Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

Pamoja na kwamba bodi imekutana mara moja ila inapata taarifa kuwa kuna kitu hiki na hiki kilichofanyika. Na pia bado kuna maswali mengi juu ya maelezo ya mkuu. Je akaunti ilifunguliwa lini? Watia sahihi ni nani na nani, je malengo yalikuwa ya kumnufaisha nani?
 
Mimi ni swali ?
kama JPM akitaka kuunda bodi nyengine inakuwaje ?
kwa sababu nadhani bodi ina undwa kwa formation hii kama ulivyo eleza
-Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

sasa hao si lazima watoke kwenye post zao wa ingie wengine ndo waunde bodi ?

Donald alisema-i love poorly educated people..
Lowassa aliseama-elimu,elimu na elimu
jpm alisema-ajesema kitu alipiga push up tu...

twendeni na kazi..
Gd question, hiyo bodo mpya sura zile zile zitarudishwa kma haxikupisha.
 
Mkuu, pamoja na maelezo yako marefu umeshindwa kufafanua kuhusu hizo fedha kama zilikusanywa lini labda tungenzia hapo.

Pili, raisi JPM amefafanua vizuri tu kuhusu fedha zinazokusanywa kwa niaba ya serikali zinavyopitiliza kwenda kwenye FDA bila kupitia serikalini wakati TRA na vyombo kama TANAPA vinakusanya mapato kwa niaba ya serikali.

Pia raisi amefafanua matumizi ya fedha za aina mbili zile za mapato na zile za miradi kama ule wa TEA ambao wamepewa fedha za kujenga shule na kutengeneza madawati na wao wakaenda moja kwa moja kufungua akaunti ya FD.

TRA ,TANAPA zinapaswa kupeleka fedha za mapato serikali kuu.

Msichokielewa ni nini khasa?

1. Uzuri ni kwamba wote tumemsoma mleta hoja. Labda tofauti ni namna kila mtu alivyomuelewa.

2. Mleta mada alichojadili ni namna ya hatua za wale wanaosemekana kuwa "wakosaji" walivyoadhibiwa na sio modality ya namna pesa zinavyokusanywa na TRA...kivipi na zinakwenda wapi!!

3. Mleta mada hakujadili kama management ya TRA na bodi yake walifanya kosa kufungua Fixed Deposit Account ktk benki za kibiashara ama laa!!

4. Kwa mtazamo wa Rais Magufuli na washauri wake, hilo ni kosa na ndiyo maana "kaitumbua" bodi hii.

Na kwa nilivyoelewa mimi, hili ndilo linaloleta msingi wa mjadala huu, kwamba, kuna makosa ya kiufundi ktk maamuzi haya yaliyochukuliwa na Rais Magufuli. Angeenda mbele zaidi ya bodi!!

Kwamba, inaleta taabu kidogo kuivunja bodi huku ukiiacha management ya TRA ambao ndiyo watendaji wa shughuli za siku kwa siku za Mamlaka ya Mapato Tanzania!

Si hivyo, bali inaleta taabu kidogo kuyaelewa na kuyaamini maamuzi haya kama ni ya kizalendo kweli au kuna kitu kingine tu nyuma ya pazia kilichofichwa nyuma ya uamuzi huu!

Kwa sbb miongoni mwa wajumbe wa bodi hii ni watu ambao wana hold positions nyeti na kwa sbb ya nafasi zao kisheria wanaingia moja kwa moja kama wajumbe wa bodi hii "iliyotumbuliwa" kwa tuhuma za kubariki ufisadi kwa mujibu wa "mtukufu" Rais!!

Watu hawa kwa nyadhifa zao ni Gavana wa BoT, Katibu Mkuu - WF - JMT na Katibu Mkuu WF- SMZ na Kamishna Mkuu wa TRA.

Sasa hawa watawezaje kuwa wachafu na mafisadi kwenye bodi ya TRA at the same time wawe clean ktk taasisi zao wanazozisimamia??

