Maalim Seif amakinike na Zitto

Yaliyokwisha tokea yametokea... Yaliyokwisha jiri yamejiri.... Sasa vumbi linaelekea kutulia japo ni kama kuna chokochoko mpya inatafutwa na hapa hatafutwi mwingine bali Maalim Seif aliyekuwa katibu mkuu wa CUF.. Hatafutwi Zitto bali wafuasi waaminifu wanayemfuata Maalim Seif popote... ACT-Wazalendo ni self styled political party.... Kwenye siasa za Tanzania hakina impact kubwa zaidi ya mwenyekiti wake anayetoa matamko ya mara kwa mara....!
CUF ni mziki mwingine kabisa ni next level na kwenye siasa za Tanzania CUF ina impact kubwa sana....
Impacts za hivi vyama viwili vya siasa inaletwa na viongozi wake.. Seif ni mkongwe wa siasa za ccm na upinzani...Amewahi kuwa mpaka Waziri kiongozi, amekaa kizuizini kwa kesi ya uhaini....kesi isiyo na dhamama... Dhamira mtazamo, maono na maamuzi yake viko wazi sana... Ama dhamira moja na uamuzi mmoja... Na akiamua ameamua HATETEREKI na ndio maana anaaminika na wafuasi wake.... Amepitia kash kash nyingi za kisiasa, mafanikio na kuanguka pia.. Lakini hajawahi kuyumba wala kuyumbishwa.... Ni jasiri hata kwa hulka...

Zitto kidogo ni tofauti kabisa na Maalim... Hupenda kujijenga binafsi... Hana misimamamo thabiti na ni mwepesi kuyumbishwa ana kununuliwa... Safari yake kisiasa kwa miaka michache imekuwa na tongotongo nyingi lakini kubwa ni pale alipotaka kukihujumu chama chake kilichomlea na kuishia kufukuzwa kisha akajiundia chama kingine kilichotumika vibaya wakati wa uchaguzi mkuu 2015 huku mfaidikaji mkuu akiwa ni yeye mwenyewe
Leo hii Maalim yuko chama cha Zitto ACT, hayuko CHADEMA imekuwa faraja ya wengi kwa yeye kutokwenda huko...yangesemwa mengi... Lakini pia asingetosha kwa nafasi za chini... Pengine kuna mkakati wa baadae wa kuja kuunganisha nguvu.... ACT iliyokuwa inapumulia mashine mara ghafla umepata uhai mpya... Ujio wa Seif umekuja na Tsunami ya wanachama.... Sidhani kama likitokea na kutokea Zitto akaondoka ACT impact itakuwa kubwa kama vile Maalim kwa sababu zozote zile akaamua tena kuhama chama.....

Maalim ni mkongwe na anazijua fitina za aina zote hivyo anaweza kumdhibiti Zitto anayependa kusikika yeye tu na kuwa juu ya mamlaka yote.... Zitto hana impact kubwa kwa wanachama wake na hata serikalini lakini Maalim anayo tena ya kutisha....
Pamoja na umahiri wa uchambuzi wa mambo mbali mbali na uwezo wa kujenga hoja lakini ni mwepesi kwenye misimamo na hachelewi kugeuka akiona mambo ni magumu ama kuna faida atapata....
Hivyo basi siasa zijazo ndani ya ACT zitategemea uguswaji wa serikali, ushiriki wake na yatakayotokea kati ya Maalim na Zitto na wanachama wao


Jr
"AMAKINIKE" limebeba tafakuri tosha juu ya kumfahamu na kumuekewa Zitto Kabwe wa Chadema na huyu Zitto Ruyagwa Kabwe wa ACT wazalendo.... Maalim Sefu ana jambo la kutafakari na kufanya hapa.

AMAKINIKE KWELI KWELI...maana nia ni Nzuri ila Dhati inabidi kumakinika NAYO.

Wacha Mapambano yaendelee...Nahisi rangi zote zitakwenda kujipambanua safari hii.

Wanasema Jasiri haachi Asili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa upande wangu naona wafuasi wa CUF hawajamfuata Maalim, ila wao na Maalim wameamua kumkimbia Lipumba Ili abaki na Jina la Chama,
kuanzisha kingine usajili ungekua ndoto, kujiunga cchadema ccm ingekua ndio ajeenda ya kuibomoa chadema na nadhani waliamini itakua hivyo.
kwahiyo ccm hawana jinsi zaidi yakufitinisha ila Zitto mwenyewe anakwambia kapigiwa simu na viongozi wa chadema kumpongeza kwa kuwapokea wafuasi wa cuf sasa ni chadema gani wanaoumia.
maalim alianza kushirikiana nao bila kujiunga nao kiitikadi hivyo hata sasa bado watashirikiana vile vile.
kwa alichokifanya lipumba hata wasiofuatilia siasa wataanza ili kumkomoa tuu kwa roho mbaya yake.
hivyo amini kama lipumba asingetambuliwa kuwa mwenyekiti na maalim angeamua kuhama chama kama alivyofanya sasa asingekuja na wafuasi kama wote vile wengi wangebaki cuf ila kidudumtu prof na analindwa na adui, hapo lazima mumkimbie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema vema!!!!! Tena vema mnooo. Maalim amejua kuzichanga karata vizuri. Na km angeondoka kabla ya kesi ya msingi kuisha kuna baadhi ya wanachama angewakosa. Hivyo kilichotokea hata kwa wale walokua wanamuunga mkono Lipumba,wamegeuka na kumuunga mkono Maalim.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"AMAKINIKE" limebeba tafakuri tosha juu ya kumfahamu na kumuekewa Zitto Kabwe wa Chadema na huyu Zitto Ruyagwa Kabwe wa ACT wazalendo.... Maalim Sefu ana jambo la kutafakari na kufanya hapa.

