Maana yake nini hapa ma engineer?

Maana yake nini hapa ma engineer?

dem boyz

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2016
Posts
7,431
Reaction score
17,060
029f97388615b68c1ba9befc094766b0.jpg
nimeikuta hii mahali,wasomi wa haya mambo mtujuze kwa taratibu za ujenzi wa ma flyover hiyo round hapo ina maana yoyote au just wasted

Nadhani picha inajieleza vya kutosha.
 
Hiyo picha inaonyesha wangeweza kujenga straight road ila wao wakaizungusha!

What i see ni kwamba labda hapo chini kuna sehem walitaka ipitiwe na barabara...au wameweka hivyo kama kivutio kwa watalii au kupamba mji!!

NB: hamna kitu kinafanyika katika uhandisi kama hakina maana!!

EDIT:

Round imewekwa ili kuua steep slope. Ukiangalia upande wa kushoto road inaanza ikiwa juu kiasi flani na kama wangeweka straight path pangekua na slope kubwa sana. So ndio maana waka introduce hiyo round kama njia ya ku counteract steep slope ya barabara!!
 
Ungekua na plan ya njia husika ingenoga, hapo ujenzi unaendelea, yaani hiyo ya chini unayoiona iyavunjwa yote na kijengwa zingine zitazoendana na hiyo flyover

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kungekuwa na flow kubwa ndio maana wakaizungusha kupunguza flow taratibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaposema flow unamaanisha nini??

Lets assume unasemea velocity ya magari and the alike!!

Yet your point will not make sense maana kama shida ni speed then wangeweka hata bumps mi naona kwa kigezo hicho kuweka hiyo round haileti uhalisia!!
 
Huo mzunguko unasaidia kupunguza mteremko.
ukitumia hiyo michoro mbadala
kutakuwepo mteremko mkali na mlima mkali.
na ukitaka kuupunguza lazima barabara itakuwa ndefu na kuchukua nafasi kubwa.
hivyo suluhisho ni huo mzunguko.
 
Kama nnaona vizuri, upande wa kushoto ni kama vile kuna reli imepita chini. Nafikiri ilibidi kuinua upande huo wa barabara kuruhusu treni kupita. Huo mduara umetumika kushusha kimo cha barabara ili iendane usawa na hizi za upande wa kulia..

According to layman Engineer Samaritan
Well said.
 
wangeweza kuijenga moja kwa moja lakini mwinuko ungekuwa mkali sana afu ukizingatia hapo pembeni kuna kama leri.
 
Namaanisha mtelemko

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasemea velocity ya magari and the alike!!

Yet your point will not make sense maana kama shida ni speed then wangeweka hata bumps au road signs...mi naona kwa kigezo hicho kuweka hiyo round haileti uhalisia!!

Na ukivisualize vizuri utaona kutumia hiyo round kwa kigezo cha speed ndio unakua umehabu na kileta hatari zaidi!!
 
Huo mzunguko unasaidia kupunguza mteremko.
ukitumia hiyo michoro mbadala
kutakuwepo mteremko mkali na mlima mkali.
na ukitaka kuupunguza lazima barabara itakuwa ndefu na kuchukua nafasi kubwa.
hivyo suluhisho ni huo mzunguko.
nakubaliana na point yako japo mimi sii civil engineer
 
Mzunguko huo umepunguza mteremko wa gafla(steep slope) ambapo magari yangeshindwa kupanda au kushuka. Hiyo barabara ya juu imevuka reli ( nazani unajua urefu treni wa kwenda juu) ndani ya mita chache toka kwenye reli barabara hiyo ingetakiwa ishuke kama ulivyoweka alama , hiyo ingesababisha mkunjo down wa gafla ambapo gari zisingepanda au kushuka
 
Kama ukiangalia vizuri kutoka kwenye reli hadi kwenye hiyo main road si mbali sana, so ukitokea kwenye hiyo Overpass (Fly over) kwa kuwa distance ni fupi hadi kwenye hiyo road hapo so kama wangeunga moja kwa moja ingekuwa ni steep slope na kiusalama pale palipo na interchange (junction) haitakiwi kwa kuwa ipo considered kuwa wakati unashuka mlima afu mbele kuna junction na unatakiwa kusubiri unaweza kuteleza na ukasababisha ajali. So walichofanya hapo ni kuiua hiyo slope.
Ni sawa na kuwa na kona nyingi unavyopandisha mlima mkali mfano Kitonga, mara nyingi zile kona ni kwa ajili ya kupunguza muinuko (As a resting phase)

Sorry wakuu, siko vizuri sana kwenye kuelezea.
 
Back
Top Bottom