Haiingii ktk akili za watu wanaofikiri vizuri, labda inawezekana kwa watu ambao akili zao zimefungiwa kwenye vibuyu pekee!!

Mwisho kabisa, naamini haya uliyohoji wewe hapa yanapaswa kuanzishiwa uzi separate kabisa nje ya huu wa Malisa GJ. Au unaonaje bhana? Niko wrong?
 
Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.

Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.

Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."

Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"

Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.

That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.

Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.

Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.

That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.

Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!

Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.

Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.

Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.

Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?

Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.

JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.

Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.

Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?

Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.

Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!

Malisa GJ
in GJ Malisa and Ben Saanane, Chadema mmepata bahati kubwa sana kupata vijana wenye uwezo mkubwa wa ku-analyse mambo kwa nyuzi 360.

sina uhakika huwa mnawatumia kwa kiasi gani katika chama chenu lakini I urge you people to utilize the unique talents of these 2 young men especially kwenye kitengo cha mawasiliano. yule mtu mwingine mlinaye pale kwenye hii role kwa sasa (anaitwa Makene or something) atafutiwe majukumu mengine ili hawa wawili (au mmoja wao) wachukue mikoba.
 
Kiongozi Nina swali moja, kuna haja gani Kua na bodi isiyo na Uwezo wa kusimamia kindakindaki watendaji?

Au kama hivyo ndivyo kwanini bodi inakutana Mara chache kwa mwaka wakati kuna mambo mengi ya kufuatilia kutoka kwa watendaji?
kwa hiyo Bodi inakubali kuwa Rubber Stamp. jamani isome hata zama basi!
 
The Boss, nakuaminia kwa michango yako mingi ambayo ni objective, lakini hili hapana!
Ktk nchi hii, kwa mazoea ya utawala uliopita amri ilikuwa inatolewa na mtu wa chini bora tu awe connected. Usijekuta Bade alikuwa connceted kuliko Bodi yenyewe. Ndivyo ilivyokuwa siku zote za miaka 10 iliyopita. Mkuu wa Wilaya alikuwa anaweza kumkoromea mkuu wa mkoa wake!

Ninachoamini ni kwamba Rais yuko informed kuliko mtu yeyote, kwa taarifa rasmi. Rais ana vyombo vya taarifa kuliko mimi na wewe. Ana haki ya kujua hata mtu aliyelazimisha ndani ya kikao, au aliyetishia wengine. Maamuzi yakitolewa sisi tunasema, upendeleo au kulindana. HAPANA!
unata
Yaani we ndo kiazi kweli kweli. Kwanza umesema unatupa shule ya uchumi kumbe upuuzi mtupu, shule ya uchumi hapo iko wapi? Zipi economic modals ambao umezielezea? Mfani, CGE or Input output matrix modals au zinginezo. Au kwa vile akili yako ni ya kupinga tu kila kitu umeona usipitwe na hilo bila kuonesha upumbafu wako.
Kama ukawa mna wachambuzi vihiyo namna hii basi nimekubali ni genge LA wahuni na kakikundi Fulani ka wanaotaka kula tu kwa namna yoyote illegal au legal.
bahati mbaya huja pinga hoja yake kwa hoja,always muhuni au malaya huona wenzie kwa jicho hilo jitafakari mheshimiwa
 
kwa hiyo Bodi inakubali kuwa Rubber Stamp. jamani isome hata zama basi!

Kwa namna yoyote ni makosa kwa bodi kuidhinisha/kubariki maamuzi mabaya!

Lakini ni makosa zaidi kwa watendaji kuandaa mipango ya kuingiza ktk makosa bodi aidha kwa kujua ama kwa kutokujua!

