinishwa wiki iliyopita inawaruhusu wahamiaji ambao si waislam kutoka nchi tatu zenye wakaazi wengi wa kiislam, Afghanistan, Bangladesh na Pakistan kupata uraia ikiwa wanasumbuliwa kutokana na imani zao za kidini.

Wakosoaji wanasema sheria hiyo iliyowasilishwa na chama cha waziri mkuu Narendra Modi cha wazalendo wa kihindu -Bharatiya Janata ni dhidi ya waislam.

Watu wanne wameuwawa katika jimbo la kaskazini la Assam tangu maandamano yalipoanza wiki iliyopita.

Machafuko yameripuka jumapili baada ya maandamano ya wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Jamia Milia Islamia mjini New-Delhi kugeuka mapambano dhidi ya vikosi vya polisi.

Polisi wametumia gesi za kutoa machozi na kuwakamata wanafunzi 100 kabla ya kuwaachia huru mapema jumatatu.

Watu wasiopungua 69 wakiwemo waandamanaji 39 na polisi 30 wamejeruhiwa na mabasi yasiyopungua manne na pikipiki 100 zimetiwa moto-msemaji wa polisi MS Radahawa amesema .

Waandamanaji wanadaai mitandao ifunguliwe
Waandamanaji wanadaai mitandao ifunguliwe

Korti kuu inatarajiwa kuamua jumanne kama sheria hiyo ni halali au la

Vyama vya upinzani vinasema tatizo kubwa zaidi katika sheria hiyo mpya ni ile hali kwamba inakiuka katiba kwa kutowapatia hifadhi waislam. Vyama vya upinzani vimeshatuma malalamiko yao mbele ya mahakama kuu kudai sheria hiyo ibatilishwe.

Naibu waziri wa mambo ya ndani G.Kishan Reddy anavituhumu vyama vya upinzani kuchochea machafuko na kuongeza kusema kwamba serikali inafanya juhudi za kurejesha nidhamu na sheria.

Waziri mkuu Narendra Modi amevitaja visa vya matumizi ya nguvu kuwa ni vya kuhuzunisha na kutoa wito wa kurejea amani."Matumizi ya nguvu katika maandamano dhidi ya sheria mpya ya uraia yanahuzunisha. Mijadala, mahojiano na maoni tofauti ni sehemu ya demokrasia lakini bila ya kuharibu mali ya umma na kuvuruga hali ya kawaida ya maisha-"amesema waziri mkuu Modi kupitia mtandao wa twitter.

Maafisa wa serikali wamejaribu kuyavunja nguvu maandamano kwa kufunga mawasiliano mtandaoni.

Wito wa kusitishwa machafuko na kurejea kwa amani umetolewa pia na korti kuu inayotarajiwa kuamua kuhusu sheria hiyo mpya ya uraia Jumanne.


Chanzo: DW Swahili
 
Hiyo sheria ina mapungufu huwezi kuwanyima ukimbizi binadamu Kwasababu ya dini zao

Japokuwa kwenye Nchi za kiislam wasio waislamu wanapata mateso makubwa sana

Ukienda Iraq utawahurumia jinsi wakristo wanavyonyanyaswa ila jumuiya ya kimataifa imekaa kimya
 
Analogia Malenga,
... waislam wakimbie nchi za kiislam (Pakistan, Afghanistan, Bangladesh) kwenda kutafuta hifadhi sijui uraia nchi yenye makafir wengi kama India inaingia akilini kweli? Hao watakuwa wanaenda India kufanya ugaidi wao na sio zaidi ya hapo.
 
Back
Top Bottom