Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

Maajabu ya Rais Magufuli na bodi ya TRA

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.

Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.

Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."

Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"

Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.

That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.

Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.

Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.

That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.

Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!

Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.

Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.

Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.

Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?

Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.

JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.

Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.

Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?

Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.

Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!

Malisa GJ
 
Kiongozi Nina swali moja, kuna haja gani Kua na bodi isiyo na Uwezo wa kusimamia kindakindaki watendaji?

Au kama hivyo ndivyo kwanini bodi inakutana Mara chache kwa mwaka wakati kuna mambo mengi ya kufuatilia kutoka kwa watendaji?
 
Malisa kuna kitu hajakielewa
Bodi ya TRA ina nguvu kuliko kamishna

ndo maana mimi nilihoji why Badie aondolewe?
huku bodi ikibaki?

sasa Magufuli kafanya kivingine this time
kaondoa bodi huku kamishna kabaki...

Magufuli anawalinda watu wake...
 
Ajasema bodi haina makosa ,lakini ishue kama JPM aliamua kuiadhibu bodi inakuaje watendaji wanabaki ? ishu vikao vya bodi ni mara ngapi kwa mwaka inategemea sheria na taratibu inasema nini alafu kumbuka bodi sio watendaji wa kila siku wao ni wapokea taarifa
 
Malisa kuna kitu hajakielewa
Bodi ya TRA ina nguvu kuliko kamishna

ndo maana mimi nilihoji why Badie aondolewe?
huku bodi ikibaki?

sasa Magufuli kafanya kivingine this time
kaondoa bodi huku kamishna kabaki...

Magufuli anawalinda watu wake...

Ni kwelii mkuu bodi ina nguvu kuliko kuliko management.lakin kama ishu ni makosa ya kiutendaji haiwezekani ukaicha management kuiadhibu
 
Kiongozi Nina swali moja, kuna haja gani Kua na bodi isiyo na Uwezo wa kusimamia kindakindaki watendaji?

Au kama hivyo ndivyo kwanini bodi inakutana Mara chache kwa mwaka wakati kuna mambo mengi ya kufuatilia kutoka kwa watendaji?
Mkuu Bodi hizi zimekuwa na matatizo makubwa mno. Bodi hizi ndizo zimeshiriki kwa asilimia 100 kufilisi mashirika ya umma. Kuna Bodi ya taasisi ya Bahari (DMI) wamekuwa wakimlipa mshahara Mwenyekiti wa bodi kwa kisingizio kuwa ni posho. Bodi zimekuwa zikiridhia taasisi kufanya madudu kibao kwa sababu hata wenyeviti na wajumbe wa bodi hizi wamekuwa wakinufaika. Hiki hiki chuo cha Bahari, walipewa bilioni 2.8 na serikali mwaka 2013 kwa ajili ya kufidia wananchi huko Mkuranga ambako taasisi hii ilinunua eneo. Aliyepewa kuzimamia mradi huo alikuwa Mkuu wa chuo Mipango fedha na Utawala, cha ajabu zaidi ya shilingi milioni 400 plus ziliishia kugawanwa kati uongozi wa chuo Pamoja na Mwenyekiti wa Bodi. Hebu fikiria jinsi gani bodi hizi zilivo za hovyo. Alichokifanya Magufuli siyo kibaya. Ila asiishie kuvunja bodi tu na Management nao wawajibishwe.
 
Malisa kuna kitu hajakielewa
Bodi ya TRA ina nguvu kuliko kamishna

ndo maana mimi nilihoji why Badie aondolewe?
huku bodi ikibaki?

sasa Magufuli kafanya kivingine this time
kaondoa bodi huku kamishna kabaki...

Magufuli anawalinda watu wake...
Ntakulinda ili unifae baadaye .
 
Nimemsikiliza Mhe.JPM leo ktk taarifa ya habari akieleza sababu za kuivunja Bodi ya TRA. Anasema watendaji wa TRA walikuwa wanachukua fedha zao za kujiendesha na kuziweka kwenye Fixed A/c katika mabenki mbalimbali ili wapate faida binafsi. Kwahiyo serikali inatoa pesa inawapa TRA, then TRA wanazichukua na kuziweka bank kwny fixed a/c halafu bank wanatumia pesa hizo kuikopesha serikali kwa riba kubwa. Kwa maana hiyo akaamua kuivunja Bodi ya TRA.

Wapiga zumari wa Mfalme kama desturi yao wameanza kupiga makofi na kutoa sifa kadha wa kadha kuonesha kuunga mkono maamuzi hayo. Lakini nimegundua ili uweze kupongeza uamuzi huu unatakiwa uwe na uelewa mdogo sana wa masuala ya kiuchumi na mambo ya utawala. Wanaoshangilia hawajui Bodi ni kitu gani, inafanyaje kazi, inawajibika kwa nani? Wao ni kupiga tu makofi ili mradi "Mfalme" awaone.

