Maalim Seif: Nimekusanya matokeo kutoka vituo vyote ninaongoza, aitaka ZEC imtangaze mshindi

attachment.php

Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni.


Amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni.

Chanzo: DW






"Mm na familia yangu tumeamua kwenda Saudi Arabia nyinyi wananchi huku kataeni matokeo hasaaaa, Sawa Sawa? " Majuha yanaitikia... "Sawa Sawa"
 
Last edited by a moderator:
Mbowe yuko wapi atuwekee zetu, hapa hakuna kuzidiana akili.

Yaani unastuka sasa hivi? Wewe wakati unapigwa na jua kuungana na wana ukiwa wenzako kutengeneza mafuriko yasiyokuwa na tija Mbowe tayari ameshamaliza kazi yake kwa kukusanya kilichochake. Sasa hivi anasubiri bingo part II kupitia ruzuku ya wabunge. Makubaliano yalikua mamvi kufa ama kupona na uraisi, akishindwa terms za biashara yao inaishia hapo
 
yaani Seif nibumbra huo ndio ubeti wake kila anapishindwa huko znz. lakini sasa watu wamekomaa nafujo haiwezi kutokea
 
Ameshinda ila shein hataki kusign papers source ni wazanzibar wenyw!! Kuwah kujitangaza ni strategy ya kulinda ushindi na haki yake. Ingekua kadanganya ZEC wangeshatoa tamko mapemaaaaaa


Na Mbowe afanye hivyo Tanganyika.
 
Eeewaa.

Hakuna haja kabisa.

Ni upotevu wa rasilimali tu.

Hatuna chaguzi zilizo huru sisi.

Huwezi ukawa na chombo cha kusimamia na kuendesha chaguzi ambacho kinaundwa na mwenyekiti wa moja ya vyama vinavyoshiriki hizo chaguzi.

Huo ni umajununi.


Hii ndio nafasi ya mwisho kwa Ukawa.
Its now or never.
Ninavyoona hiyo tume huru hatutapata CCM wakishinda.
 
Ameshinda ila shein hataki kusign papers source ni wazanzibar wenyw!! Kuwah kujitangaza ni strategy ya kulinda ushindi na haki yake. Ingekua kadanganya ZEC wangeshatoa tamko mapemaaaaaa

CCM wameshaanza kutayarisha hali ya kukataa matokeo kwa kuanza kuwalaumu Tume kwamba hawakuwa na mawakala katika jimbo kubwa ndani ya Zanzibar eti kwa sababu tume hawakutoa vitambulisho kwa mawakala wao.

Huu utakuwa mpango wameupanga na ZEK ili kuhalalisha kurudia uchaguzi katika jimbo hilo halafu watumie nguvu ya dola kuua watu na kuiba kura ili zibadilishe ushindi wa CUF kuwa wa CCM.

Seif yuko makini sana. Amelijua hilo tangu zamani ndio maana kawahi kutoa matangazo ambayo mpaka sasa ZEK haijayakanusha kwa sababu ndio hayo hayo yalio sahihi na yaliyoripotiwa kwenye vyombo vyote vya habari pamoja na redio.

Kwa sasa CCM inasikilizia upepo wa bara kwani wakiweza kuchakachua bara kama wanavyojitahidi kufanya kwenye majimbo mbalimbali kama ilivyoripotiwa leo huko Mbeya kwa gari lenye kura feki kukamatwa na wananchi na gari hilo kuvunjwa vioo kabla polisi hawajaingilia kati na kuwaokoa wahalifu basi wakati huo watahakikisha wanatumia uhalifu wao huo huo kulazimisha kuharibu uchaguzi Zanzibar ili wamuweke Shein badala ya Seif.

Sasa Serikali ya CCM iamue ama iwe tayari kuleta machafuko na kuua watu wasio na hatia kwa ajili ya kung'an'gania madaraka au itoe haki ya kura zilizopigwa na Wazanzibari kwa kuheshimu matakwa yao.

Viongozi wakuu wa CCM waliostaafu na wanaoenda kustaafu sasa hivi wajue kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, maisha ambayo hatima yake wataiamua wenyewe sasa hivi. Ama watumie ubabe kuuwa watu na kulazimisha ushindi usio wao na hivyo kujijengea uadui kote nje na ndani ya nchi, au wawe wastaarabu kama vile Jonathan ambaye ni Mwangalizi wa Kimataifa wa uchaguzi huu ambaye alikuwa Rais wa Nigeria na kukubali kuachia madaraka kwa amani kwa mpinzani wake, kitu ambacho kimempa heshima ambayo matunda yake anayaona kwa sasa kwa kuheshimiwa na kuaminiwa dunia nzima na ndio maana yupo hapa kama Mwangalizi wa Uchanguzi wetu.
 
Unajua mimi nilivyomsikia maalim seif anatangaza ushindi mchana nikajua ni zile ngonjera zake za kawaida. Ila baada ya kuona ZEC wamekaa kimya mda wote huu bila kukanusha..naanza kuona kama kuna ukweli hapa.
 
Unajua mimi nilivyomsikia maalim seif anatangaza ushindi mchana nikajua ni zile ngonjera zake za kawaida. Ila baada ya kuona ZEC wamekaa kimya mda wote huu bila kukanusha..naanza kuona kama kuna ukweli hapa.
Matokeo ngome za cuf unguja yamebanwa hadi muda huu.
 
Hii ndio nafasi ya mwisho kwa Ukawa.
Its now or never.
Ninavyoona hiyo tume huru hatutapata CCM wakishinda.

Oh yeah, tume huru hatuwezi kuipata maana hata watu ambao mtu ulidhani wangekuwa mstari wa mbele kuipigania bado wanaiona hii tuliyonayo kuwa ni huru kisa tu eti kwa vile majaji nao wanachaguliwa na rais huyo huyo wa CCM [as if hilo jambo nalo ni sawa!].

Na Watanzania wengi mno wana ujinga na ujuha uliokithiri hivyo hata uwaelezeje, walio wengi wala hawatakuelewa. Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa tu.

Ndo maana mpaka sasa niko sahihi nikisema kwamba CCM itatawala Tanzania milele.

CCM kuwa chama tawala kilichokaa madarakani kwa muda mrefu kuliko vyama vingine Afrika siyo bahati wala ngekewa.

Kina mtaji mzuri sana wa kisiasa ambao ndo unakifanya udumu hadi kwa miaka 60 sasa.
 
Back
Top Bottom