Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

UNAJITOA FAHAMU EEH?

Ukikamatwa kwa wizi, na baadaye ikagundulika ulishirikiana na mlinzi, hilo linaondoa makosa yako? Hebu irejee kesi ya Babu Seya, halafu ulinganishe na madudu yako, ndio utajua kuwa kuwa Malisa kapiga ikulu na wewe sio wa capacity ya kujibu hoja.
Below standard!
 
Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.

Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.

Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."

Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"

Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.

That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.

Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.

Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.

That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.

Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!

Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.

Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.

Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.

Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?

Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.

JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.

Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.

Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?

Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.

Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!

Malisa GJ
hiki ni kizungumkuti kama sio kizunguzungu. mimi namsubiri tuone kama atakapounda bodi mpya hatawajumuisha hao wajumbe wanaopaswa kuwemo kwenye bodi kwa mujibu wa sheria...kama vile gavana wa BoT, kamishna wa TRA, na wengine...kwa sababu hawa wanapaswa kuwamo kisheria na kwa kuwa wamekula fedha zetu hatuna imani nao tena. je atawateua tena kuwemo kwenye bodi (kama sheria inavyosema) au ataunda bodi mpya kama kwa kutumia sheria zake kam vile anavyoiendesh nchi kwa kutumia sheri zake binafsi?
 
nchi hii inasukwasukwa tu...mijitu inakula fedha za umma halafu inaachwa iendelee kutunisha macho mitaani bila kufungwa jela.
 
Magu aliwataka wale wajumbe watano tu kuwatumbua, yule Mwenyekiti anayechaguliwa na Rais na wale 4 wanaochaguliwa na Waziri wa fedha, Hawa ndio walikuwa targeted, Hao wengine as long as wanaendelea na position zao basi ikiundwa bodi mpya wamo!!
 
ARTICLE yako imeshiba sana bt maamuzi ya RAIS yalikua MUBARASHA zaid hasa kwa kipnd hiki.na yamewapendeza zaid watanzania kuliko article yako.
 
1480119085664.jpg
 
Kwa namna yoyote ni makosa kwa bodi kuidhinisha/kubariki maamuzi mabaya!

Lakini ni makosa zaidi kwa watendaji kuandaa mipango ya kuingiza ktk makosa bodi aidha kwa kujua ama kwa kutokujua!

Ndiyo inasemwa sasa hapa kuwa, kwanza utumbuaji huu ungeanza na Management ya TRA, kisha Bodi na mwisho kuwavua madaraka wajumbe wote wanaoingia ktk bodi ya TRA kwa nafasi zao ambao ni;

1. Katibu mkuu, Wizara ya Fedha - JMT

2. Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha - SMZ

3. Gavana wa BoT

4. Kamishina wa TRA
mi ninavyoelewa Bodi iko Juu ya watendaji. Sasa kama watendaji wako juu ya bodi basi sawa. Ni hii ndio Magufuli anayokataa. Katika maiusha yako yote jitahidi kuto-kucompromise nafasi yako uwe- baba wa familia, mama, mtoto, ukiwa na position Fulani. Of course binadamu wanaweza wasikuone wala kukuelewa lakini Mungu anakuona. Hii la bodi kukubali kupelekwa sijui mawapiwapi, fadhila zao au mwishowe wanakuwa chini ya watendaji. baba endelea safisha safisha, wazalendo bado wapo.
Hii inanikumbusha miaka ileeee ya nyuma. Nimeenda wizara ya elimu nilikuwa na duty ya kusafirisha wanafunzi. Wafanyakazi wale wa Enzi hizo wa wizara ya elimu ( wengi wao sio wote) yaani muhudumu anayepaswa kuchukua file from one point to another anakuzungusha. ( na mimi ni principal yangu, kwenye haki yangu siwezi toa kitu chochote asilani) any way lakina akatokea malaika ndani
 
Below standard!
The question comes: who sets the standards?

Mara nyingi, jambo la kijinga huwa halina muendelezo wenye tija. Malisa kauliza hivi: Juu ya nini watu wale wale wasio waadilifu waendelee na nyadhifa zao kwenye utumishi wa umma? Habari za standards waachie TBS
 
ARTICLE yako imeshiba sana bt maamuzi ya RAIS yalikua MUBARASHA zaid hasa kwa kipnd hiki.na yamewapendeza zaid watanzania kuliko article yako.
Tumia neno baadhi ya Watanzania. Hoja ya msingi si nani kapendezwa, ishu ni usahihi. Wingi wa watu hauhalalishi ubora wa maamuzi.
 
MMP naona unamapenzi binafsi Na huyo Malisa.Kwa sababu tu kapiga ikulu Basi tumfanye NABII EEEEH.
Simjui kama ambavyo hanijui. Hapa naizungumzia hoja yake, sio yeye mwenyewe. Mapenzi binafsi ni pale tunaposhangilia kila anachoongea mtu fulani, hiyo ni tofauti na mimi na Malisa. Ndio leo nasoma bandiko lake, mapenzi yako wapi?

Kwa kuwa hakuna sehemu nilikomuita nabii, labda tungerudi kwenye hoja yake...wewe unaionaje, na unaijibu vipi?
 
The question comes: who sets the standards?

Mara nyingi, jambo la kijinga huwa halina muendelezo wenye tija. Malisa kauliza hivi: Juu ya nini watu wale wale wasio waadilifu waendelee na nyadhifa zao kwenye utumishi wa umma? Habari za standards waachie TBS
Nani alisema siyo waadilifu? Rais katengua uteuzi kwa kuruhusu fixed deposit, wewe unasema siyo waadilifu. Polar opposite!
Najua kwa elimu yako unastahili kuwa Headteacher. Je, ukishindwa majukumu ya headteacher hufai kuendelea na ualimu wako wa teknohama?
 
Woteeeeeeeeeee wanaopiga makofi kwenye ujinga kama huu akili zao ni zaidi ya ujinga
 
Back
Top Bottom