MAANA YA HII NDOTO NI NINI?

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
389
Habari wanajanvi na polen kwa majukumu,niende moja kwa moja kwenye mada,sio mara moja hua naota ndoto ambayo kiukweli sijui maana yake na hua inajirudia sana,hua naota napaa juu angani na ninakua ninauwezo wa kwenda popote na kufanya chochote,si mara moja inanitokea hii ndoto, tena kuna siku niliota wife kaniaga anaenda sehem kumuona mgonjwa eti nikapata mashaka nikaamua kupaa juu kama drone nakuanza kumfatilia bila yeye kujua,alifika anapoenda na mimi nikarudi zangu home,msaada kwa anaefahamu maana ya hii ndoto.
 
Hiyo ni kawaida sana kupaa mm nimeanza kuiota toka nipo na miaka 4 mpaka leo nimeota..
So usiogope japo ni moja ya dalili ya kua na majini, mapepo, Makongoro, miganzaruguru from rasi ya Congo..

Jichunguze kama kwenu kuna vitu hvyo au kama kana dalili zingine unazoziona mwilini then nambie nikufafanulie..

They are in my Body..!
 
Kupaa labda ni mafanikio ila sijui chochote kuhusu ndoto mkuu.

Ngoja waje wanaojua hayo
 
Nilishapaa sana nikachoka, na sasa nimeacha, maana niliichoka hiyo ndoto, nikaachana nayo. Haina maana yoyote.
 
MIMI NINAOTA NDOTO HZO TANGU NIKIWA STD I, NAENDA KOKOTE DUNIANI, NA KAMA ADUI ANANIFUATA HUWA NAOTA NAPAA KWA KASI HUKU SALA ZOTE NIKISALI KWA BIDII.

PIA, KAMA WAKIJA WACHAWI NDOTONI ZINANIJIA SALA HUKU NIKILITAJA JINA TAKATIFU LA YESU KRISTO, WACHAWI WANAKIMBIA.

KUPAA KAWAIDA MKUU, OMBA KATIKA KUPAA KWAKO YASIKUKUTE MAJANGA, KWA SABABU ROHO HUPAA ILA MWILI UNABAKI
 
Mi pia huwa napaa ila km nakimbizwa afu nikakutana na kuzuiz, mto,, nyumba,,fens basi huwa napaa nakuwaacha maadui hawana jinsi ya kunipata... Sasa sielewagi ni kiMunngu au vp
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom