Nijuavyo mimi nakala za matokeo ziliztiwa saini na mawakala wa pande zote zinawasilishwa kwa Tume ya uchakuzi kama ushahidi kuwa matokeo yale ni halali na yamethibitishwa na pande zote shindani. Washindani wote wanasubiri Tume iyafanyie mchakato ikiwa ni kuhakiki, kuyajumlisha na aadaye kumtangaza mshindi. Nakala za matokeo za mawakala zinaweza kutumika kama kutakuwa na malalamiko yoyote. Sheria iko wazi mwenye mamlaka ya kutanganza mshindi ni Tume na siyo mshindania nafasi katika uchaguzi. Mimi ninavyoona na kwa maoni yangu ni kosa kumpatia matokeo mgombea mmojawapo kabla ya Tume kumtangaza. Msingi wa Maalim Seif kujitangaza mshindi kunatokana na kupewa matokeo kabla ya Tume. Tukiruhusu mgombea kujianga mshindi kuna hatari siku moja Maalim Seif atajiapisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya kuapishwa na Jaji kama sheria inavyotaka. Jambo hili msilione kwa wepesi kiasi hico mchelea mwana kulia hulia yeye. Hapa kuna uvunjivu wa sheria ulio wazi kabisa. Ikiwa Maalim Seif anagombea tu, hajawa Rais, akiwa Rais itakuwaje? Yeye mwenyewe atavunja sheria, pia atashindwa kuwaambia wasaidizi wafuate sheria. Nchi itakuwa ya vituko kweli kweli.
Lakini huyu huyu Maalim Seif katika kipindi cha utawala wa Abdul Jumbe amewahi kuvujisha siri za serikali mapinduzi ya Zanzibar. Mtu asiye tii sheria, asiyefuata maelekezo ya boss wake, asiyetii hata miongozo anakuwa rais wa namna gani? Kila uchaguzi anang'ang'ania kwenda Ikulu, ameweka nini. Nakumbuka nilipokuwa shule vijana wakorofi walikuwa wakipendwa zaidi na wanafunzi wenzao, isije ikawa na huyu anapendwa kwa ukorofi wake, lakini si kwa kuwaletea maendeleo wazanzibar. Maneno mengi mdomoni siyo mojawapo ya sifa za kiongozi bora