Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Taarifa zilizotufikia zimeeleza kwamba, Rais wa Zanzibar, Dr Ali Mohamed Shein amemteua Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, na Balozi Seif Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais.
============
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 39 (1),(2) na (3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Mhe. Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Kwaza wa Rais.
Taarifa fupi kutoka Ikulu ya Zanzibar kwa waandishi wa Habari, Dk Shein pia ametumia uwezo wake kwa mujibu wa kifungu 39(1),(2) na (6) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Kumteua Mhe. Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais.
Uteuzi wa balozi Iddi ambao umeanza tarehe 09 Novemba, 2010 haukutarajiwa hasa baada ya kushinda kiti cha ubunge jimbo la Kitope kwa ticket ya CCM. Kabla ya kuteuliwa Seif Iddi alikuwa naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.