Uchaguzi 2020 Maajabu ya viongozi waandamizi wa CCM

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Ni jambo la kushangaza sana kuona hadi msemaji wa Ikulu kwenye ukurasa wake wa Instagram na Twitter akipost wasanii watakaokuwepo kwenye kampeni za Magufuli.

Inastaabisha sana kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuwatangaza wasanii badala ya mgombea urais.

Hawa jamaa ni kama wamejitoa mshipa wa aibu, inawezekanaje watu wenye nyadhifa kubwa kama hizi Serikalini kutumia nguvu kubwa kunadi wasanii badala ya mgombea mwenyewe?

Haihitaji kuwa na IQ kubwa kung'amua lengo la kujitoa ufahamu kwa hawa viongozi.

Wanatambua bila wasanii mikutano ya mgombea wao haiwezi kuwa na mahudhurio yanayoridhisha, hivyo lengo lao ni kuihadaa dunia ione kuwa mgombea wa ccm anapendwa ili kuja kuhalalisha malengo yao ovu kwenye kupora ushindi.

Haiingii akilini page zote za mitandao ya kijamii za hawa viongozi waandamizi serikalini wanatangaza uwepo wa wasanii badala ya mgombea husika.

Of course madhara ya kuanguka kwa CCM ni makubwa kwao ukilinganisha na madhara ya kujitoa ufahamu. CHADEMA wanatakiwa sasa waelekeze nguvu kubwa kwenye kulinda kura zao maana ukiona watu na heshima zao wameamua kujitoa ufahamu ujue kuna sehemu watakuja kujilipa na kunufaika.
 
Shida na hali ngumu ya maisha zitatatuliwa na hao waigizaji.
 
Mwalimu Jk Nyerere alisema.

"Udikteta ni selikali ya watu wachache ama kikundi cha watu kinachotunga sheria kandamizi atakayebisha atakipata cha moto".

Dikteta jiwe
 
JPM kama mgombea Urais keshapita tyr, kilichobaki ni kukamilisha ratiba tu kwa kufanya tuvitu tudogotudogo kama burudani na mambo mengine ili kukidhi haja ya ratiba ya tume.
 
Lissu alisema akipata urais huyo msemaji wa serikali(boss wa MAELEZO) ajiandae kutafuta kazi nyingine maana wapo kwa ajili tu ya kuvibana vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom