Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

hakuna lolote kujidejesha tu wadogo zangu wawili walitiwa mimba home tulikuja gundua siku ya kujifungua imefika hakuna cha rang dagaa wala maembe
Mimba ya kubebea nyumban tofauti na ukiwa kwa mumeo nyumban lazima kujificha kuhakikisha watu hawagundui mapema mi nilikuwa sipend samaki nikula kibish then naenda kutapka choon na hakuna mtu alojua hilo, mimba ikagundulika na miez sita
 
hakuna lolote kujidejesha tu wadogo zangu wawili walitiwa mimba home tulikuja gundua siku ya kujifungua imefika hakuna cha rang dagaa wala maembe
Wewe ndugu futa hiyo kauli yako,hukua unakaa nao Masaa yote unajua waliyokua wanapitia?
 
mimi ni mwanaume sidhani kama ni nafasi ya kupitia hayo labda kama unamaanisha vingine btw stay safe.
Huzijui mimba kaka, kuna wanaume wenzio huwapokea wake zao kulea mimba badala ya wake zao kutapika hutapika wao, badala ya wake zao kusikia kichefu chefu husikia wao na kudhoofika, ndo maana nimekwambia kama hujapitia ni bora ukakaa kimya ukatulia
 
sawa nimekusikia muda ukifika nitajua.
 
WiFi alikula filigisi miezi 9 tatizo kuzipata yaan kaka aliteseka kuweka order zikikosa ananunaaa siku nzima
 
Mke wangu mjamzito, ila sasa
Natapika Mimi,
Kichefu chefu mimi,
Nilipenda sana karanga, ila sasa nazichukia kuliko chochote.
Sipendi wali,
Napenda chakula cha ndimu nyingi.
Nalamba chumvi na ndimu kama chizi.
Imefikia hatua mke wangu kaniletea dawa za kurudisha humu ya Kula na kaniletea dawa za vitamini.
Nateseka sana. Sitaki sikia habari za mimba.
 
Duh Umenikumbusha mbaaaali sana, bado kidogo niwe mvuta siagara sports maana mimba ya mwenzangu ilipenda sports nikawa nanunua nazificha home, akikumbuka tuu tunawasha napuliza pafu hewani anafurahia harufu ya moshi wake!!
Mkeo kazaliwa jikoni kuliwa na MOSHI mwingi
 
Mimba kiboko jaman heshima kwa wanawake wote waliozaa kuna mshkaj jiran yetu yy lazma kila cku amsindikize mkewe sheli akanuse harufu ya petrol na diesel
 
Huzijui mimba kaka, kuna wanaume wenzio huwapokea wake zao kulea mimba badala ya wake zao kutapika hutapika wao, badala ya wake zao kusikia kichefu chefu husikia wao na kudhoofika, ndo maana nimekwambia kama hujapitia ni bora ukakaa kimya ukatulia
Mtaani kwetu kuna bibi anasifika kwa kuwasaidia wakina mama kuhamisha madhira ya mimba kwa waume zao!! Wamama watata wanamsifia ile mbayaa!!
Mara hii umesahau nilichokuahidi wewe Joanah?
 
Habarini Wadau,

Leo asubuhi niliamka nikiwa na mood mbaya ila wakati nakunywa chai nikajikuta naanza kucheka sana na kila nikikumbuka najikuta nacheka tu hata kimoyoni.

Ni hivi nina Kaka yangu, ni mtu mzima tu na alishaoa na kuwa na mtoto mmoja na sasa mkewe ni mjamzito hivyo anatarajia mtoto wa pili.

Asubuhi nimempigia simu mama kumjulia hali, baada ya maongezi mafupi akaniambia kwa kilugha

"Hivi wewe huwezi kupiga nyumba rangi?"

Nikamwambia hapana mama, mara akaniambia

"sasa si ukaongee na kaka yako kuhusu huyo mpiga rangi?"

Akaongeza..."Nyie ni watu wazima sasa msinisumbue" akakata simu.

Ikabidi nimpigie kaka kujua kuna nini juu ya mpiga rangi.

Kumbe bana wiki mbili zilizopita alimleta mpiga rangi kwenye nyumba yake kwaajili ya kubadilisha rangi sebuleni kwake.

MAAJABU:

Mke wake (shemeji yangu) ambaye ni mjamzito aliipenda sana harufu ya ile rangi ya ukutani na kila mara alipenda kukaa sebuleni siku nzima tena karibu na ukuta kabla rangi haijakauka.

TATIZO LILIPOANZIA:

Mke wa brother alichukua namba ya simu ya fundi rangi kumbe akawa anamwambia mara kwa mara

"Fundi si uje kurudia rangi koti nyingine jamani" kwani nilikufukuza kwangu? na alikuwa akimkumbusha mara kwa mara na mume wake akaja kuona messages ila hakumuuliza chochote.

Sasa mtoto wake kachafua ukuta kwa kuchora chora ndio kaka kaja juu kuwa mke wake ndio kachafua kwa makusudi ili nyumba ipigwe rangi na fundi yule yule.

Jana alipomtembelea mama jana ndio akamwambia anahisi mke wake anamsaliti kwa kutembea na fundi rangi.

Sasa mama anachosema ni kwamba "Mimba" yake ndio imependa hiyo harufu hivyo kaka aache kulia lia.

Hivi Kweli mimba ya mwanamke inaweza kupenda harufu kali kama hiyo ya rangi na wakati inaletaga hadi mafua?

Najua mwanamke akiwa mjamzito anaweza kupenda harufu ya dagaa ama malimao.

Ila Rangi?
mbavu zanguuu
 
Mtaani kwetu kuna bibi anasifika kwa kuwasaidia wakina mama kuhamisha madhira ya mimba kwa waume zao!! Wamama watata wanamsifia ile mbayaa!!
niunganishe nae Mkuu pls
 
Mke wangu mjamzito, ila sasa
Natapika Mimi,
Kichefu chefu mimi,
Nilipenda sana karanga, ila sasa nazichukia kuliko chochote.
Sipendi wali,
Napenda chakula cha ndimu nyingi.
Nalamba chumvi na ndimu kama chizi.
Imefikia hatua mke wangu kaniletea dawa za kurudisha humu ya Kula na kaniletea dawa za vitamini.
Nateseka sana. Sitaki sikia habari za mimba.
Naona mimba umeibeba wewe duh...ni ka uchawi au?
 
Back
Top Bottom