Tumemaliza kikao cha kamati ya uteandaji ya taifa salama, updates mzipate kwenye vyombo vya habari leo kwani tulijulisha media saa 9 jioni ya leo.
Kikao cha baraza kuu la uongozi la taifa kimeitishwa, ni kikao cha dharura - kitafanyika tarehe 04 januari 2011 siku ya jumatano katika ukumbi wa mazsons zanzibar.
Ni kikao maalum cha dharura kitakachomaliza sintofahamu hizi ambazo zinaendelea ndani yama na kukuzwa sana na vyombo vya habari.
Siku zote nasisitiza hapa, CUF tuna wabunge 36, kati ya wabunge hao mmoja amehama mstari, chama kitatumia vikao kimaliza hali hiyo na chama kitabakia imara.
Kama nilivyosema awali, kamati ya utendaji ya taifa haina maamuzi juu ya HR na wenzie 13. Ni baraza kuu peke yake ndilo lina maamuzi juu yao.
Narudia tena kusisitiza kuwa hakuna mgogoro ndani ya CUF wala hakuna ugomvi - kuna watu wamehama kwenye mstari na watarudishwa mstarini kwa mujibu wa katiba.
Kinachoikuta CUF leo kinaweza kukuta chama chochote cha siasa.
Kamati ya utendaji ya taifa imemaliza kazi yake, sasa ni kazi ya baraza kuu kukaa, kujua nini kimejiri, kupewa ushahidi na kisa wahusika watasikilizwa na baraza kuu na kisha litatoa maamuzi yanayofaa kwa maslahi ya chama.
Ikumbukwe baraza kuu linaundwa na wajumbe kikanda, kuna wanaotoka kanda ya ziwa, kanda ya kati, nyanda za juu kusini, kanda ya kusini, kanda ya kaskazini, kanda mashariki, kanda ya pemba na kanda ya unguja.
Nataka kurudia tena, masuala haya ya vyama, hata kama magazeti yataandika kwa interest zao kiasi gani, hata kama wadau kadhaa watasema nini, ukweli unabakia kuwa masuala ya kisiasa huamuliwa na au kumalizwa na vikao vya chama. Na CUF itayamaliza vikaoni.