Maamuzi ya Kawaida alafu unayaita Magumu!

Maamuzi ya Kawaida alafu unayaita Magumu!

Kwa kuwa ZZK ni jembe ambalo CCM wanalikubali, nadhani ni muda mwafaka wa kulichukua ndani ya siku hizi 14 na kuliweka sehemu husika ili likikatulie chama. Kama kiliwakimbilia Mwampamba na shonza kwa nini wasifanye maradufu kwa ZZK?. Kama kitasita basi tutajua kuwa lilikuwa jembe lao huko lilikotokomezwa.

Mkuu dalili zote zinaonyesha hata CCM wanamwogopa Zitto kwa kiwango chake cha usaliti ndio maana hawataki kumkaribisha kama walivyofanya kwa hao masalia uliowataja. Inawezekana Zitto kuna mambo kawafanyia huko Chadema mpaka waliomtuma wenyewe wameogopa. Unamtuma mtu ampige jiwe mwingine kesho anakwambia NIMEMCHINJA KABISA! Lazima umwogope kuwa huyu sio kabisa!
 
Nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kiongozi wa wana ccm kwazalendo kwenye mitandao napenda kuipongeza kamati kuu ya Chadema kwa mchukulia hatua kali za kinidahamu msaliti wa Chama na kiongozi wa wawasaliti ndani ya chadema.

Maauzi sahihi na ya kizalendo ya chadema yanapaswa kuigwa na wana CCM wote wa zalendo kwakuwahulia hatua kali mafisadi wa mali za watanzania

Hongera Chadema NA POLENI WANA CCM UZAO WA MAFISADI MNAOSIKITIKA NA KUSONONEKA

CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI SISI CCM TUUMIE INSTEAD YA KUFURAHIA?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI CCM TUWALAZIMISHE WAMPENDE?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWA NINI CCM TUSIMCHUKUE?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI CCM TUUMIE NA KUSONONEKA?

Viroba vya asubuhiasubuhi hivyo,na supu ya miguu ya kuku, Haya wahi kwenye maandamano.
 
Kwa kweli lazima tukubaliane kuwa hakuna aliye juu ya Chama.Chama kinatakiwa kuwa maarufu kuliko mtu.Ukiona hayo mawasiliano ya Nchimbi na Mwigulu utakubali kuwa kweli huyu Zito alikula pesa ya kuvuruga CDM na sasa ndio maana wanajitokeza kwa wingi kutoka malalmishi.Mpango wao umetibuka.Nadhani kama wanadhani Zito ni mtu maarufu na maalumu basi ni nafasi nzuri sana kumchukua na kumpa Uenyekiti ndani ya CCM.Kama kina Mtela na Juliana ni lulu ndani ya CCM seuze Zito jamani.Kwanini kuna kulia sana juu yake?Lazima tuamini kuwa kulikuwa n mkakati wa kukiua chama hiki kutokana na kuanza kuenea kwa watu kwa kasi.
 
Hongera Emmy kwa kuthubutu kusema kile ambacho huko CCM ni STRICTLY PROHIBITED
 
Nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kiongozi wa wana ccm kwazalendo kwenye mitandao napenda kuipongeza kamati kuu ya Chadema kwa mchukulia hatua kali za kinidahamu msaliti wa Chama na kiongozi wa wawasaliti ndani ya chadema.

Maauzi sahihi na ya kizalendo ya chadema yanapaswa kuigwa na wana CCM wote wa zalendo kwakuwahulia hatua kali mafisadi wa mali za watanzania

Hongera Chadema NA POLENI WANA CCM UZAO WA MAFISADI MNAOSIKITIKA NA KUSONONEKA

CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI SISI CCM TUUMIE INSTEAD YA KUFURAHIA?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI CCM TUWALAZIMISHE WAMPENDE?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWA NINI CCM TUSIMCHUKUE?, CHADEMA HAWAMTAKI ZITTO KWANINI CCM TUUMIE NA KUSONONEKA?

wewe si useme kama mimi cdm hila nimejivisha magamba ya ccm,puuuummmbaaavuuu....
 
Hebu tazama haya mawasiliano ya Mwigulu na Nchimbi kuhusu Zitto. CDM wako sahihi kumtimua Zitto!

Subject: Fw: kazi nzuri
Date: Sunday, November 17, 2013 20:28
From: " Mwigulu Nchemba " <shimbi85@gmail.com> >
To: “Emmanuel Nchimbi” < nchimbie@yahoo.com >

On Sunday, November 17, 2013 6:15:44 PM, Mwigulu Nchemba <shimbi85@gmail.com> wrote:

sawa boss,,jumatano saa moja imekaa safi kabisa. tuchape kazi. ntakupa update nikitoka kuonana na zzk. mh. Lukuvi namtafuta punde

MN

2013/11/17 Emmanuel Nchimbi < nchimbie@yahoo.com >

bila shaka vijana wamefanya kazi nzuri sana. mapambano yanaendelea, hakuna kulala, hapa sasa tume lote livunjwe na huyo waryoba apumzishwe. mtafute mh. Lukuvi ana mazuri ya kuongea na wewe. kuna mapya pale ufipa, nimeshaongea na mh. zitto na amenipa brifieing .. tukutane jumatano basi jioni ya saa1 pale pale cheer,, Emma

Sent from my ipad

On Sunday, November 17, 2013 5:55:02 PM, Mwigulu Nchemba <shimbi85@gmail.com> wrote:

