Maalim Seif, Hamad Rashid uso kwa uso leo

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Maamuzi ya kubaki ama kutimuliwa ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mbunge wa Wawi kupitia chama hicho, Hamad Rashid Mohammed, sasa yamebakia kwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye leo anaongoza kikao cha Kamati ya Utendaji kumjadili na wenzake 12.

Kikao hicho ambacho wajumbe wake ni wakurugenzi wote wa idara mbalimbali za chama hicho kitafanyika visiwani Zanzibar kwa siku mbili kabla ya kuamua ama kumtimua uanachama ama kumpa onyo kali kwa barua.

Mwenye taarifa zaidi za kikaoni atujuze.
 
Hamad Rashid namuelewa sana tu,ni mbunge wangu wa jimbo la wawi,ameshika jimbo hilo kama MP from 2000 up to now, kabla ya hapo from 1995 alikuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia jimbo la wawi.Ila nnachokielewa kule jimboni kwetu wawi hakuna la maendeleo alilolifanya miaka yote hyo 16,wamfukuze tu yule maana ameshakuwa pandikizi ndani ya kile chama.Pale wawi HR mwaka 2010,walishamkataa kumpa nafasi yakugombea,kilichomuokoa ni viongozi wa kitaifa kuwaomba wazee wa pale jimbo wampe tena nafasi,eti ni
 
Habari za hivi karibuni nilizozipata ni kwamba hiyo kamati ya utendaji imegawanyika vipande viwili. Patamu hapo.

By the way mnafahamu kwamba chini ya katiba ya CUF kamati hiyo inaongozwa na Maalim seif tu, na si mtu mwingine, na kwamba hata Lipumba haingii?
 
Hata kumfukuza chamani ni busara pia. kumbuka baadhi ya dawa ni chungu, busara ya tiba inatuelekeza kuzinywa bila kujali uchungu!!!!

Ndio tatizo la vyama vya upinzani Tanzania..wanataka wanachama utopians wanafuata bila kuuliza na kuhoji; ukijaribu wanakufukuza..ni vigumu sana kuwa na taasisi kwa mtindo huu..

Ok sisi tunawasubiri 2015 kuwaliza vizuri kwenye uchaguzi safari hii lazima tuchukue jimbo pemba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom