Maalim Seif adai waziri wa Zanzibar hana makosa, safari ya meli ilianzia Tanganyika!!

Zomba,

..ungesoma post yangu sidhani kama ungetoa majibu hayo.

..yaani ZNZ wasajili meli mitumba au mbovu halafu wategemee zitakaguliwa na bandari za mataifa mengine!!

..again, kanuni ya IMO uliyoinukuu ilimaliza kwa maneno haya hapa chini. zingatia hapo kwenye RED.

This ensures that as many ships as possible are inspected but at the same time prevents ships being delayed by unnecessary inspections. The primary responsibility for ships' standards rests with the flag State - but port State control provides a "safety net" to catch substandard ships.

Soma kanuni za IMO utanielewa. Nimeweka link huko juu, meli za mitumba hata hapa zinasajiliwa si Zanzibar tu. Meli zinazopata maafa si za mitumba tu hata TITANIC ilipata maafa safari yake ya kwanza kabisa na ilitangazwa kuwa "unsinkable".

Hapa tunaongelea procedures za IMO na Tanzania ni mwanachama, jee walifata kanuni za IMO? Mwakyembe ajibu hilo au wewe mjibie kama unaweza. Ukweli ni ukweli hata uwe mchungu vipi.

Hiyo uliyowekea nyekundu inaongelea "standard" soma vizuri, niliyokuwekea blue inaongelea safety, upo hapo ulipo, au tofauti ya maana ya "standard" na "safety" zinakupa shida tukupe darsa?
 
haya hii ndiyo zanzibar,yakiwafika shingoni eeeh watanganyika hao,si awaitaki sumatra haya,nasikia sasa wamesajili meli zaidi ya 300,zikiwemo za iran
 
Maalim Seif anampongeza huyo waziri aliyejiuzulu baada ya kusajili boti chakavu? Ingekuwa ni kwa wenzetu huyo waziri angekuwa kizimbani akieleza ilikuwaje akatoa kibali kwa meli chakavu!

Na Maalim Seif anataka watu waamini kuwa makosa ni ya Tanganyika (again?). Vipi Spice Islander iliyouwa zaidi ya watu 1000, tena chini ya waziri huyo huyo?
 
Zomba wacha ukilaza, hizo kanuni za IMO hasa kutoka SOLAS Convention lazima ziwemo katika sheria za Tanzania ili ziweze kutumiwa Tanzania, hapo unapaswa Kuangalia Merchant Shipping Act ya Tanzania bara au Maritime Transport Act ya Zanzibar na sheria nyinginezo kama za Sumatra na ZMA, usikomalie IMO kwa kupotosha watu. Hata hivyo umesema Tanzania ni member wa IMO, uko sawa kabisa. Je Zanzibar nayo ni mwanachama wa IMO?
 
Soma kanuni za IMO utanielewa. Nimeweka link huko juu, meli za mitumba hata hapa zinasajiliwa si Zanzibar tu. Meli zinazopata maafa si za mitumba tu hata TITANIC ilipata maafa safari yake ya kwanza kabisa na ilitangazwa kuwa "unsinkable".

Hapa tunaongelea procedures za IMO na Tanzania ni mwanachama, jee walifata kanuni za IMO? Mwakyembe ajibu hilo au wewe mjibie kama unaweza. Ukweli ni ukweli hata uwe mchungu vipi.

Hiyo uliyowekea nyekundu inaongelea "standard" soma vizuri, niliyokuwekea blue inaongelea safety, upo hapo ulipo, au tofauti ya maana ya "standard" na "safety" zinakupa shida tukupe darsa?
Zomba mkuu wangu unabisha tu ili mradi kubisha. Usajiri wa meli ndio unatanguliwa safety zote na kila mwaka kuna mipango ya kulinda safety kila nchi iwe gari, meli au ndege. Hata wewe na gari lako unatakiwa kulikagua kabla ya kuandoka na Traffic Polisi wanaruhusiwa kukusimamisha na kukagua kujua safety ya gari lako, lakini kitendo hicho hakihalalishi kutembea kwa gari lako isipokuwa pale uliposajili gari hilo na kupewa liseni ya kuliendesha kila mwaka.

