Habari wanajanvi na polen kwa majukumu,niende moja kwa moja kwenye mada,sio mara moja hua naota ndoto ambayo kiukweli sijui maana yake na hua inajirudia sana,hua naota napaa juu angani na ninakua ninauwezo wa kwenda popote na kufanya chochote,si mara moja inanitokea hii ndoto, tena kuna siku niliota wife kaniaga anaenda sehem kumuona mgonjwa eti nikapata mashaka nikaamua kupaa juu kama drone nakuanza kumfatilia bila yeye kujua,alifika anapoenda na mimi nikarudi zangu home,msaada kwa anaefahamu maana ya hii ndoto.