Maana ya alama zilizopo katika lebo ya nguo

Maana ya alama zilizopo katika lebo ya nguo

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,444
Reaction score
7,980
Katika Kila nguo huwa na lebo kwa ndani chini kidogo ya kola au pembezoni lebo ambayo huashiria maelezo ya kuitunza nguo hiyo ila wengi wetu huwa hatujui maana ya alama hizo, sio nguo zote huwa na maelezo ya alama nguo zingine huwa na maelezo tu japokuwa huandikwa kwa lugha kingereza au nguo zingine utakuta lugha tofauti inategemea imetengenezwa nchi gani. Japokuwa nyingi hutumia lugha ya kingereza.

Utunzaji wa nguo unaanzia kwenye Kufua, Kuipiga pasi na kuianika, lebo hizo zitakueleza unahitaji aina gani ya maji kufua nguo hiyo kama ni maji ya baridi au uvuguvugu. Unahitaji mashine au kufua kwa mkono, Upigaji wa pasi kama ni moto mkubwa, wastani au mdogo kabisa na kuianika kama ni juani, kuianika kwenye kamba au kuitandika sehemu tambarare. Kila nguo iko na masharti yake.

Je? Umeshawaza hawa madobi wa mitaani wanajua taratibu hizi za matunzo ya nguo au tunatumia mazoea kufua nguo zetu. Usilalamike nguo yako inapauka unajua taratibu za kuianika nguo hiyo? Mara nyingi nguo inayotoa Rangi inatakiwa kuanikwa sehemu ambayo haina jua ili kuzuia mpauko huo. Kwani sio jua pekee hukausha nguo hata upepo. Nguo za rangi nyeusi zinashauriwa kuanikwa sehemu ambayo haina jua sana au hakuna jua kabisa.

Aina ya maelezo hupatikana kwenye lebo za nguo .

Dry Clean Only – Ufue kwa mashine za kufulia tu

Do not Dry Clean – Usifue kwa Mashine za Kufulia

Do Not Bleach – Usitumie Dawa za kutoa Madoa

Do not Iron – Usipige pasi

Low Iron – Piga pasi kwa Moto mdogo

Do not Wring – Usikamue nguo hiyo

Dry in Shade – Anika kwenye kivuli (hii kwa nguo ambazo hupauka zikianikwa juani)

Tumble dry – Unaweza tumia mashine ya mvuke kukausha nguo hiyo

Hand Wash – Fua kwa Mkono

Mashine wash Normal – Unaweza kutumia mashine ya kufuli
pamba.jpg


Sent from my itel A16 using JamiiForums mobile app
 
Hizi options za kufua hapa nchini kwetu sidhani kama zinaweza kuwa practical kwa asilimia kubwa ya Wa-Tz.

Mtu anamiliki nguo hiyo hiyo kauka nikuvae, afu ameambiwa asiianike juani, sidhani kama ataweza..!
 
Kikubwa nimevaa ikichafuka sabun ya Puff inahusika
 
Hizi options za kufua hapa nchini kwetu sidhani kama zinaweza kuwa practical kwa asilimia kubwa ya Wa-Tz.

Mtu anamiliki nguo hiyo hiyo kauka nikuvae, afu ameambiwa asiianike juani, sidhani kama ataweza..!
Hapa hawajakuelewa...pls ongeza sauti.
 
Kwanza mie navikataga visiniletee jam kwenye nguo.
Muhimu imefuliwa na kunyooshwa ikavaliwa.
 
Hili halituhusu sisi labda huko juu!
Gharama za kufua kwa mashine ukifua nguo zote za familia budget ya mwezi mzima...
 
Ikiwezekana utuwekee kabisa zile alama ambazo uwekwa kwenye nguo na maana yake.
 
Back
Top Bottom