Propaganda za siasa huwa zinafanikiwa sana kwetu wafuasi.
Chadema walimbania Zitto kugombea umwenyekiti mwaka 2009, wakamfukuza Kafulila kwa kushinda Bavicha 2008 kisa kwamba Zitto kaingilia uchaguzi.
Zitto akalazimishwa kuondoa jina 2009 tena kwa ushauri wa Mtei kwa kigezo cha kumwacha Mbowe amalize term zake 2, hivyo 2014 Zitto ndiyo agombee.
Baada ya kuondoa jina, vikatengenezwa vikundi vya kumshambulia Zitto, Kubenea na Mwanahalisi wakitumika, kina Yericko, Molemo, na timu yote ambayo ni wafuasi wa Mbowe wakatumika kumshambulia kila sehemu.
Kabla hatujashtuka tukaambiwa katiba ilibadilishwa kuondoa ukomo wa Mwenyekiti, kwamba anaweza kugombea mara nyingi kadri awezavyo. Tuliomba kujua ni kikao gani cha maamuzi kilipitisha hayo hatukupata, nakumbuka Dr Slaa aliahidi kuleta minutes za kikao hicho ila hakufanya hivyo. Mpaka leo Mbowe ni mwenyekiti wa maisha.
Zitto na timu yake baada ya kuona kwamba chama hakitakaa kitoke mikononi mwa Mbowe wakaja na Waraka waabadiliko, ikaondoka nao.
Tumeona Mbowe alichofanya kwenye kumleta Lowassa na kumkaanga Dr Slaa, sisi wafuasi pendwa wa CDM tukaambiwa eti Dr ni msaliti, na si kwamba wamemsaliti wao.
Ninachelea kusema kwamba Chadema kimeshafika ukomo wake, ni zamu ya ACT kuinjoi waliyokuwa wanayainjoi CDM.
Ingawa wapinzani wote wanaendeshwa na njaa na uroho wa Madaraka, mpaka sasa hakuna ambaye ana kaliba ya Dr Slaa kwa wapinzani wote Tanzania.