Anyway, kwa kuwasaidia ngoja niwape shule kdg. Bodi ya TRA kama zilivyo Bodi za mashirika mengine duniani ni non executive organ. Bodi ya TRA sio excutive, yani sio chombo kinachosimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za TRA. Sheria ya uanzishwaji wa TRA (Tanzania Revenue Authority Act, of 2006) kifungu cha 10(2) kinasema "The Board shall be a statutory organ responsible for the formulation and implementation of the policy of the Authority."

Na kifungu cha 10(4) kinasema "The Board may delegate to any member the power and authority to carry out on behalf of the Authority, such functions as the Board may determine"

Kwa mujibu wa vifungu hivi viwili shughuli za kila siku za TRA zimekaimishwa chini ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA na watendani wake kama ilivyoelezwa pia katika sheria hiyo kifungu cha 16. Kamishna Mkuu ndiye mkuu wa Executive issues zote za TRA ikiwa ni pamoja na masuala ya ajira, mapato, matumizi na shughuli zote za utendaji. Yeye na Wakurugenzi wake na wakuu wa vitendo mbalimbali hupeleka ripoti zao kwenye Bodi ya TRA angalau mara moja kwa mwaka.

That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka. Kamishna Mkuu wa TRA ndiye kama CEO au MD wa shirika. Chini yake kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na watendaji wengine. Hawa ndio hushughulika na masuala yote ya kila siku ya TRA. Bodi husubiri kupelekewa taatifa ya mipango na utekelezaji angalau mara moja kwa mwaka.

Kwahiyo kama ni deal ya kuficha pesa za TRA kwenye Fixed a/c sio issue ya Bodi. Ni issue ya management ambayo ndicho chombo executive. Kamishna na watendaji wake ndio wanaopanga kila kitu, halafu wanapeleka kwny Bodi kwa ajili ya kuseek approval.

Kwa kuwa Bodi inakaa mara moja tu kwa mwaka, kuna mambo mengi huwa yanaletwa kwa ajili ya kuseek approval. Kwa hiyo ni ngumu sana wajumbe wa Bodi kujua in details undani wa kila jambo. Watendaji ambao kimsingi wao ndio wataalamu, wanaweza kutumia opportunity hiyo kuwapotosha wajumbe wa Bodi. Wanawaambia "tuna mpango wa kuweka pesa kwny fixed a/c ni mpango mzuri na wenye faida" kisha wanataja na faida chache. Bodi inaona ni jambo jema, so ina approve. Kumbe ni deal la watu.

That means wanaopanga kila kitu ni watendaji, na Bodi ni watia muhuri tu. Bodi haijui mambo mengi kuhusu mipango ya TRA. Wanaojua ni watendaji, wanaokula dili ni watendaji, wanaoiba ni watendaji, wanaodeal na shughuli za kila siku ni watendaji. Kila kitu kinafanywa na watendaji.

Sasa katika mazingira haya kama TRA imehujumu pesa za umma unamuadhibu nani kati ya Bodi au watendaji? Kimsingi utashughulika na watendaji kwanza then Bodi baadae. Lakini eti Bodi imevunjwa halafu watendaji waliokula deal wanachwa, na watu wanashangilia. Uzwazwa.!

Hivi mnajua kazi za Bodi au mnatania? Yani deal iipangwe na watendaji, itekelezwe na watendaji, ipigwe na watendaji halafu Bodi iadhibiwe? Maajabu.

Simaanishi Bodi iko decent 100%, but my point ni kwamba JPM alitakiwa aanze na Watendaji kwanza kabla ya Bodi. Amfukuze kazi mtendaji mkuu wa TRA ambaye ni Kamishna Mkuu maana huyu ni signatory wa hizo documents huko bank zilizoidhinisha kufungua hizo fixed account. Hizo fixed account zisingeweza kufunguliwa bila saini ya Kamishna Mkuu wa TRA.

Hata Rais mwenyewe amesema "Wakuu wa Mashirika wamefanya mchezo huu muda mrefu, na wanapata mapesa mengi wanazigeuza Bodi kuwa inferior kwao." Hiki ni kielelezo kwamba JPM anajua kwamba wanaokula hizi hela ni wakuu wa mashirika, na sio Bodi. Ingekua ni deal ya Bodi basi bodi hizo zisingekubali kugeuzwa inferior na Wakuu wa mashirika.

Sasa kama JPM anajua ni deal ya wakuu wa Mashirika, imekuaje aivunje bodi badala ya kumfukuza kazi Kamishna Mkuu wa TRA na watendaji walioshiriki?

Haiingii akilini kabisa kwamba JPM anajua waliofanya deal ni watendaji, halafu anaivunja Bodi na kuwaacha watendaji wakipeta, halafu watu wanamshangilia. Nadhani hata JPM anawashangaa wanaomshangilia. Mwal.Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga na wewe ukakubali anakudharau." Im guessing JPM anawadharau wanaomshangilia.

JPM alipaswa kumfukuza kazi Kamishna mkuu wa TRA, na watendaji wote waliohusika, kabla hajafikiria kuivunja Bodi ya TRA.

