Maalumu kwa wanaume wanandoa

Fibanochi

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
475
1,015
Habari wanajamvini, ni matumaini yangu mnaendelea vyema na majukumu yenu.

Embu twende moja kwa moja kwenye hoja, hivi wewe kama mume ndani ya nyumba yako, pindi mwenzako anapofanya tukio la kukukera, linaweza kuwa kubwa sana au la kawaida, lakini ikabaki kuwa amekwazika sana na alichofanya. Je, huwa unatumia njia gani kutatua?

Ni wazi na ukweli usiopingika kuwa kila ndoa ina changamoto yake, kitendo cha kukaa au kuishi nyumba moja na mke kwa muda mrefu, huleta hali fln hv ya kuchokana au kuonana wa kawaida, na hadi kuepelekea wanawake wengine kutotimiza majukumu yao ya ki ndoa na kimahusiano Kama ilivyokuwa awali. Ni ngumu sana kuwa na muendelezo wa mapenzi au uhusiano imara kwa wana ndoa kwa muda mrefu, hata kama kuna vitu mtakuwa mnavifanya ili kurutubisha mapenzi au ndoa yenu, bado kuna mmj wenu au wote atakuwa mnafiki, na hupelekea kusababisha kutokea kwa makosa kadhaa kwenye ndoa au mahusiano.

Mfano wa makosa hayo yanaweza kutokea Ni Kama dharau toka kwa mke, kuchepuka, kutokuthamini mume ( mke hafanyi tena mmb kwa ajili ya mume), kujibishana na mume, n.k, hali zote hizi husababisha hasira isiyoelezeka, ikifikia hatua hii ndipo kila mwanaume huwa na njia yake ya ku "deal" na changamoto hy.

SWALI:
Wewe huwa unafanyaje kati ya haya?

Unampiga mwanamke kutuliza hasira na hujishughulishi ku sort tatizo?

Unakaa chini na kujadiliana nae?

Unauchuna tu?

Unamfukuza arudi kwao?

Unalipa kisasi?

Unatafuta watu wa kuwasuluhisha, Kama wazazi, mshenga, viongozi wa dini, Wana familia n.k?

Je, unaamini katika kupiga mwanamke ndy suluhisho au ndy kuongeza petrol ktk moto? Kama hupigi nini huwa unafanya ku prove ur point?

Embu funguka .
 
me Ed Kawiche sijaoa ila kuna matatizo makubwa yanayofanywa na hawa viumbe (ke) hata kusalitiwa linaweza kuwa tatizo dogo sana! huwa wanaivuruga saikologia ya mwanaume kwa kiwango kikubwa sana.
kwa kawaida mwanamke anaongozwa external foce, matatizo mengi anayoyasababisha chanzo huwa marafiki, ndugu na wengne wanaofanana na hao. inshu ni mwanaume kupambana na hyo external forces ni ngumu kwa sababu (ke) akiamini jambo lolote nje atalishikilia hilohilo mpaka yamkute ndyo ataanza kujirudi mwenyew na kuanza kutubu.
 
katika ndoa......yaani kati yenu nyie mtu mbili.........peke yenu ndio mnaweza kuyamaliza matatizo na migogoro yenu pasina shaka........mmoja wenu akianza kupeleka nje kwa namna ya kushtaki, kutafuta huruma au kujipendekeza........hapo hakuna ndoa..ni anaongeza mgogoro.......only 2 peoples....wife & husband......wa 3 iblisi nakwambia...........hakuna kupigana wala kuchuniana.......mkiona hakika mmeshindwa..........kanza anzeni kujiuliza mlipoanza kudate...........kitu kikubwa mkeo awe ni your best friend......rafikiyo mkuu.....safari yenu itakuwa nzuri.....
 
Nipo na wewe katika hili.

