huyo mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga ni nani? Mbona anakuwa Mjinga hivyo, wakati watu waliopata maafa ya Ufisadi ni wa Mkoa wa Shinyanga, maana madini yamechukuliwa, wakati miundo mbinu ya mkoa ni duni, elimu duni, umeme kimeo etc
Nyepesi nyepesi zinazojiri kutoka NEC ya CCM Dodoma jana Spika Samwel Sitta kawekwa mtu kati kwa namna anavyolipeleka Bunge mpera mpera.
Miongoni mwa wachangiaji waliomshambulia wazi wazi ni Mwenyekiti wa CCM Shinyanga ambae bila kumung'unya maneno alimwambia Sitta alirudishe kadi ya CCM. Kwa ujumla wachangiaji wengi wameonyeshwa kutoridhiswa na utendaji wa Sitta isipokuwa wawili tu Eng Stellah Manyanya na Mh John Shibuda.
Chungu kimefunikwa na kikao kinaendelea leo ambapo tusishangae kusikia Sitta kasitishwa U-Spika.
Stay tuned...
Mh sitta pamoja na wewe una matatizo lakini wakitaka kadi yao wape ukaungane na Slaa upande wa pili. Tunahitaji nguvu upande wa pili
Duh, thubutu!!Mh sitta pamoja na wewe una matatizo lakini wakitaka kadi yao wape ukaungane na Slaa upande wa pili. Tunahitaji nguvu upande wa pili
Wana Jf taarifa zilizonifikia sashivi ni kwamba JK amemuita Sita na kumwambia kuwa hali ya ukumbi umeina nitakupa DK kumi ujiteteee ukizitumia vizuri utapona ukishindwa kuzitumia sitazuia wazo la wewe kutakiwa kurudisha kadi ya ccm.
Taarifa zaidi ni kuwa babu sita wapambe wote wamemkimbia hakuna anesimama kumtetea na anaonekana mpweke amebaki na mama sita ambae inaaminika anatiiza wajibu wa mke kwa mumewe.