Iwe mtumba ama sio mtumba kinachohesabiwa hapa ni sababu ya meli kuzama.. kama imetokana na Umtumba wake, au imetokana na matengenzo yasiyoruhusiwa kupewa kibali cha kubeba abiria hili ni kosa la wahusika. Na ndio maana hakuna usajili wa mara moja hadi kitu kiishe isipokuwa kila mwaka lazima upasishwe safety kabla ya chombo kupewa tena leseni ya kuendelea na kazi zake, zaidi ya hapo meli zile zilifutiwa kibali cha kusafirisha watu kutokana na sheria inayolazimishwa zifanyiwe ukarabati kwanza...

Hili ni jukumu la nchi iliposajiliwa, sema tu kunamakosa makubwa sana tunapoosema imesajiliwa Zanzibar as if Zanzibar ni nchi tofauti ama Maalim Seif kusema meli imetoka Dar ni upumbavu mwingine kwa sababu kinachotazamwa hapa ni sababu za meli hiyo kuzama na imesababishwa na makosa gani.

TATANIC iligonga mwamba na inajulikana wazi yalikuwa makosa ya nahodha! mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwezi inajulikana wazi kwamba miamba ya Ice huvunjika toka sehemu za Canada na kusogea chini ktk njia za meli kama vile wewe unapoendesha gari lako Mikumi unategema wanyama kupita. Sii kwa sababu ya kuwa meli ilikuwa kubwa sana ndio maana imekuwa hadithi kubwa isipokuwa vifo vya watu waliokufa kwa makosa ya nahodha..

Zipo meli nyingi sana zimezama na watu wamekufa lakini sii kwa uzembe mkubwa unaohudhunisha kama ule ulotungiwa hadi sinema.. Hizi meli zetu zote mbili zimezama na kuua watu kutokana na makosa ya watu na ingeweza kabisa kuepukika kama tungethamini safety za wananchi..Tunayaona ktk mabus, daladala na malorry nchini hakuna wa kulaumiwa isipokuwa vyombo vya usajili..
 
Soma kanuni za IMO utanielewa. Nimeweka link huko juu, meli za mitumba hata hapa zinasajiliwa si Zanzibar tu. Meli zinazopata maafa si za mitumba tu hata TITANIC ilipata maafa safari yake ya kwanza kabisa na ilitangazwa kuwa "unsinkable".

Hapa tunaongelea procedures za IMO na Tanzania ni mwanachama, jee walifata kanuni za IMO? Mwakyembe ajibu hilo au wewe mjibie kama unaweza. Ukweli ni ukweli hata uwe mchungu vipi.

Hiyo uliyowekea nyekundu inaongelea "standard" soma vizuri, niliyokuwekea blue inaongelea safety, upo hapo ulipo, au tofauti ya maana ya "standard" na "safety" zinakupa shida tukupe darsa?

Zomba,

..Standards na Safety go hand-in-hand.

..hata mimi nimewanukuu IMO ambao wewe pia umewanukuu.

..ulichokosea wewe ni kuweka nusu ya nukuu toka IMO. sasa mimi nimeongezea kile kipengele ulichokuwa umekificha ambacho kinaitia mamlaka ya ZNZ kitanzi.

..imeelekezwa kabisa kwamba PRIMARY RESPONSIBILITY iko upande wa yule aliyesajili meli.

..meli hiyo ilikuwa inapigwa mnada kwenye EBAY na haikupata manunuzi. sasa hao waZNZ kwa tamaa zao wakainunua, na SMZ kwa uzembe wao wakaisajili, na matokeo yake ndiyo hivyo tena MAAFA.

..meli 2 zimezama ndani ya mwaka mmoja, badala ya kuangalia wapi mnakosea mko busy kulaumu wa-Tanganyika.
 
