Maalim Seif: Haturudii Uchaguzi

Maalim Seif: Haturudii Uchaguzi

Ni ngumu sana kudhani kwamba Uchaguzi hautarudiwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Tume hii ina wawakilishi toka CCM na CUF.

Tume ndiyo inatangaza matokeo toka majimbo lalini Tume ndiyo inafanya kazi ya kuandikisha wapiga Kura kabla ya Uchaguzi, hii ina maana gani? Tume ina idadi ya wapiga Kura wote kwa idadi ya Majimbo na vituo vya kupiga Kura.

Endapo itatokea tofauti ya wapiga Kura hasa kama idadi yao itaongezeka Tume itafuta Uchaguzi hiyo ni Haki yake.

Tume imetoa sababu 9 kwa nini imefuta Uchaguzi

1. Makamishna walivua mashati ili kutwangana makonde
9. Idadi ya wapiga Kura ilikua kubwa kuliko waliojiandikisha.

Ktk hali hiyo kinachotakiwa ni tafsiri tu ya Katiba kuhusu majukumu ya ZEC inapotokea hali kama hiyo.
Ukirudiwa ni nani atausimamia ikiwa Tume ina mapungufu iliyoyasema yenyewe?
 
Maalim Seif anazo nakala za matokeo. Je; ni utaratibu mgombea mmoja wapo kupewa nakala za matokeo? Ilikuwaje yeye akawa nazo wakati ana wawakilishi? Hii haithibitishi kuwa makamishena wa ZEC waligeuka kuwa wawakilishi wa vyama vyao. Pale idadi ya kura zinazidi wapiga kura waliojiandikisha katika daftari la wpiga kura, ZEC ifanye nini aeleze Maalim Seif. Pale kura zimefutwa futwa, inajulikana kuwa kura hizo zitakuwa zimeharibika na hapewi mgomba yeyote, je; hii ikionekana kupunguza kura zake itakuwaje
Chama au mgombea hazuiliwi kupara matokeo kutoka vituoninkwa mawakala wake, ndiyo maan upewa nakala ya fomu husika. Haya nfiyo matokeo aliyoyasema Maalimu - rejea tena statemeny yake utaelewa. Ndiyo maana ni vigumu kumshitaki pamoja na keleke wanazopiga watu za kwamba akamatwe, ajavunja sheria yoyote.
 
Time time muda haupo na sioni kama kweli kuna jitihada za kuikwamua Zanzibar ilipo kwama hiyo Tume inasubiri nini kutangaza tarehe ya uchaguzi
 
Kama CUF ina uhakika imeshinda, maana yake sera zake zinakubalika na wananchi wa Zanzibar. Huu ndiyo ukweli wa mambo. Ikiwa hivyo ndivyo, hata uchaguzi ukirudiwa mara tano CUF watashinda tu. Kuna sababu gani sasa kkataa kurdia uchaguzi? Hofu inatoka wapi?

Comredi
hakuna namna uchaguzi utarudiwa Mwenyekiti ndiye Tume kisha toa sababu 9 za kwa nini kafuta Uchaguzi. Hoja ni Je? Tume hii itasimamia uchaguzi ujao ni swala la mjadala
 
kitakacho tokea jamaa wanaweza kuvuruga fomu na vifaa vyote ili kama tume itataka kuendelea kutangaza matokeo itakosa nyaraka muhimu.
 
Kuna makada wawili STDVII na bantulile wanajitahidi kweli kutetea uamauzi wa Jescha lakini hata trained dog can establish Jecha flows...kwa hili ndugu zangu kwa sheria na kanuni Jecha amechemka, wadau wamewajibu kwa hoja thabiti kabisa.

Kilichobaki ni CCM kutumia ubabe na mabavu kurudia uchanguzi. Wote tunajua matokeo ya ubabe na dhulma. Wataiingiza Z'bar katika machafuko yasiyo ya lazima.
 
Last edited by a moderator:
Maalim Seif anazo nakala za matokeo. Je; ni utaratibu mgombea mmoja wapo kupewa nakala za matokeo? Ilikuwaje yeye akawa nazo wakati ana wawakilishi?
kuna watu wajuaji humu lakini watupu mno,eti anashanga Seif kuwa na nakala ya motokeo ya vituoni
 
Kunya anye kuku akinya bata kaharisha.

Kushinda ishinde ccm wakishinda wengine hawana haki?
 
kuna watu wajuaji humu lakini watupu mno,eti anashanga Seif kuwa na nakala ya motokeo ya vituoni

Lumumba wenye nafuu hawatii miguu hapa. Wanajua hakuna hoja ya kuisimamia zaidi ya viroja. Wapo wawili vichwa maji wanahangaika tu na kuhubiri ubabe wa CCM!
 
ccm pasuak kichwa.kwahiyo wanataka warudie ili wao wafanye mbinu washinde ?
 
Kwa taarifa zinavyojionesha uchaguzi uliofanyika ulikuwa na figisu nyingi ikiwemo mawakala wa vituo kutohudhuria kwa baadhi ya vituo na wapiga kura kuzidi idadi waliojiandikisha.

Leo wanadai eti hawawezi kurudia kupiga kura.

Hilo linaonekana kuleta vurugu Zanzibar tumekoma sisi wananchi hatutaki vurugu wafanye wao viongozi.sisi tunaendelea na kazi zetu hatuhitaji uvunjifu wa amani.
 
CCM ...huwa mnamatatizo kura za rais wa mungano halal ila rais wa zanzibar haramu..nimeamin kwel ccm ......ni ilelile......
 
kwa taarifa zinavyojionesha uchaguzi uliofanyika ulikuwa na figisu nyingi ikiwemo mawakala wa vituo kutohudhuria kwa baadhi ya vituo na wapiga kura kuzidi idadi waliojiandikisha.
leo wanadai eti hawawezi kurudia kupiga kura.
hilo linaonekana kuleta vurugu znz tumekoma sisi wananchi hatutaki vurugu wafanye wao viongozi.sisi tunaendelea na kazi zetu hatuhitaji uvunjifu wa amani
Yani sioni uhalali wa Magufuri kuwa Rais kama figisu figisu zilikuwepo aisee
Yani sioni uhalali wa Tamko la Jeche kama alikuja kugundua figisu figisu na kuzidi kwa idadi ya wapiga kura baada ya kutangaza matokeo ya Majimbo 31. kwanini basi alitangaza matokeo ya kwengine

Sioni kabisa mantiki ya CUF kurudia uchaguzi chini ya tume ambayo Mwenyekiti wake ashasema haipo huru na Makamishna walikunjana mashati sasa tukirudia si watu watachomana visu
 
Magufu akikusikia basi utajuta yaani unataka kumuharibia mlo ,

Je mtakubali uchaguzi usimamiwe na UN kuanzia A mpaka Z ,huko Zanzibar tu ! CUF wapo tayari kwa hilo !
 
kikwete kakabidhiwa nchi ikiwa salama kamwachia mwenzake ikiwa vipandevipande namwonea huruma sana magufuli anakazi kubwa sana
 
CCM ...huwa mnamatatizo kura za rais wa mungano halal ila rais wa zanzibar haramu..nimeamin kwel ccm ......ni ilelile......


Akili hawana! Hawajawahi kufikiri! Huwa wanawaza Tu!
 
Back
Top Bottom