Lakini kuvunja Bodi na kuwaacha watendaji wakiendelea kupeta wakati watendaji ndio wamepanga hiyo deal si SAHIHI hata kidogo. Ni sawa na kusema katika Halmashauri fulani Mkurugenzi na watendaji wake wafanye ufisadi, halafu Rais avunje baraza la madiwani kwa sababu ya ufisadi huo, then amuache mkurugenzi na watendaji wake wote katika nafasi zao, bila kuwachukulia hatua zozote.

Anyway. Ngoja tumuamini JPM. Tuachane na hayo mambo ya kusema sijui Bodi sio watendaji. Tufanyie kazi alichosema Mhe.JPM kwamba Wajumbe wa Bodi walishiriki kupiga deal. Kama aliyosema JPM ni kweli kwamba wajumbe wa Bodi walipiga deal, kwanini bado wameachwa katika nafasi zao zingine za utumishi?

Nadhani kuna watu hawajanielewa, ni hivi; kwa mujibu wa sheria ya TRA, ya mwaka 2006 kifungu cha 16, kinawataja wajumbe wa Bodi ya TRA kuwa ni; Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais, Katibu Mkuu wizara ya Fedha (Muungano), Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zanzibar), Gavana BOT, Kamishna mkuu wa TRA, na wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha.

Sasa Rais ametuambia Bodi ilicheza na pesa zetu kwa kuziweka kwenye Fixed Account. This means waliohusika ni waliotajwa hapo juu. Yani Katibu mkuu wa wizara ya fedha bara na yule wa Zanzibar walicheza na pesa zetu. Gavana wa BOT alicheza na pesa zetu. Kamishna mkuu TRA alicheza na pesa zetu. Lakini ajabu ni kwamba wote wamevuliwa ujumbe wa Bodi lakini bado wapo kwenye nafasi zao za urumishi.

Yani wameondolewa kwenye Bodi ya TRA lakini nafasi zao zilizowafanya kuwa wajumbe wa Bodi hazijatenguliwa. Gavana bado yupo BOT, Makatibu wakuu wa wizara za fedha bado wapo kwenye wizara zao, Kamishna bado yupo TRA etc. Na huko walipo wanasifiwa kuwa ni wachapakazi hodari, licha ya kwamba kwenye wanadaiwa walipiga dili. Paradox.!

Malisa GJ

Mkuu, pamoja na maelezo yako marefu umeshindwa kufafanua kuhusu hizo fedha kama zilikusanywa lini labda tungenzia hapo.

Pili, raisi JPM amefafanua vizuri tu kuhusu fedha zinazokusanywa kwa niaba ya serikali zinavyopitiliza kwenda kwenye FDA bila kupitia serikalini wakati TRA na vyombo kama TANAPA vinakusanya mapato kwa niaba ya serikali.

Pia raisi amefafanua matumizi ya fedha za aina mbili zile za mapato na zile za miradi kama ule wa TEA ambao wamepewa fedha za kujenga shule na kutengeneza madawati na wao wakaenda moja kwa moja kufungua akaunti ya FD.

TRA ,TANAPA zinapaswa kupeleka fedha za mapato serikali kuu.

Msichokielewa ni nini khasa?
 
Unachotetea ni nini? Kwamba Bodi haikuwa na makosa au ulitaka siku hiyo hiyo mtendaji mkuu naye afukuzwe kazi? Umeandika hivi: "That means watendaji ndio wanaopanga kila kitu then wanaleta kwenye Bodi ili kupata baraka." Ulimaanisha bodi ilitoa baraka akaunti hiyo ifunguliwe. Nani ashikishwe adabu kwanza? Bodi iliyobariki au mtendaji aliyeomba kuruhusiwa?

Maswali kama hayo yaliibuliwa wakati wale jamaa wa pesa ya maafa Kagera wanakamatwa. Ooh mkuu wa mkoa kaachwa, ooh sijui na yule akamatwe. Lakini sisi tunaojidai kujadili hatujiulizi zaidi ya hapo kwa kudhani Rais anapungukiwa taarifa kama sisi hapa JF. Rais hawezi kupungukiwa taarifa za aina hiyo. unawajua Polisi jamii ktk ofisi yako wako wangapi?

Tusichoshe vidole kujidai kuwa analytical wakati kosa liko wazi. Kama ataamua kumuachisha mtendaji mkuu wa TRA hiyo ni kwa info alizonazo ambazo wewe huna. Ulitakiwa ugundue kwamba hao board members wa TRA, kiutendaji wa serikali ni bosses wake. Unajua ni nani aliyeleta wazo hilo kwa kamishna wa TRA? stop guessing facts!
 
Kwani kisheria majukumu ya bodi ni yapi.?
 
Tufanye kuwa upo sahihi. Hebu jibu swali lake la mwisho la kwanini hao watu bado wapo kwenye nafasi zao?
 
Back
Top Bottom