Maalim Seif kalianzisha, Hamad Rashid Kamaliza

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Salaam WanaJF!

Natumai sote tumeshuhudia rais wa Zamzibar akizindua baraza la wawakilishi huku mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid akiteuliwa barazani.Siku zinaenda kasi...Hamad Rashid akiwa kiongozi mwenye ushawishi CUF na bungeni alimpinga Maalim Seif mwaka 2010 kuingia ubia na CCM hadi kupelekea kuundwa zengwe kumtimua.

Ikumbukwe pia Chadema walikataa kushirikiana na CUF bungeni kisa SUK huko zanzibar,Tundu Lissu aliueza umma na Dunia kwamba kushirikiana na CUF ni sawa na kushirikiana na CCM na kabla kidonda hakijapona Wenje akiwa bungeni aliueleza ulimwengu kuwa CUF wanafungamana na siasa zinazokubali ushoga...dah ilikuwa tafrani nusura achapike.

Hamad Rashid alilazimika kuhamia ADC huku ndoa ya Seif na CCM ikiyumba,mwishowe Hamad Rashid kaunga mkono uchaguzi wa marudio na kwa sasa ni kiungo muhimu barazani kama ilivyokuwa Seif kabla ya uchaguzi mkuu.

Je kati ya Seif,CUF na Hamad Rashid nani mnafiki....?...tuchangie huku tukizingatia misingi ya uhuru wa kufungamana kisiasa.

Kuntu
 
Bila CUF kushiriki Hamad amepata 3% bila mwakilishi wala diwani hata mmoja unawezeje kumfananisha na nguli Seif
Hayo mengine kwa kuwa wewe ni novice kwenye siasa hujui there's no permanent friends or foes jifunze toka Marekani
 
Salaam WanaJF!

Natumai sote tumeshuhudia rais wa Zamzibar akizindua baraza la wawakilishi huku mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid akiteuliwa barazani.Siku zinaenda kasi...Hamad Rashid akiwa kiongozi mwenye ushawishi CUF na bungeni alimpinga Maalim Seif mwaka 2010 kuingia ubia na CCM hadi kupelekea kuundwa zengwe kumtimua.

Ikumbukwe pia Chadema walikataa kushirikiana na CUF bungeni kisa SUK huko zanzibar,Tundu Lissu aliueza umma na Dunia kwamba kushirikiana na Cuf ni sawa na kushirikiana na CCM na kabla kidonda hakijapona Wenje akiwa bungeni aliueleza ulimwengu kuwa CUF wanafungamana na siasa zinazokubali ushoga...dah ilikuwa tafrani nusura achapike.

Hamad Rashid alilazimika kuhamia ADC huku ndoa ya Seif na CCM ikiyumba,mwishowe Hamad Rashid kaunga mkono uchaguzi wa marudio na kwa sasa ni kiungo muhimu barazani kama ilivyokuwa Seif kabla ya uchaguzi mkuu.

Je kati ya Seif,Cuf na Hamad Rashid nani mnafiki....?...tuchangie huku tukizingatia misingi ya uhuru wa kufungamana kisiasa.

Hii ina ihusiano wowote na hali ya sasa ya kisiasa?inaleta suluhu yeyote juu ya uchafuzi wa 20th march?kama majawabu ni hapana tafuta unaofanana nao akili mujadili hii hoja!
 
Sasa Hamad Rashid kafaidika kitu gani zaidi ya kuiondolea heshima,mwanaume kutoka kuchaguliwa mpaka kuteuliwa unamsifia......aende barazani akapiganie haki za wateuliwa wenzie ndo kilichobaki....ila amepoteza hata ile heshima ndogo aliyobaki nayo
 
Bila CUF kushiriki Hamad amepata 3% bila mwakilishi wala diwani hata mmoja unawezeje kumfananisha na nguli Seif
Hayo mengine kwa kuwa wewe ni novice kwenye siasa hujui there's no permanent friends or foes jifunze toka Marekani

Naona mada hujaielewa....kifupi mleta kaeleza unafiki wa wana siasa wetu.

Hawaishi kwenye hoja zao kifupi ni vigeugeu.

Hivi mwaka 2011 ulitegemea Lowasa angekua shujaa wa Chadema hadi kugombea Urais 2015.?
 
Tatizo mnakuwa na kumbukumbu kidogo sana, mbona Mbatia alipata nafasi kama hiyo na alifanya alichoamini na watu wakashangaa!
 
Wewe unafananisha Mbatia na mtu aliyekuwa mwakilishi kwa miaka 40,mbunge wa jamhuri kwa kuchaguliwa?? Mtu aliyekuwa anatabiriwa kuwa urais wa Zanzibar baadaye,tumia akili usijitie kujua kila kitu
 
Mtoa mada unadanganya.

Hamad Rashid hakulazimika kujiunda ADC kwa hiari alifukuzwa CUF hilo ulijuwe.

