Maalim Seif adai waziri wa Zanzibar hana makosa, safari ya meli ilianzia Tanganyika!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif adai waziri wa Zanzibar hana makosa, safari ya meli ilianzia Tanganyika!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Aug 14, 2012.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  ..someni hapo kwenye RED.

  ..meli hiyo ni mali ya waZNZ.

  ..imesajiliwa na serikali ya waZNZ.

  ..kwanini Maalim Seif atubebeshe mzigo wa lawama kwa kuzama kwa meli hiyo??!!

  ..anadai waziri wa Zanzibar hapaswi kubeba lawama kwasababu safari ya meli haikuanzia ZNZ[read ilianzia Tanganyika].

   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jokakuu,
  Huyu maalim Seif unajua wakait mwingine ana Ujinga wa kuzaliwa. hata ndege zinapokaribia anga za tanzania ni jukumu la tanzania kuiongoza ndege sio Jukumu la kule ilipotoka. kama hali ya hewa zanzibar vilikuwa mbaya taarifa inatolewa na zanzibar kwamba meli haziruhusiwi kutia nanga hivyo aidha safari zinaahirishwa ama zina pewa njia mpya..

  Meli ilionodka dar salama na hali hakikuwa mbaya zaidi ya upepo ambao usingewez akuizuia kuondoka na ndio maana iliondoka na salama. Tatizo lilikuwa Zanzibar kwenyewe ilipozamia na ndio siku zote ajali hutazamwa ilipotokea.. Hivyo kama sababu ilikuwa muundo mbaya wa meli ambayo kwanza navyosikia ilikuwa Pantoni ikabadilishwa na kufanyiwa marekebisho iwe meli ya abiria. Hii pekee ilitakiwa kufanyiw auchunguzi mkubwa sana kina nani walihusika , kutazama kwa makini hilo Pantoni liliweza vipi kubadilishwa na kuweza kufanya safari ndefu za kwenda na kurudi kati ya Zanzibar na Dar..
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  Anajikosha tu hana lolote
   
 4. mito

  mito JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,653
  Likes Received: 2,039
  Trophy Points: 280
  Jamani yule waziri alijiuzuru kwa sababu ya wizara yake kuruhusu meli isiyo na viwango ku-operate na wala si kwa sababu ya ajali hiyo. Mbona wakati wa ajali ya Mv Spice hakujiuzuru?

  Maalim anataka tu kumsafisha, kwanza hakuwepo, alikuwa amelazwa, wanasiasa bwana!
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  poor him!
   
 6. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  afadhali wazanzibar wamempata kiongozi wa ngazi ya juu wa kuwavunjia muungano.!
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sheria za usalama wa meli duniani zina ainisha kuwa lawama huenda kwenye bandari iliyotoka meli mara ya mwisho ikitokea hitilafu ya usalama wa hiyo meli. Siyo ilipoandikishwa.

  Dunia nzima, hilo linajulikana, meli inaweza kuwa ni ya nchi fulani lakini toka iondoke bandari iliyosajiliwa inaweza kupita mwaka isirudi iwe kazini, na kila bandari duniani inabeba jukumu la kuikaguwa na kuhakikisha usalama ikiwa bandarini kwake.

  Ni kama ndege, kama haikidhi usalama wa kuruka au wakaguzi wanaona italeta madhara basi hawairuhusu kuondoka mpaka amma itengenezwe itengemae au hali ya hewa iruhusu au isimamishwe na kuwa scrap bila kuihusisha nchi iliyosajiliwa.

  Mzigo wa hii meli, tukitaka tusitake unadondokea bandari ilipoanza safari yake ya mwisho. Iwe ni kwa ubovu wa hiyo meli au hali ya hewa ilikuwaje wakati inaruhusiwa kuondoka.

  Hawezi kutoka inspector Zanzibar kukaguwa kila meli iliyosajiliwa Zanzibar kila inapokuwa bandari za nje.

  Port State Control (PSC) is the inspection of foreign ships in national ports to verify that the condition of the ship and its equipment comply with the requirements of international regulations and that the ship is manned and operated in compliance with these rules.
  [​IMG]
  Many of IMO's most important technical conventions contain provisions for ships to be inspected when they visit foreign ports to ensure that they meet IMO requirements.
  These inspections were originally intended to be a back up to flag State implementation, but experience has shown that they can be extremely effective, especially if organized on a regional basis. A ship going to a port in one country will normally visit other countries in the region before embarking on its return voyage and it is to everybody's advantage if inspections can be closely co-ordinated.

