EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hakuna mambo yaliyoainishwa kuwa ni matakatifu ambayo hayatakiwi kuguswa wakati wa kujadili Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano, hivyo aliwataka Wazanzibari wajiandae kutoa maoni yao juu ya Katiba wanayoitaka, ikiwamo mfumo wa Muungano wenye masilahi kwao.
Alisema kutokana na Rais Jakaya Kikwete kutia saini muswada uliopitishwa na wabunge kuhusu katiba mpya, hatua inayofuata ni kuundwa tume ya kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba hiyo, na wananchi wanapaswa kujiandaa kutoa maoni bila woga, bali la muhimu ni kuhakikisha katika maoni yao hawatoi lugha chafu.
Alisema tume hiyo itakayokuwa na wajumbe wanaotoka Zanzibar na Tanzania Bara, itatoa fursa ya kipekee kwa wananchi wa Tanzania, hivyo itakuwa nafasi ya kipekee kwa Wazanzibari kueleza nini wanataka, likiwamo suala la mfumo au muundo wa Muungano.
Nyinyi Wazanzibari na ndugu zetu wa Tanzania Bara ndio tuliovaa kiatu (Muungano) na aliyevaa kiatu ndiye anayejua msumari unachomea wapi, au anayelala kwenye kitanda ndiye anayejua kunguni wake, alisema Maalim Seif.
Hata hivyo, alisema kwamba litakuwa ni jambo la maana zaidi Wazanzibari wakiwa na msimamo mmoja juu ya mambo wanayotaka katika katiba mpya na waweke kando itikadi zao za kisiasa katika jambo hilo.
Alieleza kwamba ni vema wakaendelea na na msimamo kama ule waliouonesha wakati wa kutoa maoni juu ya rasimu ya muswada wa katiba mpya ulioandaliwa mara ya kwanza, kabla ya kuwasilishwa bungeni, ambapo Wazanzibari kwa kauli moja waliupinga na ukarekebishwa.