Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Katika watu ninaowaona hawafai kuwa katika uongozi wa nchi hii ni Jussa na Seif..yaani kwao wanatumia mwanya wa kujulikana na nguvu zao kisiasa kufikia malengo yao binafsi na wala siyo ya nchi...
 
yaana kama anataka passport ya Zanzibar ajue kabisa na mashamba yake aliyonayo huku arudishe..yaani watu wengine point zao zikiisha ndio wanaanza kuhamisa Uamsho na mambo mengine. Bora tuwe kama North Korea sasa maana siasa yetu siyo kabisa.
 
Nasema, lazima Serikali ya Chama Changu Murua iing'ang'a Zanzibar katika Muungano kwani huko ndiko zitokako kura za ushindi usiodhibitika. Lasivyo hakuna sababu ya kuilazimisha Znzbr kubaki ktk muungano isiyoutaka.

Mungano ni kwa faida ya waunganao. Sasa mmoja ktk kuungana anasema haioni faida hiyo. Jamani kwanini tuendelee kumlazimisha?
 
nani anakwamisha ama kuna vitu vyao wameviweka huku bara wanataka tuwape? Na arusha alifuata nini?
 
Bado anatafuna maneno! Seif hajatamka kuvunja muungano. Hayo ni maneno ya kutafuna.
Amesema tunataka ujirani mwema kama ule wa Kenya, safi sana! halafu anakula matapishi yake kwa kusema tunataka mkataba na Tanganyika.

Huyu mwanasultani anawavuruga WZNZ hadi waonekane majuha. Ukitaka uhuru unavunja muungano, period.
Unaporudi kusema unataka mkataba ni upuuzi wa kiwango cha kimataifa. Mkataba wa nini nawe unataka uwe huru.

Sisi Tanganyika tunasema hatutaki mkataba, tunataka muondoke zenu!
Mwambieni Seif hoja za kupiuuzi za mkataba mwisho Chumbe! Hatuiihitaji ZNZ jamani!

Seif Sharif Hamad anauma maneno, futa neno mkataba katika hotuba zako weka neno muungano uvunjwe.
 
Vijana wengi wa znzbr hawaupendi pia Muungano. Ambao wanaongea positive kuhusu Muungano ni we walioajiriwa ktk Serikali ya JMT kwa hofu ya kupoteza ajira zao. Huku bara, vijana pia hawautaki muungano lkn hawawezi kulisema hilo kwa uwazi kwa kuogopa kisigino cha chuma.

Ukiwa Bara, Kuzungumzia kuvunjwa kwa Mungano ni kuzungumzia kuitoa CCM madarakani. Kwa maana hiyo huwrxi kumkuta kijana wa Bara akitamka wazi kutoutaka muungano. Lasivyo, vitimbi na maudhui ya katiba ya znzbr ni kielelezo mwafaka kwamba hawa watu hawautaki muungano na wamekwishaanza safari kuelekea kujitenga.

Tukizidi kuwalazimisha iko siku tutakuta WAMEAMUA. Kwa hali ilivyo, its only a matter of time, iko siku muungano utayeyuka kama siyo kuyeyushwa

Huyu ni Mpemba na wapemba hawatakiwi Unguja na hawapendwi hili liko wazi so wauguja ndio hawataki kuvunja muungano ni wapemba tu... na wamanga..

Kumbe Watanganyika ndio wamezuia uchimbaji wa mafuta Zanzibar duh Sijalijua hili!!!!
 
Huyu Ndio alikuwa Arusha Juzi kuwaambia vijana kuwa wamalishwa Viroba.....Huku akitumia Ndege ya Tanganyika .........na kupewa heshima zote....,Kumbe nia yake atumalize.......Hajui anachokitaka...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Bado anatafuna maneno! Seif hajatamka kuvunja muungano. Hayo ni maneno ya kutafuna.
Amesema tunataka ujirani mwema kama ule wa Kenya, safi sana! halafu anakula matapishi yake kwa kusema tunataka mkataba na Tanganyika.

Huyu mwanasultani anawavuruga WZNZ hadi waonekane majuha. Ukitaka uhuru unavunja muungano, period.
Unaporudi kusema unataka mkataba ni upuuzi wa kiwango cha kimataifa. Mkataba wa nini nawe unataka uwe huru.

Sisi Tanganyika tunasema hatutaki mkataba, tunataka muondoke zenu!
Mwambieni Seif hoja za kupiuuzi za mkataba mwisho Chumbe! Hatuiihitaji ZNZ jamani!

Seif Sharif Hamad anauma maneno, futa neno mkataba katika hotuba zako weka neno muungano uvunjwe.

Mkataba mwisho Chumbe... ha ha ha haaaa.

Maalim inabidi aanze kuongea sasa baada ya pazia la Uamsho kuondolewa. Mwezi ujao kuna kikao cha bunge la muungano, kama kweli anataka uhuru na akiwa kama makamu wa kwanza wa SUK awaambie wabunge wa Zanzibar hawana ruhusa ya kupanda boti.
 
Tung'ang'ani kitu gani? Si tuachane nao muungano gani ambao sisi bara hatuoni tija yake? Pamoja na kwamba sera ya CCM ni kulinda muungano nadhani ipo haja ya kuujadili muungano huu kwa mapana na marefu, hatuwezi kuendelea na muungano kwa shinikizo za kisiasa ni ukweli usiofichika muungano ni mzigo kwetu, ikiwa wao wanaona eti Bara tunawala tuawaachie binafsi sijawahi kufaidika na matunda ya muungano huu ila nawafahamu wapemba na waunguja wanaonufaika na muungano huu wengi tu.
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkataba mwisho Chumbe... ha ha ha haaaa.

Maalim inabidi aanze kuongea sasa baada ya pazia la Uamsho kuondolewa. Mwezi ujao kuna kikao cha bunge la muungano, kama kweli anataka uhuru na akiwa kama makamu wa kwanza wa SUK awaambie wabunge wa Zanzibar hawana ruhusa ya kupanda boti.

FJM,

..hawawezi kugoma kuhudhuria vikao vya bunge la muungano.

..yaani waache mishahara na posho za ubunge kwa ajili ya ZNZ??
 
Only last week Maalim alikwenda Arusha kwa ndege ya Tanganyika! Then anafika huko (Arusha) na kuwambia vijana wanaolipa kodi ya kununulia mafuta ndege iliyomleta, kuwa wanakunywa viroba!

Nadhani muda umefika sasa kila akija Tanganyika watu wamuulize -anafuata nini?
 
Bado anatafuna maneno! Seif hajatamka kuvunja muungano. Hayo ni maneno ya kutafuna.
Amesema tunataka ujirani mwema kama ule wa Kenya, safi sana! halafu anakula matapishi yake kwa kusema tunataka mkataba na Tanganyika.

Huyu mwanasultani anawavuruga WZNZ hadi waonekane majuha. Ukitaka uhuru unavunja muungano, period.
Unaporudi kusema unataka mkataba ni upuuzi wa kiwango cha kimataifa. Mkataba wa nini nawe unataka uwe huru.

Sisi Tanganyika tunasema hatutaki mkataba, tunataka muondoke zenu!
Mwambieni Seif hoja za kupiuuzi za mkataba mwisho Chumbe! Hatuiihitaji ZNZ jamani!

Seif Sharif Hamad anauma maneno, futa neno mkataba katika hotuba zako weka neno muungano uvunjwe.

Ha ha haa..nao povu linafoka , taratibu usije ukadondoka chini...Muache Maalim Seif atumie uhuru wake wa ki-demokrasia. Bado mawazo ya kidikteta yanakusumbua, yamemshinda baba wenu...
 
Sasa serikali ya umoja wa kitaifa cuf na ccm yanini? Mnajua ccm wanataka muungano kwani ni sera yao.
 
Huyu Maalim Seif bado hajitambui kisiasa amesiamamia mlango gani naona atakuwa Bukoba j4 kwa nini kwenye hiyo mikutano asihamasishe agenda yake ya kutaka uhuru wa Zanzibar?
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Only last week Maalim alikwenda Arusha kwa ndege ya Tanganyika! Then anafika huko (Arusha) na kuwambia vijana wanaolipa kodi ya kununulia mafuta ndege iliyomleta, kuwa wanakunywa viroba!

Nadhani muda umefika sasa kila akija Tanganyika watu wamuulize -anafuata nini?

Umesahau hata hewa avuta kutoka Tanganyika ....Brain washed.
 
Mkataba mwisho Chumbe... ha ha ha haaaa.

Maalim inabidi aanze kuongea sasa baada ya pazia la Uamsho kuondolewa. Mwezi ujao kuna kikao cha bunge la muungano, kama kweli anataka uhuru na akiwa kama makamu wa kwanza wa SUK awaambie wabunge wa Zanzibar hawana ruhusa ya kupanda boti.
Maalimu kashindwa kutmaka neno vunja muungano, kuna mbunge gani atakayethubutu?

