Kuna tofauti kubwa sana kati ya haya maneno mawili: Waathirika na Wahanga! Tatizo lililojitokeza ni kuwa waandishi, watangazaji na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiyachanganya haya maneno na kuyatumia bora liende! Yaani wakati mwingine natamani Mzee kifimbo cheza akatembeze bakora kule bungeni!
Wahanga ni watu waliojitolea na mara nyingi wakapoteza maisha yao katika hiyo shughuli (au kitu wao wanachokiamini sana): Mfano kuna wahanga wa mapinduzi ya Zanzibar- wao walijitoa muhanga mpaka hayo mapinduzi yakatokea. Hawakujali uhai au afya zao. Pia Kule msumbiji, Angola, nk wanakuwa na watu wao waiojitolea muhanga kwa nchi yao. Miaka ya karibuni kuna wahanga wa CUF pia, wao waliuwawa kwa imani ya chama chao cha siasa, piia wale wa Mwembechai enzi za Mzee Mkapa, na pia wapo hawa wa juzi kule Arusha! wote hao walijitoa muhanga kwa imani zao/ukereketwa wao.
Kuna yule bwana akiitwa Seti Benjamin (kama sikosei), JK Nyerere alipotangaza Azimio la Arusha, yeye na wenzake walitembea kwa miguu kuunga mkono, yeye akafia njiani-alijitoa muhanga na akawa mhanga!
Waathirika ni kama wale wa mabomu kule gongo la mboto au hawa wa mafuriko! Ni kutoelewa tu ndo kunafanya kila waitwe wahanga! Ila, kama yupo ambaye wakati mabomu yanaanza kulipuka alikimbilia kuyazuia au alijaribu kuokoa watu, na katika mchakato huo akaaga dunia atakuwa ni Mhanga, siyo muathirika.
Muathirika / waathirika ni mtu / watu walioathiriwa ni kitu fulani-mvua, vita, mabomu nk.
Mkuu, hapo nyekundu. kufariki na kupoteza maisha, tafauti iko wapi?1. wahanga, waathirika wa moja kwa moja
2. waathirika inajumuisha wale wa moja kwa moja na wassio wa moja kwa moja
mfano,
wahanga wa mafuriko ni waliokosa makazi, waliofariki kwa kuzolewa na mafuriko nk. lakini waathirika wa mafuriko ni wale waliopoteza maisha, mali zao nk pamoja na waliochelewa kufika majumbani au makazini kwao kwa sababu ya mafuriko kukata mawasiliano na wengine wote waliothirika kwa namna moja ama nyingine
Maelezo yako yanakubalika kabisa. labda kwa kuongezea tu ni kuwaKuna tofauti kubwa sana kati ya haya maneno mawili: Waathirika na Wahanga! Tatizo lililojitokeza ni kuwa waandishi, watangazaji na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiyachanganya haya maneno na kuyatumia bora liende! Yaani wakati mwingine natamani Mzee kifimbo cheza akatembeze bakora kule bungeni!
Wahanga ni watu waliojitolea na mara nyingi wakapoteza maisha yao katika hiyo shughuli (au kitu wao wanachokiamini sana): Mfano kuna wahanga wa mapinduzi ya Zanzibar- wao walijitoa muhanga mpaka hayo mapinduzi yakatokea. Hawakujali uhai au afya zao. Pia Kule msumbiji, Angola, nk wanakuwa na watu wao waiojitolea muhanga kwa nchi yao. Miaka ya karibuni kuna wahanga wa CUF pia, wao waliuwawa kwa imani ya chama chao cha siasa, piia wale wa Mwembechai enzi za Mzee Mkapa, na pia wapo hawa wa juzi kule Arusha! wote hao walijitoa muhanga kwa imani zao/ukereketwa wao.
Kuna yule bwana akiitwa Seti Benjamin (kama sikosei), JK Nyerere alipotangaza Azimio la Arusha, yeye na wenzake walitembea kwa miguu kuunga mkono, yeye akafia njiani-alijitoa muhanga na akawa mhanga!
Waathirika ni kama wale wa mabomu kule gongo la mboto au hawa wa mafuriko! Ni kutoelewa tu ndo kunafanya kila waitwe wahanga! Ila, kama yupo ambaye wakati mabomu yanaanza kulipuka alikimbilia kuyazuia au alijaribu kuokoa watu, na katika mchakato huo akaaga dunia atakuwa ni Mhanga, siyo muathirika.
Muathirika / waathirika ni mtu / watu walioathiriwa ni kitu fulani-mvua, vita, mabomu nk.
1. wahanga, waathirika wa moja kwa moja
2. waathirika inajumuisha wale wa moja kwa moja na wassio wa moja kwa moja
mfano,
wahanga wa mafuriko ni waliokosa makazi, waliofariki kwa kuzolewa na mafuriko nk. lakini waathirika wa mafuriko ni wale waliopoteza makzi, maisha, mali zao nk pamoja na waliochelewa kufika majumbani au makazini kwao kwa sababu ya mafuriko kukata mawasiliano na wengine wote waliothirika kwa namna moja ama nyingine
Mkuu, hapo nyekundu. kufariki na kupoteza maisha, tafauti iko wapi?