Ndiyo inasemwa sasa hapa kuwa, kwanza utumbuaji huu ungeanza na Management ya TRA, kisha Bodi na mwisho kuwavua madaraka wajumbe wote wanaoingia ktk bodi ya TRA kwa nafasi zao ambao ni;

1. Katibu mkuu, Wizara ya Fedha - JMT

2. Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha - SMZ

3. Gavana wa BoT

4. Kamishina wa TRA
 
Kumuelewa Malisa kunahitaji utulivu katika kusoma alichoandika.
Kama nimemuelewa vizuri ni kwamba:
i. Kwa ujumla anakubaliana na hatua alizochukua JPM.
ii. Bodi na watendaji wote walikosea, ila JPM kaanza na Bodi, sasa hoja ni kwamba hao wajumbe wa bodi (wapanga deal) walipata ujumbe huo kwa nyadhifa zao zingine, sasa swali je Kama wameachwa kwenye hizo nafasi zilizowapa sifa ya kuwa wajumbe wa bodi, je kwakuwa wameachwa si wanaweza kuendelea na hujuma hata huko waliko? Kama kufukuzwa ujumbe wa bodi labda ingetakiwa na zile nyadhifa zingine walizonazo wangeachishwa.
Hivyo badala ya kuendelea kupiga vigelegele, kama wananchi tupige kelele hao wapiga deal wawajibishwe zaidi kwa kwenda kinyume na agizo la Rais, ikibidi na hizo nyadhifa zao zingine wapigwe chini ili liwe funzo
 
Kwa namna yoyote ni makosa kwa bodi kuidhinisha/kubariki maamuzi mabaya!

Lakini ni makosa zaidi kwa watendaji kuandaa mipango ya kuingiza ktk makosa bodi aidha kwa kujua ama kwa kutokujua!

Ndiyo inasemwa sasa hapa kuwa, kwanza utumbuaji huu ungeanza na Management ya TRA, kisha Bodi na mwisho kuwavua madaraka wajumbe wote wanaoingia ktk bodi ya TRA kwa nafasi zao ambao ni;

1. Katibu mkuu, Wizara ya Fedha - JMT

2. Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha - SMZ

3. Gavana wa BoT

4. Kamishina wa TRA

..siyo hao tu.

..kuna wajumbe wengine wa bodi hiyo ni watumishi wa serikali.

..nimesoma kuna kamishna toka wizara ya fedha ni mjumbe wa bodi iliyovunjwa.

..lakini la msingi zaidi ni kwamba gavana,kamishna mkuu, na ps, watarudi ktk bodi mpya ya tra kwasababu sheria inaelekeza hivyo.
 
Hapa ni dhahiri Mhe. RAIS alishapanga kumtimua kazi Gavana na wenzake sasa amepata sabb.
 
..siyo hao tu.

..kuna wajumbe wengine wa bodi hiyo ni watumishi wa serikali.

..nimesoma kuna kamishna toka wizara ya fedha ni mjumbe wa bodi iliyovunjwa.

..lakini la msingi zaidi ni kwamba gavana,kamishna mkuu, na ps, watarudi ktk bodi mpya ya tra kwasababu sheria inaelekeza hivyo.

Kwa hili la mwisho, sidhani kama kuna shida kama tu zitaingia sura mpya nje ya hizi zilizotumbuliwa!!

Kama anataka kuthibitisha mashaka ya watanzania dhidi ya nia yake ya kupambana na ufisadi, basi Magufuli ashindwe kuifunga hii penati ambapo yuko yeye, goli na kipa pekee!!

He has no option to this........
 
Kwa hili la mwisho, sidhani kama kuna shida kama tu zitaingia sura mpya nje ya hizi zilizotumbuliwa!!

Kama anataka kuthibitisha mashaka ya watanzania dhidi ya nia yake ya kupambana na ufisadi, basi Magufuli ashindwe kuifunga hii penati ambapo yuko yeye, goli na kipa pekee!!

He has no option to this......
..

..kwa uelewa wangu hao wanaingia ktk bodi ya tra kutokana na nyadhifa zao.

..kamishna mkuu, ps wa hazina, ps wa fedha znz, na gavana wa bot, wakishateuliwa ktk nyadhifa hizo moja kwa moja ni wajumbe wa bodi ya tra.

..pia wakiondoka ktk nyadhifa hizo ujumbe wao kwenye bodi ya tra unakoma.