Naona vijana wametekeleza shuguli vizuri, na cham imewakilishwa vizuri sana. Msangi jembe, sasa tutaipata katiba tunayoitaka hicho kikwazo kikishaondolewa bila shuruti. Alafu upande wa pili (cdm) inabidi tuongeze dau ili shujaa zzk abakie ndani, nasikia kuna mkakati wa kumtoa kwenye kinyang'anyiro. tujitahidi sana sana kumsaidia kujenga mtandao wa ndani apate u wenyekiti. taarifa zaidi za ndani zinasema wkamba wanajaribu kumfukuza kabla ya mwisho wa mwaka, tuendeleze vita hilo lisitokee, naona kundi ndani ya bavicha hasa hiyo mitoto inafanya sana mashambulizi lakini hawataweza. inabidi wadhibitiwe. rockup wiki mbili itawasambaratisha. Tuongeze kasi kwa wajumbe wa kamati kuu. wengi wao ni njaa sana nazani 5mil kila moja inatosha kabisa.wananifata sana kuomba hela ili wasaidie nakutana na ZZK baadae plae pa siku ile, unaweza kufika saa 1 jioni

MN

Endeleeni ila mtaula wa chuya
​

duh!zzk kumbe ww ni fisi aliyejivika ngozi ya migebuka jamani
 
Sitakuwa najadili sana uhalali wa kuondolewa kwa Zito Kabwe au la. Nitakuwa najadili uthubutu uimara na wa chama. Wote tunakubali kuwa Zito Kabwe ni maarufu kwa watu wengi. Lakini kwamba CHADEMA wamethubutu kufanya maamuzi magumu ni jambo la kupongezwa. Suala la kaonewa au hapana hilo kila chama kina vikao vyake vya kupima uhalali au uonevu.

Chama kikubwa kama chama cha mapinduzi kimekuwa kila mara kinapiga kelele za kuchukua hatua lakini wanasuasua. Mapacha watatu walikuwa wachukuliwe hatua, mpaka leo ni kigugumizi.

Ikafika wakati wa kuvua gamba lakini gamba halitoki. Ikafika wakati wa kuwachukulia hatua walipata madaraka kwa rushwa. Hakuna kilichofanyika.

Tuhuma kila kukicha lakini hakuna hatua.

Ninasikitika kuona mtu wa CCM anathubutu kuongelea hatua ya kamati kuu.

Nawapongeza CHADEMA kwa ujasiri na uthubutu wa kutokuogopa kuchukua hatua mnayoamini ni kinyume na maadili yenu.

MNAFAA KUAMIMINIWA NA WANANCHI KUWA PAKIWEPO NA TUHUMA MTACHUKUA HATUA BILA WOGA.

CCM igeni mfano huo. Fanyeni maamuzi magumu kwa wanaoharibu sifa ya chama.
 
Nadhani hujaelewa ujumbe. Narudia kuwa ccm wajifunze angalao kusimamia maadili hata wakionekana wameonea kuna taratibu za kumpatia mtu aliyeonewa haki yake.
 
Ipo siri moja kubwa sana ya demokrasia.. Yaani mabadiliko lazima yatokane na demokrasi yenyewe na si uporaji wa madaraka au demokrasi kama walivyotaka kufanya kina MM.MM1,MM2 na MM3. Mawazo yao yalipaswa yafuate mkondo wa chama au wajitoe chamani na kuanzisha chama chao kipya kitakachoongozwa na mtazamo mpya walioouandika kwenye kabrasha lao...kinyume cha hivyo..hayo ni mapinduzi ambayo hayana tofauti na yale ya kijeshi la kutumia mtutu na MM group walitaka kutumia Itikikadi kinzani. Kama mawazo hayajakubalika basi ujue na ukubali kwamba wakati wake bado. Hiyo ndio tofauti ya mapindui ya kijeshi na mabadiliko katika demokrasia.
 
Unataka wamfukuze EL mkuu?

Hiki chama kimefika ukomo na kutekwa na mabepari wauza ndovu na sembe

Wapumzike ili tuwaoneshe kuona wasikoona tena
 
Hata wasipoweza kuwafukuza mafisadi basi wenzao wanapothubutu wanyamaze
 
Sitakuwa najadili sana uhalali wa kuondolewa kwa Zito Kabwe au la. Nitakuwa najadili uthubutu uimara na wa chama. Wote tunakubali kuwa Zito Kabwe ni maarufu kwa watu wengi. Lakini kwamba CHADEMA wamethubutu kufanya maamuzi magumu ni jambo la kupongezwa. Suala la kaonewa au hapana hilo kila chama kina vikao vyake vya kupima uhalali au uonevu.

Chama kikubwa kama chama cha mapinduzi kimekuwa kila mara kinapiga kelele za kuchukua hatua lakini wanasuasua. Mapacha watatu walikuwa wachukuliwe hatua, mpaka leo ni kigugumizi.

Ikafika wakati wa kuvua gamba lakini gamba halitoki. Ikafika wakati wa kuwachukulia hatua walipata madaraka kwa rushwa. Hakuna kilichofanyika.

Tuhuma kila kukicha lakini hakuna hatua.

Ninasikitika kuona mtu wa CCM anathubutu kuongelea hatua ya kamati kuu.

Nawapongeza CHADEMA kwa ujasiri na uthubutu wa kutokuogopa kuchukua hatua mnayoamini ni kinyume na maadili yenu.

MNAFAA KUAMIMINIWA NA WANANCHI KUWA PAKIWEPO NA TUHUMA MTACHUKUA HATUA BILA WOGA.

CCM igeni mfano huo. Fanyeni maamuzi magumu kwa wanaoharibu sifa ya chama.

kama mtu alikuwa anawaletea gozigozi kwenye upigaji kwanini wasifanye maamuzi magumu
 
Back
Top Bottom