Alafu anaejua uzito au wepesi wa tatizo ni yule aliekutwa nalo, na sy 3rd part utakaemuelezea. Ukimueleza mtu mwingine atakupa jibu la short cut tu sababu ya generalization, either akwambie muache wanawake au wanaume wako wengi, au Kama kaenda kwa marriage counselor atamwambia hapo hakuna ndoa, kisa amekuta massage ya ajabu au umechepuka mara moja, au hata amemsimulia issue ya zamani, au wakati mwingine kwa yeye mwanamke kutojiamini akahisi Kuna kitu tofauti unafanya. Ki msingi matatizo ya ndoa yanakuwa yanachochewa zaidi na wanawake kuliko sisi wanaume.
katika ndoa......yaani kati yenu nyie mtu mbili.........peke yenu ndio mnaweza kuyamaliza matatizo na migogoro yenu pasina shaka........mmoja wenu akianza kupeleka nje kwa namna ya kushtaki, kutafuta huruma au kujipendekeza........hapo hakuna ndoa..ni anaongeza mgogoro.......only 2 peoples....wife & husband......wa 3 iblisi nakwambia...........hakuna kupigana wala kuchuniana.......mkiona hakika mmeshindwa..........kanza anzeni kujiuliza mlipoanza kudate...........kitu kikubwa mkeo awe ni your best friend......rafikiyo mkuu.....safari yenu itakuwa nzuri.....
 
Mkuu mm nipo nje ya mada kidogo na sijaowa, ila mwaka Jana mwez wa 12 nilienda kwenye ndoa ya ndugu yangu, cha kushangaza juzi nikapokea taarifa kuwa yule ndugu tayari alishaachana na mke wake tena wameshaachana siku nyingi nilishangaa sana nikihesabu ile ndoa haijafika hata miez 6.
Lakin pia hili suala la ndoa nyingi kuvunjika kadri miaka inavyozid kwenda ndo linazidi kukuwa , wanawake wengi nikipitia huko insta, Twitter maneno wanayolishana ni ya kuzikaanga ndoa zao wenyewe kwa wenyewe.
 
Yaani kuchepuka nalo ni kosa katika makosa ambayo anategemewa Mke ayafanye siku hizi?
Na la kuomba ushauri?
Mkuu ndoa ni taasisi ngumu na nzito Sana, ndani ya ndoa Kuna mengi sana yanatokea kiasi mengine ukiambiwa unaweza baki mdogo wazi.....unaweza usiombe ushauri lkn ikabaki kuwa limetokea na ni choice yako wewe sasa kuishi nalo au vinginevyo. Ndoa za siku hz zinamb mengi ya ajabu sana mkuu.

Kama umeskia, hv karibuni Kuna msanii wa kuitwa Stamina, amemsamehe mke wake, pmj na kulalamika kusalitiwa na huyo mke wake, kiasj akatunga mpk verse khs usaliti huo. Ila Cha ajabu leo wameyajenga na inasemekana wamerudiana.
 
Mkuu mm nipo nje ya mada kidogo na sijaowa, ila mwaka Jana mwez wa 12 nilienda kwenye ndoa ya ndugu yangu, cha kushangaza juzi nikapokea taarifa kuwa yule ndugu tayari alishaachana na mke wake tena wameshaachana siku nyingi nilishangaa sana nikihesabu ile ndoa haijafika hata miez 6.
Lakin pia hili suala la ndoa nyingi kuvunjika kadri miaka inavyozid kwenda ndo linazidi kukuwa , wanawake wengi nikipitia huko insta, Twitter maneno wanayolishana ni ya kuzikaanga ndoa zao wenyewe kwa wenyewe.
Unatakiwa uwe matured enough ili uweze kudumu au kuhimili mikikimikiki ya ndoa, huyo ndugu yako kuachana baada ya meiezi 6 huwenda Kuna sababu lukuki zimepelekea hy Hali ikiwemo kubwa kumuoa mtu asiemjua vyema.
 
Mkuu ndoa ni taasisi ngumu na nzito Sana, ndani ya ndoa Kuna mengi sana yanatokea kiasi mengine ukiambiwa unaweza baki mdogo wazi.....unaweza usiombe ushauri lkn ikabaki kuwa limetokea na ni choice yako wewe sasa kuishi nalo au vinginevyo. Ndoa za siku hz zinamb mengi ya ajabu sana mkuu.

Kama umeskia, hv karibuni Kuna msanii wa kuitwa Stamina, amemsamehe mke wake, pmj na kulalamika kusalitiwa na huyo mke wake, kiasj akatunga mpk verse khs usaliti huo. Ila Cha ajabu leo wameyajenga na inasemekana wamerudiana.
Wasanii wengi ni kiki Tu na kuzusha jambo

Mwanamke akusaliti halafu wewe uombe msamaha mrudiane?Ina make sense?
 