Hamad Rashid hakupinga CUf kujiunga kwenye SUK, alifanya usaliti wa wazi kwa tamaa ya madaraka.

Tukija kwenye mada sasa. mimi sioni wapi Hamad Rashid kapatia. Kilichotokea Zanzibar ni kusinyaa kwa demokrasia na kuuliwa dhana nzima ya mamlaka ya wananchi katika kubadilisha utawala.

Hamad na wenzake wametumia Opportunity yenye madhara kwa Umma na Zanzibar yote. Precedence iliyowekwa na kuzalisha uongozi batili zanzibar unamuweka Hamad na Shein katika daftari jeusi la KUVUNJA KATIBA na MARIDHIANO.

Tayari wameingia katika historia mbaya.

Sioni Faida yoyote ya maana katika mizania ya haki, usawa, utu mna demokrasia.

Huu ni msiba kwa vyama vyote vya siasa HASA UPINZANI TANZANIA.

SI YA KUFURAHIA.
 
Naona mada hujaielewa....kifupi mleta kaeleza unafiki wa wana siasa wetu.

Hawaishi kwenye hoja zao kifupi ni vigeugeu.

Hivi mwaka 2011 ulitegemea Lowasa angekua shujaa wa Chadema hadi kugombea Urais 2015.?
Mheshimiwa
Nimezungumzia sehemu mbili la andishi lake hayo mengine kwangu hayana maana wala sikuona mantiki ya kuyajibu
 
Na kama kuna mtu anadhani kwamba alichokifanya Hamad Rashid ni sawa anajidanganya. Kundi hili ni lile lile tu kama la wana CCM Zanzibar.
Wako pale kwa madaraka tu na maslahi binafsi.

Utawezaje kuvunja katiba na maridhiano yaliyowekwa kwa kupigiwa kura ya maoni kwa hoja nyepesi eti " makamo wa kwanza hakuridhiwa na wananchi ndio maana hakuna chama kilichopata asilimia 10" shame.

wanajitoa fahamu kwamba uwepo wa makamo wa kwanza na wa pili sharti la kikatiba.

wewe unamsifia Hamad Rashid anayelipwa fadhila za kushiriki batili.

Wakati utasema
 
Hiyo post yako yenyewe pumba kuna sehemu umesema ndoa ya ccm na cuf ndiyo nini hapo kabla ya kujadili tufanye wewe ndiyo mnafiki namba moja
 
Bila CUF kushiriki Hamad amepata 3% bila mwakilishi wala diwani hata mmoja unawezeje kumfananisha na nguli Seif
Hayo mengine kwa kuwa wewe ni novice kwenye siasa hujui there's no permanent friends or foes jifunze toka Marekani
Sasa Hamad Rashid kafaidika kitu gani zaidi ya kuiondolea heshima,mwanaume kutoka kuchaguliwa mpaka kuteuliwa unamsifia......aende barazani akapiganie haki za wateuliwa wenzie ndo kilichobaki....ila amepoteza hata ile heshima ndogo aliyobaki nayo
Hamad anawafuasi wengi na ushawishi kiasi cha kutosha hadi ndani ya CUF.
Wana CUF wamemfuata Maalim na kususia uchaguzi, baada ya kuyaona makosa na mapungufu ya Maalim katika mikakati yake kisiasa, wengi watayarudia maonyo ya Hamad na influence ya Maalim itapungua kwa zaidi ya nusu.
Ingawa tungependa iwe tofauti, lakini mwenendo wa viongozi wakuu wa upinzani katika uchaguzi mkuu umekatisha tamaa wengi. Haswa katika hatua walizotumia kuhakikisha hawaporwi ushindi na muendelezo wa mapambano ya kisiasa baada ya hapo.
 
Salaam WanaJF!

Natumai sote tumeshuhudia rais wa Zamzibar akizindua baraza la wawakilishi huku mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid akiteuliwa barazani.Siku zinaenda kasi...Hamad Rashid akiwa kiongozi mwenye ushawishi CUF na bungeni alimpinga Maalim Seif mwaka 2010 kuingia ubia na CCM hadi kupelekea kuundwa zengwe kumtimua.

Ikumbukwe pia Chadema walikataa kushirikiana na CUF bungeni kisa SUK huko zanzibar,Tundu Lissu aliueza umma na Dunia kwamba kushirikiana na Cuf ni sawa na kushirikiana na CCM na kabla kidonda hakijapona Wenje akiwa bungeni aliueleza ulimwengu kuwa CUF wanafungamana na siasa zinazokubali ushoga...dah ilikuwa tafrani nusura achapike.

Hamad Rashid alilazimika kuhamia ADC huku ndoa ya Seif na CCM ikiyumba,mwishowe Hamad Rashid kaunga mkono uchaguzi wa marudio na kwa sasa ni kiungo muhimu barazani kama ilivyokuwa Seif kabla ya uchaguzi mkuu.

Je kati ya Seif,Cuf na Hamad Rashid nani mnafiki....?...tuchangie huku tukizingatia misingi ya uhuru wa kufungamana kisiasa.

Kuntu

Afrika bana ndo mana vita haviishi kuendekeza chuki tu badala ya ushaur wa kujenga taifa unaongelea mambo yaliyopita lengo lako ni nn cuf wawachukie chadema? Au chadema wasiongee na cuf au cuf wasikosolewe bila kukosolewa ccm magufuli angetumbua majipu? Yupo serikalini kitambo tena wazir umewah kumsikia kamtimua aliyechini yake kwa matumiz mabaya ya ofis? Au wizara ya ujenzi hakukua na makanjanja? … Huwez kufanikiwa bila changamoto hujafanikiwa hata kuwa balozi wa nyumba kumi moyoni umejaa chuki na kumbukumbu za maovu ukipewa ubaloz si utagawa wanakijiji wewe siasa hazina uadui tukiendekeza uadui taifa haliwez kuwa moja kamwe hasa chuki ya siasa na udini ni mbaya sna leo zanzibar wakianza kupigana jua hatuponi kamwe.
 
Hamad anawafuasi wengi na ushawishi kiasi cha kutosha hadi ndani ya CUF.
Wana CUF wamemfuata Maalim na kususia uchaguzi, baada ya kuyaona makosa na mapungufu ya Maalim katika mikakati yake kisiasa, wengi watayarudia maonyo ya Hamad na influence ya Maalim itapungua kwa zaidi ya nusu.
Ingawa tungependa iwe tofauti, lakini mwenendo wa viongozi wakuu wa upinzani katika uchaguzi mkuu umekatisha tamaa wengi. Haswa katika hatua walizotumia kuhakikisha hawaporwi ushindi na muendelezo wa mapambano ya kisiasa baada ya hapo.

Looooo!!! Leo hamad unaushawish hadi ndani ya CUF? Nitajie watu wawili aliohama nao baada ya kufukuzwa CUF tujue huo ushawishi wake!!
 
Hamad anawafuasi wengi na ushawishi kiasi cha kutosha hadi ndani ya CUF.
Wana CUF wamemfuata Maalim na kususia uchaguzi, baada ya kuyaona makosa na mapungufu ya Maalim katika mikakati yake kisiasa, wengi watayarudia maonyo ya Hamad na influence ya Maalim itapungua kwa zaidi ya nusu.
Ingawa tungependa iwe tofauti, lakini mwenendo wa viongozi wakuu wa upinzani katika uchaguzi mkuu umekatisha tamaa wengi. Haswa katika hatua walizotumia kuhakikisha hawaporwi ushindi na muendelezo wa mapambano ya kisiasa baada ya hapo.
Hamna shida ukiamua kujifurahisha kwa maneno
 
Hamadi huwezi mfananisha na Maalim hata siku moja. Kama angekuwa na umaarufu huo asingepata zile kura za aibu ambazo hazikufika hata asilimia moja, na hakuna hata muwakilishi wake mmoja aliefanikiwa kuingia katika barazaa la wawakilishi, Hamad hawezi kung'ara sana sana anachafuka tu, ngestaafu angekuwa shujaa sio kutembelea nafasi za usaliti.
 
Salaam WanaJF!

Natumai sote tumeshuhudia rais wa Zamzibar akizindua baraza la wawakilishi huku mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid akiteuliwa barazani.Siku zinaenda kasi...Hamad Rashid akiwa kiongozi mwenye ushawishi CUF na bungeni alimpinga Maalim Seif mwaka 2010 kuingia ubia na CCM hadi kupelekea kuundwa zengwe kumtimua.

Ikumbukwe pia Chadema walikataa kushirikiana na CUF bungeni kisa SUK huko zanzibar,Tundu Lissu aliueza umma na Dunia kwamba kushirikiana na Cuf ni sawa na kushirikiana na CCM na kabla kidonda hakijapona Wenje akiwa bungeni aliueleza ulimwengu kuwa CUF wanafungamana na siasa zinazokubali ushoga...dah ilikuwa tafrani nusura achapike.

Hamad Rashid alilazimika kuhamia ADC huku ndoa ya Seif na CCM ikiyumba,mwishowe Hamad Rashid kaunga mkono uchaguzi wa marudio na kwa sasa ni kiungo muhimu barazani kama ilivyokuwa Seif kabla ya uchaguzi mkuu.

Je kati ya Seif,Cuf na Hamad Rashid nani mnafiki....?...tuchangie huku tukizingatia misingi ya uhuru wa kufungamana kisiasa.

Kuntu
Wote wanafiki hakuna wa afadhali,lengo ni kiti cha pale karibu na hospitali ya Mnazi mmoja
 
Back
Top Bottom