..mwingine ni secretary to the board. Huyu huwa ni mwanasheria wa tra. Lakini yeye huwa hapigi kura.

..ngoja nitapitia taarifa za tra kujiridhisha kuhusu muundo wa bodi ya wakurugenzi.
 
nipo sayari ya mars hapa nawachora tu.any way nawatakia kila lakheri ktk maamuzi yenu mnayoona yanawasaidia
 
Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.

Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.

Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."

Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"

Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.

That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.

Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.

Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.

That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.

Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!

Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.

Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.

Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.

Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?

Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.

JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.

Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.

Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?

Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.

Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!

Malisa GJ
wee malisa usilete porojo zako za kijinga. hujui wala corporate governance inavyo function. kwa ufupi sana usahihi ni kwamba bodi ni ndio ipo kwa niaba ya mwenye mali na ndio yenye madaraka na kuwajibika kwa mwenye mali hapa tuna maana serikali na kwa wananchi kupitia bunge. unashangaza unaposema eti bodi kazi yake ni ku rubber stamp. hiyo bodi ya kurubber stamp ndio bodi gani ya ajabu. hapa kuna maelekezo ya serikali wasifungue fixed deposit. kama bodi walitakiwa ku observe kama sera au kujenga hoja serikalini against uamuzi huo sio kupuuza. kweli day to day ni ceo na management lakini wanafanya within laid down policies budgets etc zinazosimamiwa na board. wacha kupotosha watu kwa faida ya kisiasa.
 
nipo sayari ya mars hapa nawachora tu.any way nawatakia kila lakheri ktk maamuzi yenu mnayoona yanawasaidia

Ivalishe nguo basi hoja yako mkuu.

Uko sayari ya Mars halafu unawachora? Kina nani hao unaowachora?
 
Mkuu, pamoja na maelezo yako marefu umeshindwa kufafanua kuhusu hizo fedha kama zilikusanywa lini labda tungenzia hapo.

Pili, raisi JPM amefafanua vizuri tu kuhusu fedha zinazokusanywa kwa niaba ya serikali zinavyopitiliza kwenda kwenye FDA bila kupitia serikalini wakati TRA na vyombo kama TANAPA vinakusanya mapato kwa niaba ya serikali.

Pia raisi amefafanua matumizi ya fedha za aina mbili zile za mapato na zile za miradi kama ule wa TEA ambao wamepewa fedha za kujenga shule na kutengeneza madawati na wao wakaenda moja kwa moja kufungua akaunti ya FD.

TRA ,TANAPA zinapaswa kupeleka fedha za mapato serikali kuu.

Msichokielewa ni nini khasa?
Akili mbovu ni hata kutoelewa alichosema rais. Pesa ile haikuwa ya makusanyo ila ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi wanayogaiwa. Halafu TRA hawafanyi biasha zaidi ya kutekeleza majuku yao kisheria. Malisa jifunze nature ya board kwanza kabla ya kuleta siasa. Pili mmamuzi ya kuhamisha pesa za taasisi kwa matumizi ya OC na development kwenda katika matumizi mengine hasa ya kuwekeza fixed account hiyo ni moja ya corporate decision of an organization ndio maana ikapata kibali cha board vinginevyo menejimenti wangeamua wao. Ujinga utatufikisha kubaya.
 
Malisa kuna kitu hajakielewa
Bodi ya TRA ina nguvu kuliko kamishna

ndo maana mimi nilihoji why Badie aondolewe?
huku bodi ikibaki?

sasa Magufuli kafanya kivingine this time
kaondoa bodi huku kamishna kabaki...

Magufuli anawalinda watu wake...
Kwa maelezo ya Malisa, kama ni kweli ina maana kuwa Gavana wa Bank kuu na makatibu wakuu wa Wazara ya Fedha Bara na Visiwani wao hawajafukuzwa kwa kuwa watarudi tena kutokana na nyadhifa zao!! Issue hapa itakuwa ni Mwenyekiti. Ndiye aliyekuwa target!! Hapa imetafutwa sababu tu ya kumalizana naye!
 
Back
Top Bottom