Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.
Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.
Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."
Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"
Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.
That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.
Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.
Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.
That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.
Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!
Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.
Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.
Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.
Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?
Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.
JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.
Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.
Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?
Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.
Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.
Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!
Malisa GJ
You have a VALID point!
Japokuwa nao memba wa bodi ni lazima wawe makini, well informed na wenye kuuliza maswali kabla ya kuidhinisha jambo kama hilo.
Kwa mfano one of the Board members could resent na kusema
"Mimi naona kuna maswali na ninaona sitaweka saini yangu hapo"
Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa kama vigogo wote wa juu wali push. Basi board haina namna niku timiza matakwa ya wakuu hawa:
MAKATIBU wakuu wa FEDHA Bara na Visiwani
KAMISHINA wa MAPATO TRA na
GAVANA wa Benki kuu.
Hawa ni liability na wachukue njia fupi katika mambo ya kiofisi yaani collective responsibility na kufanya jambo la heshima WAJIUZULU kabla HAWAJAFUKUZWA!!
Vinginevyo Rais Magufuli atakuwa anafanya SELECTIVE justice na DOUBLE STANDARD katika maamuzi yake na hiyo ita kuwa ni bad precedent/ Mfano mbaya wa kuigwa
Na hawa jamaa WATAACHWA basi ni kusema kwa kuwa walizoea, watatafuta njia nyingine ya kula pesa za serikali kwa kutumia staili tofauti!