Maana ya rangi mbalimbali katika ulimwengu wa roho

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,835
MAANA YA RANGI MBALIMBALI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

RANGI NYEUPE
Hii ni rangi ya usafi, utakatifu, nuru, palipo na weupe hakuna chochote kinachoweza kusitirika, hata uchafu unaonekana kirahisi katika kitu cheupe, sehemu nyingi utaona Mungu anajitambulisha yeye kama mwenye mavazi meupe, kichwa cheupe na nywele nyeupe (Danieli 7:9, Ufunuo 1:14 ), na kiti chake cha enzi ni cheupe(Ufunuo 20:11), vilevile watakatifu watapewa mavazi meupe. (Ufunuo 3:5)

Mbingu pia ni nyeupe, Hivyo Mungu ukikutana na rangi hii, kwenye maandiko au kwenye maono sehemu kubwa ya ujumbe wake ni Utakatifu, au usafi war oho, au Uwepo wa Bwana.

RANGI NYEKUNDU

Hii ni rangi ya mwadamu, Adamu alitolewa katika udongo mwekundu, hivyo Mungu akamwita Adamu, Rangi hii pia ni rangi ya uhai, na maangamizo, hatari. Hivyo jambo kama hili ukiliona. Ujue upo umwagaji damu mbeleni au hatari fulani, au maangamizo mbeleni..Ukisoma Ufunuo 17, utaona yule mwanamke kahaba, Babeli mkuu akiwa ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, ikiashiria kuwa ni muuaji.

Ufunuo wa Yohana 17:1 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;

2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.

Unaona, ukisoma pia Ufunuo sura ya 6 utaona yule mpanda wa pili, akiwa amepanda farasi mwekundu sana, ikiashiria kuwa ataeleta mauaji vita n.k.

Ufunuo 6:3 “Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! 4 Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.”

Hivyo ukiona rangi hii ukiona rangi hii nyekundu kwa sehemu kubwa imetumika kama hatari, umwagikaji damu, au dhiki, au machafuko yapo mbeleni.

RANGI YA NJANO
Hii ni rangi inayowakilisha thamani ya kitu kilichotakaswa, ukisoma kitabu cha ufunuo utaona Mji ule Yerusalemu mpya njia zake zikiwa ni za dhahabu tupu (Ufunuo 21:18,21). Vilevile katika agano la kale vyombo vya madhabahuni vilivyokuwa ni vya dhahabu. Rangi hii pia inawakilisha moto, Moto hutakasa, na kusafisha, moto unamwakilisha Roho Mtakatifu.

Hivyo Rangi hii inasimama kama utakaso..Kitu kilichotakaswa, kimewekwa wakfu kwa ajili ya kazi fulani maalumu ya Mungu. Ni ishara kwamba kuna utakaso utapita ambapo utakufanya au kumfanya mtu awe thabiti kiimani kama dhahabu.

RANGI YA ZAMBARAU

Rangi ya zambarau Rangi kifalme, rangi za kikuhani, mavazi ya Haruni yalikuwa yamenakshiwa na rangi za zambarau. Kutoka 26:1. Hata wale askari waliomsulibisha Bwana Yesu, waliyatwaa mavazi ya kifalme ya zambarau na kumvika ili wamdhihaki.(Marko 15:17). Hivyo rangi hii inawakilisha ukuu, utawala, au mamlaka fulani.. Hata tuliposoma hapo juu habari za yule Babeli mkuu mama wa makahaba tumeona alikuwa amevaa nguo za rangi ya zambarau, kuonyesha ameketi katika kiti cha kitawala, kama malkia,..

Hivyo ukikutana na rangi hii ujue inazungumzia Ufalme, au utawala fulani.

RANGI NYEUSI

Rangi nyeusi Hii ni Rangi ya giza, uovu, upotevu, uchafu, . Siku zote giza ni jeusi..Na ndio maovu yote yanapofanyikia.(Yuda 1:13). Hivyo utakapokutana na rangi hii basi ujue inasimama kuonyesha ufalme wa giza na mamlaka ya shetani. Hivyo kama ni katika mazingira ya maono basi unapaswa umuulize Mungu ushindane vipi na hali hiyo, kwasababu zipo nguvu za shetani mbeleni.

RANGI YA KIJANI

Rangi ya kijani kibibliaRangi ya uhai,ustawi, ubichi, palipo na uhai pana ukijani, mvua ikinyesha juu ya nchi, majani yanayochipuka huonekana katika rangi ya kijani..na hivyo ni rangi inayoashiria neema na baraka kutoka kwa Mungu.

Mwanzo 1:11 “Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.

12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Hivyo ukikutana na rangi hiyo katika maandiko au katika maono basi ujue neema ipo mbeleni.

RANGI YA BLUU
Maana ya rangi ya bluu kibibliaHii ni rangi ya utukufu wa Mungu..nikiziangalia mbingu ni kazi ya vidole vyako (Zaburi 8:3)…Milima japo kwa karibu utaiona na rangi tofauti tofauti lakini ukiitazama kwa mbali utaona yote inabadilika na kuwa rangi moja ya bluu, vivyo hivyo hata na vyanzo vikubwa vya maji kama vile maziwa na bahari, ukiyatazama kwa mbali muonekana wao unabadilika na kuwa wa bluu..

Hivyo hii ni rangi ya utukufu wa Mungu.. Mungu kukuonyesha rangi hii basi ujue, Mungu anataka uuone utukufu wake. Usipoipenda rangi hii basi hii dunia itakuwa ya-kuboa sana kwako kwasababu popote utakapoutazama ukuu wa Mungu rangi hii utaiona.

RANGI YA KIJIVU
Hii inafunua mauti na kuzimu.

Ufunuo 6:7 “Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo!

8 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”.

Hivyo ikiwa utakutana na rangi kama hizi basi ujue hizo ndio maana zake kibiblia, Na kama tulivyosema, hakuna rangi iliyobora Zaidi ya nyingine tukizungumza kwa namna ya kawaida, usiache kuvaa nguo yako ya rangi nyeusi kwa hofu kuwa mapepo yatakuvamia, au rangi ya kijivujivu, hilo jambo halipo. Mungu akikuonyesha rangi fulani katika ndoto au maono au katika Neno lake basi ujue kuwa analengo la kukufundisha jambo fulani rohoni na sio mwilini.

MUNGU akubariki sana.
 
hizi ni stories. Science is the answer! PV=nRT formula hii hana ubishi

Kama science ni story, Panda juu ya mti ujiachie, you will face the wrath of acceleration of gravity!
Kama siasa sio sayansi, kwanini Kuna kozi ya political science chuo kikuu?
 
Back
Top Bottom