Unajua baada ya hoja ya Seif ya serikali 3 kudadavuliwa hapa JF alijiona dhalili, sijui iliishia wapi.
Sasa wanataka mkataba. Nakuhakikishia siyo Maalim, Ahmed, Jusa au awaye atakayeweza kutamka hata jambo moja la huo mkataba.

Siri kubwa ya mkataba ni kutaka kujificha nyuma ya mgongo wa Tanganyika.
Maalimu amesema eti bidhaa za ZNZ zinatozwa ushuru zikiingia bara. Alichotaka ni kuwa ziingie ZNZ, SMZ ichukue kodi halafu ziingie bara kama zimetoka Tabora. Kwamba soko la Waarabu lisiwe na kodi huku bara.

Seif anafahamu kuwa soko la ZNZ ni Tanganyika, nje ya muungano ni maumivu.
Tena soko si la biashara, ni pamoja na ardhi. ajira n.k.

Hakuna taifa lolote duniani lililowabeba WZN wengi kama Tanganyika.
Hakuna taifa linaloajiri WZNZ kwa upendeleo kama Tanganyika
Hakuna taifa linalosemesha WZNZ bure kama Tanganyika
Hakuna taifa linalotoa nishati ya bure ZNZ kama Tanganyika.
Hakuna taifa linalogharamia ulinzi na usalama wa ZNZ kama Tanganyika

Ikifika hapo, wote wananywea in fact wanaufyata kutamka neno vunja muungano kama alivyoufyata Seif.
Tanganyika ni ya ajabu sana, tumewabeba hawa watu halafu tunawapa muda wa kucheza msewe mgongoni.
LET THEM GO! Period.

Tanganyika inanufaika na nini na serikali 3 ua mkataba na ZNZ!

Maalim Seif Sharif Hamad Mshirazi, bado unauma maneno tena sana. Toa neno mkataba katika hotuba zako weka neno vunja muungano! hapo tutakuelewa kinyume chake unakula matapisha yale yale.

Mwisho wa mkataba ni Chumbe, baada ya kuvuka hapo nidhamu na adabu mbele!
 
Ha ha haa..nao povu linafoka , taratibu usije ukadondoka chini...Muache Maalim Seif atumie uhuru wake wa ki-demokrasia. Bado mawazo ya kidikteta yanakusumbua, yamemshinda baba wenu...

takashi, huo sio uhuru wa demokrasia bali ni usanii. Anataka uhuru lakini wakati huo huo anataka 'ndege' ya kumtembeza Tanganyika!

Kama anataka uhuru kwanini kesho asubuhi asiwa-summon wabunge wa zanzibar (walioko bunge la muungano), mawaziri toka zanzibar pamoja na VP na kuwaambia 'face to face' kwamba kuanzia sasa wako 'huru', hawatakiwi tena kuhudhuria vikao au kufanya kazi kwa 'mkoloni'?
 
Umesahau hata hewa avuta kutoka Tanganyika ....Brain washed.

Tatizo Maalim anafikiri yeye ni smart sana. Sasa kama kweli yeye ni mwanaume na haumi maneno, aseme maneno mawili tu - "Vunja Muungano".
 
takashi, huo sio uhuru wa demokrasia bali ni usanii. Anataka uhuru lakini wakati huo huo anataka 'ndege' ya kumtembeza Tanganyika!

Kama anataka uhuru kwanini kesho asubuhi asiwa-summon wabunge wa zanzibar (walioko bunge la muungano), mawaziri toka zanzibar pamoja na VP na kuwaambia 'face to face' kwamba kuanzia sasa wako 'huru', hawatakiwi tena kuhudhuria vikao au kufanya kazi kwa 'mkoloni'?

Siku itafika Muungano utavunjika tu, sio kwasababu ya Maalim Seif bali wazanzibari walio wengi wamechoshwa na usanii wenu. Maalim Seif ni mtu mmoja, akiwepo asiwepo harakati za ukombozi zitaendelea mpaka kieleweke.

Kasumba za Nyerere ndio zinawasumbua...
 
Only last week Maalim alikwenda Arusha kwa ndege ya Tanganyika! Then anafika huko (Arusha) na kuwambia vijana wanaolipa kodi ya kununulia mafuta ndege iliyomleta, kuwa wanakunywa viroba!

Nadhani muda umefika sasa kila akija Tanganyika watu wamuulize -anafuata nini?

Kodi yapombeincluding viroba wanavyokunywa vijana ndo vimenunua mafuta ya ndege iliyompeleka Arusha.

Huyu jamaa ni zuzu kweli kweli.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom