Maalim Seif: Haturudii Uchaguzi

Maalim Seif: Haturudii Uchaguzi

Ni ngumu sana kudhani kwamba Uchaguzi hautarudiwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Tume hii ina wawakilishi toka CCM na CUF.

Tume ndiyo inatangaza matokeo toka majimbo lalini Tume ndiyo inafanya kazi ya kuandikisha wapiga Kura kabla ya Uchaguzi, hii ina maana gani? Tume ina idadi ya wapiga Kura wote kwa idadi ya Majimbo na vituo vya kupiga Kura.

Endapo itatokea tofauti ya wapiga Kura hasa kama idadi yao itaongezeka Tume itafuta Uchaguzi hiyo ni Haki yake.

Tume imetoa sababu 9 kwa nini imefuta Uchaguzi

1. Makamishna walivua mashati ili kutwangana makonde
9. Idadi ya wapiga Kura ilikua kubwa kuliko waliojiandikisha.

Ktk hali hiyo kinachotakiwa ni tafsiri tu ya Katiba kuhusu majukumu ya ZEC inapotokea hali kama hiyo.

Sababu nyingine vituo vingi vya kupigia kura mawakala walikuwa wa CUF/UKAWA, mawakala wa vyama vingine walinyang'anywa kadi zao za utambulisho hivyo walishindwa kushiriki mchakato wa kusimamia upigaji kura mpaka pale walipopata vitambulisho vyao.
 
Sababu nyingine vituo vingi vya kupigia kura mawakala walikuwa wa CUF/UKAWA, mawakala wa vyama vingine walinyang'anywa kadi zao za utambulisho hivyo walishindwa kushiriki mchakato wa kusimamia upigaji kura mpaka pale walipopata vitambulisho vyao.

Nani kiongozi wa serikali na nani kaaandaa uchafuzi ? Je ukawa wanapawa kuliko Ccm? Mbona bara wametangaza huku kukiwa na kasoro nyingi sana ? Na kama uchaguzi ulikuwa siyo huru why? Wasi hairishe kote ? Au Ccm ikishindwa hakukua na amani ila wakishinda ulikuwa huru na haki? Muwe positive bana ache unguvunu wenu
 
Nani kiongozi wa serikali na nani kaaandaa uchafuzi ? Je ukawa wanapawa kuliko Ccm? Mbona bara wametangaza huku kukiwa na kasoro nyingi sana ? Na kama uchaguzi ulikuwa siyo huru why? Wasi hairishe kote ? Au Ccm ikishindwa hakukua na amani ila wakishinda ulikuwa huru na haki? Muwe positive bana ache unguvunu wenu

Ndugu yangu, mimi binafsi sikuona wala kusikia kasoro kubwa iliyojitokeza kwenye uchaguzi huku Tanzania bara, kasoro niliyoiona tena haikuwa kubwa ni ile ya watu wa Mbezi kushindwa kupiga kura tarehe 25 badala yake wakapiga tarehe 26. Kasoro zilizojitokeza Zanzibar ni kubwa na hazifanani na kasoro zilizojitokeza huku bara... Tutake tusitake uchaguzi lazima urudiwe hakuna namna!
 
Tunakubaliana kuwa nchi yetu ni nchi ya kidemokrasia. Uchaguzi nia aina ya utafiti wa kujua wananchi kwa uwingi wao wanakipenda chama gani au mtu gani ili awatawale. Ni makosa kumtawala mtu bila ridhaa yake. Mtu yeyote anayefanya hila za kupindisha matakwa ya wananchi kwa uwazi au kwa kificho anafanya kosa la jinai. Ni kosa kitaaluma kupika takwimu za utafiti ili kupata matokeo tofauti na ya utafiti halisi ( research unethical). Hii haijalishi inafanywa na CCM au na CUF.
Hata hivyo kosa halihalalishi kufanywa kwa kosa lingine. Makosa ya CCM (kama yapo) hayawezi kuwa kibali kwa CUF kuvunja sheria kwa kisingizio ati CCM watafanya makosa. CCM iadhibiwe kwa makosa yake, lakini CUF isifanye makosa kwa sababu CCM inafanya makosa. Huu ndiyo msingi wa hoja yangu.
Pili mwananchi aambiwe sera na baada ya hapo aachwe atumie haki yake ya kuchagua kwa uhuru pasipo kulazimishwa.Vitendo vya CUF kuwalazimisha Wapemba waipigie CUF kwa lazima siyo vya kidemokrasia. Zipo fununu kuwa mwananchi wa Pemba akitaka kuipigia CCM anafanyiwa vituko kama: kuvamiwa na wahuni, kuzuwa kupata huduma za kijamii kama vile maji, usafiri hata kupewa talaka ili kumtisha asithubutu kuichagua CCM. Hapa hata kama CUF wanashinda lakini wananchi hawakuchagua kwa uhuru wao. Hakuna tofauti na utawalawa mabavu usiokuwa na demokrasia. Uchaguzi siyo tu kupata idadi ya kura lakini pia ziambatane na uhuru na haki.
Bantulile wewe unauwelewa wa mambo mengi ila kwenye hili Ccm wamezoeya kuiba sana na waga hawashindwi je kwa mfano malimu angekuwa anagombea kupitia Ccm je haya yote yange jitokeza?
 
Yatakuwa yale ya mwaka 2000, kuwasusia ccm uchaguzi wafanye peke yao na kura za maruhani.
 
Mbona hoja zako nyepesi sana..... kwani ni unahisi matokeo alipewa na wakala lakini hujawaza kama alikua anaweza kujumlisha matokeo yanayo tolewa na zec, niambie zec walikua hawatoi matokeo ya majimbo mbali mbali....lakin ntakusamee hukujua seif alitatangaza ushindi wakati gani...lakin swala la seif kuvunja sheria ni kutokana na zec kuchelewesha kumtangaza lakini tujiulize kwanini walichelewa au kusita kumtangaza pengine walikua wana jiandaa kuvunja sheria kitu ambacho mwenyekiti wa tume alikitekeleza au utanikumbusha labda mwenyekiti hakuvuja sheria alipo Futa matokeo ntakusaidia pengine hufahamu baada ya kupata matokeo ya majimbo ni kuyajumlisha na kutangaza mshindi kwaiyo uhalisia ulikua ni seif mshindi wa matokeo ambayo ayakutangazwa ambapo sheria inakataza chombo chochote kufuta matokeo kiti ambacho mwenyekiti hakujali (de facto) na kwakua seif alikuahana wala chombo chochote kilikua hakina namna ya kuhoji kilichotokee sion sababu ya kumlaumu seif!!!!

Anaweza yote hayo uliyoandika.

Si atuwekee bayana?

Hizi hapa kura nilizopata.

Mbona ni maneno matupu bila ushahidi?
 
Huyu foxy siza mwelewe vizuri ila kwa kuwa ni pole pole mpya siyo mbaya sana yupo kichama huku akiwa amevaaa ngozi ya utetezi wa wanyonge no shida

Utanielewa tu nisome tena:

quote_icon.png
By FaizaFoxy
Anaweza yote hayo uliyoandika.

Si atuwekee bayana?

Hizi hapa kura nilizopata.

Mbona ni maneno matupu bila ushahidi?


Hapo nnamaanisha kwanini Maalim Seif asituoneshe ushahidi wa ushindi wake?
 
Utanielewa tu nisome tena:

quote_icon.png
By FaizaFoxy
Anaweza yote hayo uliyoandika.

Si atuwekee bayana?

Hizi hapa kura nilizopata.

Mbona ni maneno matupu bila ushahidi?


Hapo nnamaanisha kwanini Maalim Seif asituoneshe ushahidi wa ushindi wake?

Foxy si alitaja na kiwango alicho pata na asilimia jaman au aweke zipi ?
 
Kutaja tu bila ushahidi?

Tume wakitangaza wanaweka na ushahidi.

Ushahidi Wa NEC mwaka huu

idadi ya wapiga kura ilikuwa watu 15,589,639

mgawanyo wa wagombea wawili ulikuwa hivi

MAGUFULI 8,882,935

LOWASSA 6,072,848

jumla kura zao 15,96,778 idadi ambayo inazidi zaidi ya kura 376,139.

Jumla Ya Kura za wagombea wawili zimezidi idadi ya wapiga kura! hapo hatujajumlisha zile kura za wagombea wengine 6 kama ACT, TLP, UDP nk.

je, huo ndio ushahidi wa tume unayotuaminisha tuiamini?
 
Ushahidi Wa NEC mwaka huu

idadi ya wapiga kura ilikuwa watu 15,589,639

mgawanyo wa wagombea wawili ulikuwa hivi

MAGUFULI 8,882,935

LOWASSA 6,072,848

jumla kura zao 15,96,778 idadi ambayo inazidi zaidi ya kura 376,139.

Jumla Ya Kura za wagombea wawili zimezidi idadi ya wapiga kura! hapo hatujajumlisha zile kura za wagombea wengine 6 kama ACT, TLP, UDP nk.

je, huo ndio ushahidi wa tume unayotuaminisha tuiamini?

Hizo porojo na uongo mtupu, weka shahada ya tume tuione.

Kama huiamini tume usipeleke wabunge wako bungeni.
 
Back
Top Bottom