Ndoa ni taasisi kama nyingine
Kila upande uki cheza vema nafasi yake hakuna mbwayi
Ila mkurugenzi anataka kuwa mlinzi na mlinzi kuwa mkurugenzi hapo hakuna ndoa
Pia 3rd party ni mwiba wa ndoa nyingi especially kwa wanawalke
Ila akikushinda mwache aende usipige utaishia jela bure mambo yako na kids waparaganyike
 
me Ed Kawiche sijaoa ila kuna matatizo makubwa yanayofanywa na hawa viumbe (ke) hata kusalitiwa linaweza kuwa tatizo dogo sana! huwa wanaivuruga saikologia ya mwanaume kwa kiwango kikubwa sana.
kwa kawaida mwanamke anaongozwa external foce, matatizo mengi anayoyasababisha chanzo huwa marafiki, ndugu na wengne wanaofanana na hao. inshu ni mwanaume kupambana na hyo external forces ni ngumu kwa sababu (ke) akiamini jambo lolote nje atalishikilia hilohilo mpaka yamkute ndyo ataanza kujirudi mwenyew na kuanza kutubu.
Tatizo ni mwanamke kukuvuruga au ni wewe kukubali kuchezeshwa ngoma?
 
Msingi mkuu wa yote hayo ni kosa la kuchagua mke. Kuna mahali nilisema mke wa ndoa anapaswa kutambua kuwa ndoa sio uwekezaji wa 50/50. Ili ndoa idumu ni LAZIMA kuwe na clear line kati ya mke na mume, kwamba ni nani mwenye ndoa!!

Sasa kwa ndoa za kisasa ambapo mwanamume na mwanamke wana hisa sawa kwenye ndoa, inahitaji mke mwenye busara na malezi bora mno. Wengi wanaingia wakiwa na mtazamo wa kiuanaharakati ndani ya ndoa ndio products za kina Kiria hizo.

Nikisema mume awe mume namaanisha kwamba mke anatakiwa atambue wazi kuwa maisha yake yanategemea ndoa, kwamba bila ndoa basi dunia kwake ni chungu. Kama ukioa mke ambaye ana mtazamo wa kuwa ukiona sifai nirudishe kwetu, basi jua hukupata mke bali mwanamke. Siku hizi kuna ujinga fulani umetamalaki, kwenye send off ni kawaida kusikia wazazi wa mwanamke wakisema binti huyu hajafukuzwa kwao, hivyo ukiona kakushinda mrudishe kwa amani. Ukisikia kauli kama hiyo jua mwanamke huyo atabaki na connection na watu wa kwao na atakusumbua kweli.

Nikija kwenye swali lako, mke akikuletea hayo wala hakuna haja ya kuita vikao, MWONYE. Wewe ni mume, umetoa mahali kujenga mji wako sio wenu. Akikusikia umepata mke, la hajakusikia basi jua iko sauti anayoisikiliza huko nje, yaweza kuwa kidume au mashoti zake. Hapo sasa kama atakuwa anarudia na kuleta dharau na kiburi KUWA MWANAMUME. Mrudishe kwao akapumzike kwanza, hilo litamshitua mno kama ni mke anayestahili ndoa, tena hawezi kucheza na mambo yako ya msingi.

Mwanamke ukimruhusu akudharau basi jiandae kwa maumivu makubwa zaidi. Lazima ajue kuna mahali umechora mstari na kwamba hatothubutu kuuvuka. Akishajua hilo atakuheshimu na ataogopa kukuletea ujinga. Lakini kumbuka wewe pia unapaswa kuwa mume mwenye kujitambua.
 
Wasanii wengi ni kiki Tu na kuzusha jambo

Mwanamke akusaliti halafu wewe uombe msamaha mrudiane?Ina make sense?
Mkuu ni kweli wasanii wetu wanapenda Sana mmb ya kiki, na pengine hili ikawa ni moja wapo. Ila tukirudi katika maisha ya kawaida ya wanandoa ukweli utabaki kuwa ni kweli kuna wanaosamehe baada ya mke kuchepuka, na sy mmj Ila hii itabaki kuwa Siri ya chumba. Na hapo ndipo inapokuja suala la namna gani kila watu tofautitofati hutatua changamoto za kindoa. Na siku zote ndoa inayopitia changamoto nyingi ndy inayodumu sana.
 
Msingi mkuu wa yote hayo ni kosa la kuchagua mke. Kuna mahali nilisema mke wa ndoa anapaswa kutambua kuwa ndoa sio uwekezaji wa 50/50. Ili ndoa idumu ni LAZIMA kuwe na clear line kati ya mke na mume, kwamba ni nani mwenye ndoa!!