  Soma zaidi: IMO | Port State Control
   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,743
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Hapa mwenye makosa ni msajili wa meli ambaye alisajili meli mbovu isiyokidhi viwango vya usalama kubeba abiria. Kuongelea masuala ya wapi kiliondokea kuelekea Zanzibar ni upuuzi ambao ni mwanasiasa asiye makini pekee anaweza kuusema.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Soma hizo kanuni za International Maritime Organization kabla hujakurupuka: IMO | Port State Control
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,743
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio unakurupuka. Na kwa kuonyesha jinsi ulivyo mkurupukaji ume "copy" na ku "paste" link ambayo inaongelea port state control. Kwa taarifa yako hiki ulicho bandika hapa kinaongelea ukaguzi wa meli za kigeni zinazotia nanga bandari za ndani ya nchi. Labda kama unasema Zanzibar ni nchi ya kigeni kwa Tanganyika.

  Hakuna nchi duniani yenye registry mbili isipokuwa ni Tanzania tu. Na bahati mbaya zaidi hiyo ya pili ya hiki kinachoitwa na wanasiasa kuwa ni "nchi" ya Zanzibar haipo unguja wala pemba na wala hawana control nayo kwa sababu wametoa hiyo kazi kwa mkandarasi aliye Dubai. Huu ndio ninaouita upuuzi wa wanasiasa.
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Baada ya Seif kugeuzwa nyumba ndogo ya CCM ameishiwa kila kitu. Alichobaki nacho ni mshipa kukosa aibu wa kujikomba kwa kila kitu ili aweze kupata marupurupu. Amepewa nafasi isiyo na kazi zaidi ya kuwa kama fanicha nyumbani. Angalia balozi Idd Seif anayeitwa makamu wa pili anavyofanya kila kitu huku Seif akiachwa uani. Kweli walijua kumtenda. Amegeuka kituko karibu katika kila kitu. Kweli mshahara wa usaliti aibu.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  Zomba,

  ..it will be interesting kusikia wahusika toka bandari za ZNZ na Dsm wana maelezo gani.

  ..lakini ukumbuke kwamba mamlaka ya ZNZ ndiyo iliyosajili meli 2 ambazo zimepata ajali mwaka huu.

  ..mwisho, kuna maelezo ya ziada hapa ambayo yanaelekeza kwamba "primary responsibility" iko upande wa ZNZ.

  This ensures that as many ships as possible are inspected but at the same time prevents ships being delayed by unnecessary inspections. The primary responsibility for ships' standards rests with the flag State - but port State control provides a "safety net" to catch substandard ships.
   
 13. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sultani anaropoka tu....haya sultani.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hata isajiliwe New York. Dhamana ni bandari iliyotoka, soma kanuni za IMO, nimeweka link juu huko, tusiongee ushabiki. Kwenye kosa tubainishe ili tusiendelee kuwa na makosa. Ukificha maradhi kifo kitakuumbuwa.

  Na ile iliyozama Lake Victoria ikauwa mamia kama si maelfu ilisajiliwa Zanzibar?
   
 15. h

  hans79 JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Iwe bara au visiwani wote ni wazembe walohusika na usajili pamoja na wanaosimamia suala nzima,kuanzia Mr Dhaifu na nyinyiemu wote pamoja nawe.Lakini hatushangai ndo utawala wenu wa kuua.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mlitaka Kikwete aende bandarni akasimame akaguwe kila jahazi na meli na Mwakyembe afanye kazi gani? Na waziri wenu kivuli anaepaswa kusimamia haya madudu alikuwa wapi? anachangisha M4C halafu zikajenge mbezi kwa nanihii?
   
 17. m

  markj JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  aaah! malizia mkuu, mbezi kwa josephin au? kuchimba kisima cha ges kilwa! usiogopee za kawaida tu hizo
   
 18. M

  Msajili Senior Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Zomba
  hizo provisions za IMO ulizocopy na kupaste zinahusiana sana na ocean going vessel, si kwa usafiri wa ndani. Usikurupuke soma kwanza.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  Zomba,

  ..ungesoma post yangu sidhani kama ungetoa majibu hayo.

  ..yaani ZNZ wasajili meli mitumba au mbovu halafu wategemee zitakaguliwa na bandari za mataifa mengine!!

  ..again, kanuni ya IMO uliyoinukuu ilimaliza kwa maneno haya hapa chini. zingatia hapo kwenye RED.


  This ensures that as many ships as possible are inspected but at the same time prevents ships being delayed by unnecessary inspections. The primary responsibility for ships' standards rests with the flag State - but port State control provides a "safety net" to catch substandard ships.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Utajaza mwenyewe, niogope kwani mie Ulimboka!
   
Loading...