Maalim Seif amakinike na Zitto

-
Zito hakuwahi kuisaliti CHADEMA. Huo ulikuwa ni uzushi wa wafuasi wa Mbowe ambao hawakupendezwa na kitendo cha Zito kutaka kugombea uenyekiti wa CHADEMA
Zitto ni mtu anaefikiria, ilikuwa ngumu kukaa na Mbowe anaetaka kumfanya kila aliye chini yake msukule wa ndio mzee.

Hata Nape anaonekana kuwa yuko hivyo.
 
Dah...nimesikia Maalim ni Mzee wa Macumb Show toka kitambo sana...nimesikia tu

Sent using Beretta ARX 160
Huyoo anasepa zake
tapatalk_1553094773184.jpeg


Jr
 
Kwa hiyo kifupi Chadema watapumzika na figisu za serikali, hizo figisu zitahamia ACT hasa Zanzibar kwa Sefu.

Kwa jinsi ninavyozijua siasa zetu , naona Chadema wako tayari kushirikiana na CCM kuwahujumu ACT

Sent using Jamii Forums mobile app
not this time !kama kuna kipindi chama cha siasa kitakuwa na wakati mgumu basi ni CCM na CuF buguruni.
the rest will just move in for a kill! CHADEMA and ACT now they simply smell blood!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa upande wangu naona wafuasi wa CUF hawajamfuata Maalim, ila wao na Maalim wameamua kumkimbia Lipumba Ili abaki na Jina la Chama,
kuanzisha kingine usajili ungekua ndoto, kujiunga cchadema ccm ingekua ndio ajeenda ya kuibomoa chadema na nadhani waliamini itakua hivyo.
kwahiyo ccm hawana jinsi zaidi yakufitinisha ila Zitto mwenyewe anakwambia kapigiwa simu na viongozi wa chadema kumpongeza kwa kuwapokea wafuasi wa cuf sasa ni chadema gani wanaoumia.
maalim alianza kushirikiana nao bila kujiunga nao kiitikadi hivyo hata sasa bado watashirikiana vile vile.
kwa alichokifanya lipumba hata wasiofuatilia siasa wataanza ili kumkomoa tuu kwa roho mbaya yake.
hivyo amini kama lipumba asingetambuliwa kuwa mwenyekiti na maalim angeamua kuhama chama kama alivyofanya sasa asingekuja na wafuasi kama wote vile wengi wangebaki cuf ila kidudumtu prof na analindwa na adui, hapo lazima mumkimbie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilkuwa najiuliza haya "matarumbeta" aliyokuwa anapiga Zitto bila kukemewa wala kuitwa kuhojiwa ni ya nini, yaani mtu aliyebakia mwenye uwezo wa kukosoa serikali ya awamu hii ni huyu dogo, kumbe yalikuwa ni mazingaombwe tu, chambo ya kuinasa KAFU, ukishamuangusha Seif nani mwingine sasa maana Prof. alishananswa enzi za Dr> Mihogo
 
Nilkuwa najiuliza haya "matarumbeta" aliyokuwa anapiga Zitto bila kukemewa wala kuitwa kuhojiwa ni ya nini, yaani mtu aliyebakia mwenye uwezo wa kukosoa serikali ya awamu hii ni huyu dogo, kumbe yalikuwa ni mazingaombwe tu, chambo ya kuinasa KAFU, ukishamuangusha Seif nani mwingine sasa maana Prof. alishananswa enzi za Dr> Mihogo
Wengi hawajaliona hili

Jr
 
Afanikiwe zaidi ya ubunge ambao amakua akishinda?
Zitto Ana asili ya usaliti hawezi kufanikiwa kisiasa ataishia kuwa mpiga kelele tu

Kwa usaliti alioufanya dhidi ya chadema hakuna wa kumwamini labda ndugu zake waha

