Mwanaume au mume kuwa juu haimanishi kuwa ni ticket ya kumuonea mke, au haimaanishi kuwa hakuna upendo, amani, n.k la hasha. Mwanaume kuwa juu maana yake ni kuwa mwanaume au mume awe kiongozi wa nyumba. Mnaweza sikilizana, heshimiana n.k sawa, lkn mwanaume nafasi yake ya yeye kuwa mtu wa mwisho kwenye maamuzi liwepo. Mbona hili hata kwenye vitabu vya dini lipo wazi na hata kiasili lipo hvy. Ndy maana sisi tunatoa mahali, tunawanunulia mashela kipindi Cha kufunga ndoa..... Yaani hii ni fact.
Binafsi siamini katika kumkandimiza au kumuonea KE, hapana, Naamini katika kuridhiana, kuheshimiana, kuvumiliana, n.k! Lkn pia Naamini ya kuwa mwanaume ndy kiongozi wa familia.
Huwezi wewe mke, ukamkaribisha rafiki yako/zako uliesoma nae shule bila ya kunipa Mimi taarifa. Au hauwezi wewe kwenda kwa mfano kuchora tatoo mwili wako bila ya kunipa Mimi mumeo taarifa hata Kama ni mwili wako.