Zomba mkuu wangu unabisha tu ili mradi kubisha. Usajiri wa meli ndio unatangulia safety zote na kila mwaka kuna mipango ya kulinda safety kila nchi iwe gari, meli au ndege. Hata wewe na gari lako unatakiwa kulikagua kabla ya kuandoka na Traffic Polisi wanaruhusiwa kukusimamisha na kukagua kujua safety ya gari lako, lakini kitendo hicho hakihalalishi kutembea kwa gari lako isipokuwa pale uliposajiri gari hilo..

Iwe mtumba ama sio mtumba kinachohesabuwiwa hapa ni sababu ya meli kuzama.. kama imetokana na UUmtumba wake, au imetokana na matengenzo yasiyoruhusdsiwa kupewa kibali cha kubeba abiria hili ni kosa la wahusika..Na ndio maana hakuna usajili wa mara moja hadi kitu kiishe isipokuwa kila mwaka lazima upasishwe safety kabla ya chombo kupewa tena leseni ya kuendelea na kazi zake..

Hili ni jukumu la nchi iliposajiliwa, sema tu kunamakosa makubwa sana tunapoosema imesajiliwa Zanzibar as if Zanzibar ni nchi tofauti ama Maalim Seif kusema meli imetoka Dar ni upumbavu mwingine kwa sababu kinachotazamwa hapa ni sababu za meli hiyo kuzama na imesababishwa na makosa gani.

TATANIC iligonga mwamba na inajulikana wazi yalikuwa makosa ya nahodha! mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwezi inajulikana wazi kwamba miamba ya Ice huvunjika toka sehemu za vanada na kusogea chini ktk njia za meli kama vile wewe unapoendesha gari lako Mikumi unategema wanyama kupita..Hizi meli zote mbili zimezama na kuua wa tu kutokana na makosa ya watu na ingeweza kabisa kuepukika..

Kusajili kunafata kitu kinaiwa "standard procedures" na usalama kuna kitu kinaitwa "safety procedures:. msivichanganye hivyo, ni vitu viwili tofauti.

Mfano: Ikiwa meli imesajiliwa Zanzibar na ilipofika Tanzania waliona ina makosa na inaweza kuleta hatari wana haki ya "kuipandisha", hii term ya "kuipandisha" mabaharia wanajuwa maana yake. Wacha meli kupandisha kwa safety standards, meli inapandishwa port yoyote mwanachama wa IMO duniani hata kwa kuwalipa mabaharia kinyume cha sheria.

Unaweza kusajili meli kwa kufata standard zote za IMO na ikapita salama lakini inapofika bandari ya mwisho inaweza kuzuiliwa kupakia zaidi ya standard iliyopasishiwa (meli zote zinatakiwa ziwasilishe documents za usajili zinapoingia bandarini ili ziweze kufanyiwa uhakiki na kuelewa standard yake ni ipi) na ni lazima zifanyiwe inspection ya "IMO safety procedures" kuwa ipo salama au haipo salama na hilo ni jukumu la bandari ya mwisho iliyotoka meli na si iliko sajiliwa. Umeelewa?

Nawaombeni msome hili, msichukulie ushabiki tu. Maalim Seif hapa yuko sahihi. Link hii hapa: IMO | Port State Control
 
Musajili kunafata kitu kinaiwa "standard procedures" na usalama kuna kitu kinaitwa "safety procedures:. msivichanganye hivyo, ni vitu viwili tofauti.

Mfano: Ikiwa meli imesajiliwa Zanzibar na ilipofika Tanzania waliona ina makosa na inaweza kuleta hatari wana haki ya "kuipandisha", hii term ya "kuipandisha" mabaharia wanajuwa maana yake. Wacha meli kupandisha kwa safety standards, meli inapandishwa port yoyote mwanachama wa IMO duniani hata kwa kuwalipa mabaharia kinyume cha sheria.

Unaweza kusajili meli kwa kufata standard zote za IMO na ikapita salama lakini inapofika bandari ya mwisho inaweza kuzuiliwa kupakia zaidi ya standard iliyopasishiwa na kuwa haipo salama na hilo ni jukumu la bandari ya mwisho iliyotoka meli na si iliko sajiliwa. Umeelewa?