God first

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Ni kweli hujawahi kusoma,kusikia au kuoana Zitto akiitwa polisi,kupelekwa mahakamani na simu zake kushikiliwa?
Nilkuwa najiuliza haya "matarumbeta" aliyokuwa anapiga Zitto bila kukemewa wala kuitwa kuhojiwa ni ya nini, yaani mtu aliyebakia mwenye uwezo wa kukosoa serikali ya awamu hii ni huyu dogo, kumbe yalikuwa ni mazingaombwe tu, chambo ya kuinasa KAFU, ukishamuangusha Seif nani mwingine sasa maana Prof. alishananswa enzi za Dr> Mihogo

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Yaliyokwisha tokea yametokea... Yaliyokwisha jiri yamejiri.... Sasa vumbi linaelekea kutulia japo ni kama kuna chokochoko mpya inatafutwa na hapa hatafutwi mwingine bali Maalim Seif aliyekuwa katibu mkuu wa CUF.. Hatafutwi Zitto bali wafuasi waaminifu wanayemfuata Maalim Seif popote... ACT-Wazalendo ni self styled political party.... Kwenye siasa za Tanzania hakina impact kubwa zaidi ya mwenyekiti wake anayetoa matamko ya mara kwa mara....!
CUF ni mziki mwingine kabisa ni next level na kwenye siasa za Tanzania CUF ina impact kubwa sana....
Impacts za hivi vyama viwili vya siasa inaletwa na viongozi wake.. Seif ni mkongwe wa siasa za ccm na upinzani...Amewahi kuwa mpaka Waziri kiongozi, amekaa kizuizini kwa kesi ya uhaini....kesi isiyo na dhamama... Dhamira mtazamo, maono na maamuzi yake viko wazi sana... Ama dhamira moja na uamuzi mmoja... Na akiamua ameamua HATETEREKI na ndio maana anaaminika na wafuasi wake.... Amepitia kash kash nyingi za kisiasa, mafanikio na kuanguka pia.. Lakini hajawahi kuyumba wala kuyumbishwa.... Ni jasiri hata kwa hulka...

Zitto kidogo ni tofauti kabisa na Maalim... Hupenda kujijenga binafsi... Hana misimamamo thabiti na ni mwepesi kuyumbishwa ana kununuliwa... Safari yake kisiasa kwa miaka michache imekuwa na tongotongo nyingi lakini kubwa ni pale alipotaka kukihujumu chama chake kilichomlea na kuishia kufukuzwa kisha akajiundia chama kingine kilichotumika vibaya wakati wa uchaguzi mkuu 2015 huku mfaidikaji mkuu akiwa ni yeye mwenyewe
Leo hii Maalim yuko chama cha Zitto ACT, hayuko CHADEMA imekuwa faraja ya wengi kwa yeye kutokwenda huko...yangesemwa mengi... Lakini pia asingetosha kwa nafasi za chini... Pengine kuna mkakati wa baadae wa kuja kuunganisha nguvu.... ACT iliyokuwa inapumulia mashine mara ghafla umepata uhai mpya... Ujio wa Seif umekuja na Tsunami ya wanachama.... Sidhani kama likitokea na kutokea Zitto akaondoka ACT impact itakuwa kubwa kama vile Maalim kwa sababu zozote zile akaamua tena kuhama chama.....

Maalim ni mkongwe na anazijua fitina za aina zote hivyo anaweza kumdhibiti Zitto anayependa kusikika yeye tu na kuwa juu ya mamlaka yote.... Zitto hana impact kubwa kwa wanachama wake na hata serikalini lakini Maalim anayo tena ya kutisha....
Pamoja na umahiri wa uchambuzi wa mambo mbali mbali na uwezo wa kujenga hoja lakini ni mwepesi kwenye misimamo na hachelewi kugeuka akiona mambo ni magumu ama kuna faida atapata....
Hivyo basi siasa zijazo ndani ya ACT zitategemea uguswaji wa serikali, ushiriki wake na yatakayotokea kati ya Maalim na Zitto na wanachama wao


Jr
nakubaliana na wewe kabisa awe makini sana na huyo kijana
 
Back
Top Bottom