AMAKINIKE KWELI KWELI...maana nia ni Nzuri ila Dhati inabidi kumakinika NAYO.

Wacha Mapambano yaendelee...Nahisi rangi zote zitakwenda kujipambanua safari hii.

Wanasema Jasiri haachi Asili.

Sent using Jamii Forums mobile app


Jr
 
Anachaguliwa na waha kwa sababu kule mbumbumbu ni wengi, Zitto ni msaliti hawezi kufanikiwa Kwa lolote hata marafiki zake hawamwamini
Afanikiwe zaidi ya ubunge ambao amakua akishinda?

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves

God first
 
Utanirekebisha kama nitakosea. Kama umetumia tribe card ku comment nikwambie tu. Hao unao waita mamangi ni wamesha ji establish kimaisha.. so wana source nyingi sana za kuingizanpesa. Hawategemei siasa.
Ila kama hujatumia triba card basi nimekosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja ya siasa na kutafuta hela wapi na wapi?huoni ramli za mtoa hoja dhahiri ni kupinga harakati za Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wapiga ramli mmeanza

CHADEMA si ilimuita Lowasa Fisadi kwa miaka 8, kisha wakampa bendera ya kupeperusha chama chao katika uchaguzi!. Sasa Zitto ndo aliwaambia Chadema wampe nafasi mtu waliyemuita fisadi?

Halafu Maalim Seif mwenyewe keshasema , alifanya tafiti karibia vyama vyote na kuridhika na ACT kwa hiyo wewe mleta mada kaana sumu yako, Watu wameshusha Tanga wamepandisha Tanga safari inaendelea
 
sefu na zitto wote wana uchu wa madaraka
Atakachofanya sefu ni kuhama na kipande chake cha ACT kwenda kukikita zanzubar
Huko sultani zitto hatokua na sauti
 
Mshana mbona umesahau kuandika zitto ni mchumia tumbo siasa yake ni biashara hivyo haoni hatari kuwauza wenzie kwa manufaa yake, yani zitto simuamini hata chembe mtoto mnafiki sana yule
 
Mshana mbona umesahau kuandika zitto ni mchumia tumbo siasa yake ni biashara hivyo haoni hatari kuwauza wenzie kwa manufaa yake, yani zitto simuamini hata chembe mtoto mnafiki sana yule
kuna hatari kadi namba 2 ikawa ya Maembe ili watuvuruge 2020 na kamanda mwenye magongo Ubelgiji!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim ni level nyengine kabisa, kama jela kashalala, hatishiki, na Ndio maana yupo na msimamo. Love to maalim
FB_IMG_1553217555463.jpeg
FB_IMG_1553205635034.jpeg
Screenshot_20190322-040509.jpeg
IMG-20190321-WA0040.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna hatari kadi namba 2 ikawa ya Maembe ili watuvuruge 2020 na kamanda mwenye magongo Ubelgiji!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiongozi amini ipo siku, hawa wanasiasa hawatamini kitakachotokea watanzania tumechoka tuliamini wana siasa ila nao ndio hivyo wamejawa na njaa wapo kutumia kutuhadaa wapiga kura, sasa ipo siku haina jina na ajulikani mungu atamua tusaidia kwa uovu tunaofanyiwa na unyanyasaji tunaofanyiwa

South Africa ubaguzi wa ranging uliwatesa sana miaka na miaka vyama vilijitahidi muondoa mzungu vilishindwa ila mungu akatumia maandamano ya wanafunzi Soweto kama njia ya kuwakomboa wana south afrika hivyo basi hata sisi ipo siku lipo tukio halitafanywa na ACT wala CHADEMA wala CCM litafanywa na wanainchi dunia itajua na itakuja tusaidia
 
Makelele yaliyomtoa zitto chadema na makelele yaliyomtoa maalim cuf yanaweza kuwa beats sound saw a ila miziki miwil tofaut
 
I always respect your analyses and observations Mr. Mshana. But I'll hold a different opinion over this matter. It's an open truth that from the day Zitto was dismissed from CHADEMA, it was a big blow to the party, though it had never been admitted openly by CHADEMA. Again today the same party either out of jealous or poor analysis, is trying to undermine the political impact that is coming with admission of Maalim Seif Sharif Hamad by establishing joint force with Zitto within ACT. It's high time now CHADEMA should consider to work with Zitto rather than trying to tarnish his image
 
Back
Top Bottom