Nawaombeni msome hili, msichukulie ushabiki tu. Maalim Seif hapa yuko sahihi. Link hii hapa: IMO | Port State Control
Zomba huwezi kusajili meli kama haikupita ktk safety Procedures. Unapitia safety kwanza kabla ya kusajili na hata Insurance inatakiwa kabla ya usajili wa meli, sasa kama Zanzibar wanafanya tofauti haya ndio makosa tunayozungumzia na inatakiwa kila baada ya muda kuhakikisha hivi vitu vipo sawa..

Labda niseme hivi huwezi kufunga ndoa kama hukupeleka posa kwanza. Posa na Ndoa ni vitu viwili tofauti lakini cha pili kinategemea cha kwanza.. Huwezi kusajili gari, ndege wala meli kama haikupitia safety kwanza.. katika karatasi utakazo walikisha ili Meli isajiliwe SAFETY ni mojawapo na muhimu zaidi na unafanya renewal kila mwaka..
 
Zomba huwezi kusajili meli kama haikupita ktk safety Procedures. Unapitia safety kwanza kabla ya kusajili na hata Insurance inatakiwa kabla ya usajili wa meli, sasa kama Zanzibar wanafanya tofauti haya ndio makosa tunayozungumzia na inatakiwa kila baada ya muda kuhakikisha hivi vitu vipi sawa..

Labda niseme hivi huwezi kufunga ndoa kama hukupeleka posa kwanza. Posa na Ndoa ni vitu viwili tofauti lakini cha pili kinategemea cha kwanza.. Huwezi kusajili gari, ndege wala meli kama haikupitia safety kwanza.. katika karatasi utakazo walikisha ili Meli isajiliwe SAFETY ni mojawapo na muhimu zaidi na unafanya renewal kila mwaka..

Mkandara,

..unajua SMZ na Baraza la Wawakilishi waliamua kuizuia Sumatra isifanye kazi ZNZ ili waweze kusajili mimeli mibovu.

..matokeo yake ndiyo haya. Within 1 yr meli mbili zimezama na kusababisha upotevu wa maisha na mali.

..halafu bila aibu Maalim Seif analeta siasa na kujaribu kututupia lawama wa-Tanganyika.
 
Kuhusu Maalim Seif kusema kweli anawatumia sana Wazanzibar na kuwajaza ujinga. naona muda wake unakaribia kwisha hivyo anaanza na gear mpya..Lakini tukirudi nyuma swala la SAFETY nchini halina SUMATRA wala nani yaani wote hawaifanyi kazi inavyotakiwa, ajali zimekithiri kote bara na visiwani. - Again, kwa maskini wenye njaa utaweza vipi kuharamisha Nguruwe ikiwa ndio nyama rahisi kuliko zote..
 
Zomba huwezi kusajili meli kama haikupita ktk safety Procedures. Unapitia safety kwanza kabla ya kusajili na hata Insurance inatakiwa kabla ya usajili wa meli, sasa kama Zanzibar wanafanya tofauti haya ndio makosa tunayozungumzia na inatakiwa kila baada ya muda kuhakikisha hivi vitu vipo sawa..

Labda niseme hivi huwezi kufunga ndoa kama hukupeleka posa kwanza. Posa na Ndoa ni vitu viwili tofauti lakini cha pili kinategemea cha kwanza.. Huwezi kusajili gari, ndege wala meli kama haikupitia safety kwanza.. katika karatasi utakazo walikisha ili Meli isajiliwe SAFETY ni mojawapo na muhimu zaidi na unafanya renewal kila mwaka..

Hilo unalosema ni sawa kabisa.

Umesha sajili, ukapata "green light" ya safety zote umemaliza. Umeondoka umeenda Dar. Ukapakia zaidi ya "standard" yalo uliyopatia usajili. yaani umeruhusiwa kupakia abiria 200, wewe Dar ukapakia 300, umeruhusiwa tani 100 za mzigo, Dar ukapakia tani 150. Hapo ndipo zinapoingia kanuni za "port state control".

Sijui umeelewa au bado.

Mfano: Basi lako limesajiliwa Kenya na limeruhusiwa kupakia abiria 65, ulipoingia Tanzania ukapakia abiria 80, Traffic wa Tanzania anatakiwa asiliruhusu kutembea au aliwachie? likipata ajali utamlaumu Mkenya aliyelisajili? Fikiri. Au liliposajiliwa taa zilifanyiwa inspection zinawaka, kufika Tanzania, askari kalipiga mkono, dereva kuambiwa washa taa, haziwaki, hapo ni lazima uwajibike na ule usajili wako wa Kenya hauingilii hilo.

Ndio maana kuna makubaliano ya Kimataifa kuhusu hizi kanuni na ndio hizo nilizoweka za Interbational Maritime Organization.

Meli inaweza kuwa ya miaka 50 nyuma lakini ikawa na safety standards zote za usajili na zikawa ni sawa kabisa, lakini kuna hitilafu zinatokea ikiwa njiani, na kuna uvunjaji wa shria kama kujaza sana, kupakia abiri wengi zaidi, hizo zote zinahusika na bandari ya mwisho. Au la hali ya hewa na kuruhusiwa kuondoka, kwani unaweza ukawa bandarini hali ya hewa ni nzuri tu lakini kilomita 20 tu nje ya mji hali ya hewa ni mbaya na kituo cha hali ya hewa kinatakiwa kikujulisha kabla na ni jukumu la bandari uliyotoka na si ulikosajili.

Kama hata haya huwezi elewa endeleza tu nami sitochoka kukupa darsa.

Hili halina unazi liko wazi kabisa. Inabidi Serikali yetu ilaumiwe na wahusika wawajibike ingawa ni ya chama nnachokipenda.
 
Kuhusu Maalim Seif kusema kweli anawatumia sana Wazanzibar na kuwajaza ujinga. naona muda wake unakaribia kwisha hivyo anaanza na gear mpya..Lakini tukirudi nyuma swala la SAFETY nchini halina SUMATRA wala nani yaani wote hawaifanyi kazi inavyotakiwa, ajali zimekithiri kote bara na visiwani. - Again, kwa maskini wenye njaa utaweza vipi kuharamisha Nguruwe ikiwa ndio nyama rahisi kuliko zote..

Hapo unavuka mipaka na unaingilia kazi si yako, kama vile aliyeharamisha ni binaadam. Tuwe makini katika haya mambo. Mifano mingine ni kufru. Hakuna kigezo kinachoonesha kuwa Nguruwe aliharamishwa kwa ughali wake.
 
Mkandara,

..unajua SMZ na Baraza la Wawakilishi waliamua kuizuia Sumatra isifanye kazi ZNZ ili waweze kusajili mimeli mibovu.

..matokeo yake ndiyo haya. Within 1 yr meli mbili zimezama na kusababisha upotevu wa maisha na mali.

..halafu bila aibu Maalim Seif analeta siasa na kujaribu kututupia lawama wa-Tanganyika.

Tatizo sio usajili, tatizo ni kanuni zilikiukwa kutoka bandari ya mwisho. Tuwe wakweli. Hata kama mna chuki na Zanzibar au Maalim Sef hili hapa hamna hoja.

Nini kiliwazuia bandari ya Dar Es Salaam kuizuwia hiyo meli isiondoke kama ilikuwa haina viwango vya usalama vya kusafiri? hata kama imesajiliwa Amsterdam. Wakati sheria zinawataka waikaguwe na wahakikishe usalama wake, tena hizi za abiria ndio kabisa.

Kuna ndege yetu Tanzania iliruka hapa imeruhusiwa, kufika Ufaransa ikasimamishwa, hakuna kuruka mpaka ifikie viwango vya usalama vya kuruka au hilo hamjui? ilisajiliwa wapi ile?

