Naombeni tafsiri ya ndoto hizi

Ionic banner

Member
Jul 19, 2023
5
9
Ni muda sasa nimekuwa napitia mazingira magumu sana ya kimaisha ajira ikiwa kwangu ni jambo lisilotatulika pamoja na kutegemewa na familia niliyonayo. Nimekuwa nikijitahidi sana kutafuta kazi kwa nguvu nyingi but naishia kuambulia patupu.

Jambo ambalo limekuwa likinikosesha raha ni namna ya ujumbe tofautitofauti ninaokuwa nikiupata katika ndoto mara kwa mara. Nimejaribu kutafsiri hizi ndoto mimi mwenyewe nimeishia kujihisi labda hii ni ishara ya ufura yaani umasikini uliopitiliza ndio utabiri wa maisha yangu ya mbeleni? Najiuliza.

Ndoto zenyewe ni wakati fulani naota nakutana na marundo ya mavi kila ninapoingia chooni. Mara naota naokota vimia-mia njiani, lakini wakati fulani nikaota mara niko na chawa sikioni. Sasa hii ndoto niliishangaa nikajisemea ndoto zingine bhana hazina adabu chawa sikioni? Ina maana sasa nimekuwa beberu alaa.

We mdau hii kitu unaisemaje?!
 
Back
Top Bottom