Gordian Anduru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2021
- 334
- 657
August 10, 2019 Simba alitoka sare ya bila bila ugenini na UD Songo ya Msumbiji na Yanga walitoka sare ya 1-1 na Township Rollers ya Botswana. Kama kawaida yao wachambuzi maandazi waliishambulia sana Yanga kwa kuruhusu bao nyumbani na kuisifu sana Simba kutoka sare tasa ugenini.
Tulinyanyasika wiki nzima lakini mwisho wa wiki tarehe 24 Jumamosi yake Yanga akashinda moja bila ugenini na kufuzu hatua inayofuata halafu watu wa Simba wakacheka sana, wakasema subirini wanaume kesho.
Looh, ilipofika hiyo Jumapili wakatoka sare ya moja moja na kuaga mashindano kwa kucheza mechi mbili tu. Haisemwi semwi na nadhani ni makusudi lakini msimu huo 2019/20 Simba ilicheza mechi mbili ikatolewa, Yanga ikacheza mechi sita. Naona wiki hii imejirudia, walienda raundi ya pili wakacheza na Zesco na Pyramid kwenye play off ya shirikisho.