Tena wale wenye meli wakiwa na mawakili wazuri na ikionekna bandari ya Dar ilikiuka kanuni, inabidi walipe gharama zote pamoja na fidia za waliofiwa. Amini usiamini. Utaruhusu vipi meli iondoke ikiwa na abiria zaidi ya uwezo wake? au shehena zaidi ya uzito ulioruhusiwa. Uzembe ulifanyika Dar na kama hatua hazijachukuliwa utaendelea kufanyika na hii haitokuwa mara ya kwanza wala ya mwisho.

Na IMO wakiingilia kati na wakikuta kanuni zimekiukwa, wanaweza kuwatia adabu Tanzania kwa kuwazuia meli wanachama kutumia bandari mpaka wahakikishe kuwa kanuni zote ziwe zinafatwa na waliofanya uzembe kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hapa ndio wale wapayukaji wanaojifanya wanaharakati wa haki za binaadam walitakiwa wapakazanie na sio kwa yule muuwaji wa wagonjwa.
 
Jokakuu,
Huyu maalim Seif unajua wakait mwingine ana Ujinga wa kuzaliwa. hata ndege zinapokaribia anga za tanzania ni jukumu la tanzania kuiongoza ndege sio Jukumu la kule ilipotoka. kama hali ya hewa zanzibar vilikuwa mbaya taarifa inatolewa na zanzibar kwamba meli haziruhusiwi kutia nanga hivyo aidha safari zinaahirishwa ama zina pewa njia mpya..

Meli ilionodka dar salama na hali hakikuwa mbaya zaidi ya upepo ambao usingewez akuizuia kuondoka na ndio maana iliondoka na salama. Tatizo lilikuwa Zanzibar kwenyewe ilipozamia na ndio siku zote ajali hutazamwa ilipotokea.. Hivyo kama sababu ilikuwa muundo mbaya wa meli ambayo kwanza navyosikia ilikuwa Pantoni ikabadilishwa na kufanyiwa marekebisho iwe meli ya abiria. Hii pekee ilitakiwa kufanyiw auchunguzi mkubwa sana kina nani walihusika , kutazama kwa makini hilo Pantoni liliweza vipi kubadilishwa na kuweza kufanya safari ndefu za kwenda na kurudi kati ya Zanzibar na Dar..

JokaKuu, Mkandara

Wakati Seif anataka kumsafisha Waziri aliyejiuzulu na kutoa visingizio hivi na vile, na sisi hatupaswi kulichukulia hili la ajali kwa ushabiki huu mnaouanzisha hapa.

Meli au boti lilikuwa bovu/ halikidhi kiwango? Hilo ni kosa la kwanza, kusajiliwa na kupewa kibali cha kubeba abiria.Hilo ok, ni tatizo la Znz na mamlaka za Zanzibar.

Seif anasema safari ya boti ilianzia Dar. Hapo hapana ubishi. Swali je Tanganyika/ mamlaka za Tanganyika kwa nini hawakuizuia kufanya safari zake katika bandari za Tanganyika kama walishajua kuwa boti hii ilikuwa ni bomu linalosubiri kuchukua roho za wananchi wetu?

Pili, Imeripotiwa kuwa Boti hili lilibeba abiria kupita uwezo wake. Hapo vipi watumishi/ maafisa wa Bandari Dar tunawasafisha kwa uzembe wa kuruhusu chombo kusafiri kikiwa kimebeba abiria na mizigo kupita kiwango kinachoruhusiwa/ uwezo wake?

Waliokufa ni watanganyika,wazenj na wageni..sasa huku kutupiana lawama au kusafishana kiushabiki hakusaidii.

Uzembe umefanyika Dar na Znz.

Mkandara una point unaposema boti lilipasa kuongozwa na mamlaka za Znz kikiwa kimeingia katika mkondo wa Znz lakini tusisahau kuwa hili boti lilisheheni abiria kupita uwezo wake. Je hakuna utataratibu wa kudhibiti idadi ya abiria wanaosafiri na vyombo vya baharini?Kama udhibiti unafanyika basi hili lingefanyika Dar au vipi?

Watanzania tunakufa na kuuliwa kwa uzembe halafu tunajadili kusafishana. Sisi watu wa ajabu kweli.Waliofanya uzembe wanapaswa kuchukuliwa hatua/ kuwajibika au kuwajibishwa na sio kuingiza siasa. Ni wazi kuwa wapo waliofanya uzembe, Zanzibar na pia Dar.

Angalia video hapa usikie uzembe ambao tunauruhusu,hata abiria pia wanakubali kuharakishiwa kifo halafu tunabaki kulalama tu.
https://www.jamiiforums.com/jamii-p...o-hapo-78-wajeruhiwa-kwenye-ajali-tabora.html

na hii https://www.jamiiforums.com/great-t...-raia-wao-tujifunze-nini-kenya-na-rwanda.html
 
Mkuu JokaKuu,
Kama alivyonenena Mkandara, huyu Maalimu Seif ni mtu wa ajabu na sichelei kusema ana madai na siasa za kipuuzi sana.
Anajaribu Ku-insinuate kuwa tatizo la meli limetokana na Muungano, na kwamba kwasababu Zbar inaonewa ndiyo maana Tanganyika hakuna aliyejiuzulu. Angalia huu kama si upuuzi ni nini.

1. ZNZ iliunda ZMO ili kuweza kumiliki usalama wa vyombo vyao. Meli iliyozama ilikuwa ni pantoni Marekani. ZMO wakakubali ilipofanyiwa matengenezo ili iwe meli hata kama matengenezo hayo yamefanywa na Daktari wa meno.
Usalama wa kwanza ni jukumu la SMZ na ZMO.

2. Maalimu anampongeza waziri, kwani wakati meli ya spice ilipozama nani alikuwa waziri na nani aliwajibika? Tena meli ilitoka Unguja kwenda Pemba, nani aliwajibika

3. Wakati wa mauaji ya 2001 ambayo chanzo chake ni uchochezi wa Maalimu Seif, mbona yeye hakuwajibika ili kujenga heshima ya kisiasa? Mauaji yametokea si mara moja lini Maalimu amefikiria kuwajibika zaidi ya kutaka urasi.

4. Mkandara anasema hivi, jukumu la hali ya hewa si la bandari ya Dar es Salaam kwasababu wakati meli inaondoka hali iliruhusu, ni jukumu la ZNZ kujua hali iliruhusu meli kutia nanga katika gati? Ndege ikitoka Oman ikaingia anga la Tanzania mwenye control na ndege ile ni Tanzania si Oman.

Zomba, Ethiopia airline ilipootekwa Tanzania ilichukua jukumu la kuiongoza kwenda ilikotarajiwa. Baada ya muda fulani rubani alipata mawasiliano na Comoro akamuomba controller Dar amuachie aendelee na wa Comoro. Taarifa zote za kuanguka kwa ndege zinapatikana Comoro hadi kilichosikika katika black box kwa mara ya mwisho.

Haya ni matatizo yenu ya kufanya vitu substandard. Msiwasingizie Sumatra, kama wanachunguza wanasaidia tu lakini uzembe wote unatokana na watu wenye akili kama Maalimu. Yeye haoni tatizo la kusajili meli tena pantoni anaona tatizo ni Muungano. Kwanini Maalimu Seif amewafanya ndondocha kiasi hiki?
 
Naona chuki yako dhidi ya Maalim Seif umeivalia njuga...Muungano tanaukataa sisi wznz kwa madhila munayotufanyia. Maalim Seif ,akiwepo asiwepo harakati zitaendelea. Angalia post #36 ya mtu mwenye busara. Ushabiki ukizidi busara inapungua. LET ZNZ GO! Ha ha hah...
 
Kwa hiyo mnataka kusema tatizo lilikuwa hali ya hewa tu wala hakukuwa na matatizo mengine kama kujaza watu zaidi ya uwezo na shehena ya mizigo kuzidi viwango?

Kwa sababu kama kuna dosari kati ya hayo mawili Mamlaka ya Bandari Dar Es Salaam inahusika

Pia Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitakiwa kutoa maelezo ya kina kuwa hali ya hewa hadi mwisho wa maji ya Tanganyika ni salama ila huko kwa Zanzibar hatujui.
 
Back
Top Bottom