Sasa kwa ndoa za kisasa ambapo mwanamke na mwanamke wana hisa sawa mwenye ndoa, inahitaji mke mwenye busara na malezi bora mno. Wengi wanaingia wakiwa na mtazamo wa kiuanaharakati ndani ya ndoa ndio products za kina Kiria hizo.

Nikisema mume awe mume namaanisha kwamba mke anatakiwa atambue wazi kuwa maisha yake yanategemea ndoa, kwamba bila ndoa basi dunia kwake ni chungu. Kama ukioa mke ambaye ana mtazamo wa kuwa ukiona sifai nirudishe kwetu, basi jua hukupata mke bali mwanamke. Siku hizi kuna ujinga fulani umetamalaki, kwenye send off ni kawaida kusikia wazazi wa mwanamke wakisema binti huyu hajafukuzwa kwao, hivyo ukiona kakushinda mrudishe kwa amani. Ukisikia kauli kama hiyo jua mwwnamke huyo atabaki na connection na watu wa kwao na atakusumbua kweli.

Nikija kwenyebswali lako, mke akuleta hayo wala hakuna haja ya kuita vikao, MWONYE. Wewe ni mume, umetoa mahali kujenga mji wako sio wenu. Akikusikia umepata mke, la hajakusikia basi jua iko sauti anayoisikiliza huko nje, yaweza kuwa kidume au mashoti zake. Hapo sasa kama atakuwa anarudia na kuleta dharau na kiburi KUWA MWANAMUME. Mrudishe kwao akapumzike kwanza, hilo litamshitua mno kama no mke anayestahili ndoa, tena hawezi kucheza na mambo yako ya msingi.

Mwanamke ukimruhusu akudharau basi jiandae kwa maumivu makubwa zaidi. Lazima ajue kuna mahali umechora mstari na kwamba hatothubutu kuuvuka. Akishajua hilo atakyheshimu na ataogopa kukuletea ujinga. Lakini kunbuka wewe pia unapaswa kuwa mume mwenye kujitambua.
Wewe unaishi ndoa za kale za mabibi
 
Umemaliza kila kitu mkuu!
 
Hapana me naona yuko sahihi, ili ndoa iweze kuwa na ustawi lazima kusiwe na balance, yaani haitakiwi kuwe na 50/50 Kama mdau alivyosema. Lazima mwanaume awe juu, mwanaume mtu wa mwisho kimaamuzi. Hii haimanishi mwanaume ambuluze mwanamke, au amuonee hapana, hapa inakusudiwa kuwa kauli ya mume iwe ya mwisho na iheshimiwe. Haiwezekani me nakwambia supendi nione unafanya kitu fln, eti we kwasababu una uwezo na resources za kufanya unafanya.

Na unapomkataza mwanamke aache kufanya kitu fulani lazima utoe sababu za msingi na madhara ambayo yatasababishwa na yeye kufanya hicho kitu unachomkataza. Siyo unaamua tu kumkataza eti kwa sababu wewe ni mwanaume huo sasa ndiyo uonevu wenyewe.
 
Hapana me naona yuko sahihi, ili ndoa iweze kuwa na ustawi lazima kusiwe na balance, yaani haitakiwi kuwe na 50/50 Kama mdau alivyosema. Lazima mwanaume awe juu, mwanaume mtu wa mwisho kimaamuzi. Hii haimanishi mwanaume ambuluze mwanamke, au amuonee hapana, hapa inakusudiwa kuwa kauli ya mume iwe ya mwisho na iheshimiwe. Haiwezekani me nakwambia supendi nione unafanya kitu fln, eti we kwasababu una uwezo na resources za kufanya unafanya.
Huko ni kutokujiamini ni Nani alisema mwanaume awe juu na mwingine chini bila kuheshimiana hyo haipo eti mwanaume awe juu hata Kama anafanya utopolo, lazima mubadilike ndoa nikusikilizana na kushauriana, Sasa nyie wanaume mnataka muonee wanawake eti ili ndoa idumu kwanini nyie msiwe sehemu hyo mnatolea wababu mfano wakati walikuwa wajinga tu .
Ili ndoa idumu lazima mpendane, mhurumiane mheshimiane, msikilizane hyo ya kuwa juu ni Chaka letu wanaume kuendekeza ukandamizaji tu kwa wanawake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom