Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Duh Umenikumbusha mbaaaali sana, bado kidogo niwe mvuta siagara sports maana mimba ya mwenzangu ilipenda sports nikawa nanunua nazificha home, akikumbuka tuu tunawasha napuliza pafu hewani anafurahia harufu ya moshi wake!!
umeshatoka sober house?
 
sion mama alopenda kwenda jera kwa sabab ya mimba!!!
 
Jamani mi naomba mnifahamishe ni sehemu gani Dar hii hata nikienda saa nane usiku naweza kupata MISHKAKI maana jana niliagizwa MISHKAKI usiku saa nane sikwenda kutafuta, basi mpaka sahv nimekasirikiwa[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Daaaah! Me Dada angu alikuwa anakuagiza kaninunulie chips sajusi unafika sajusi chips zimeisha naamua kufata sehem nyingne ile nafika nampta tu akizfungua ananambia hizi cyo za sajusi anatupa kuleee

Sure, niliwahi kutumwa chips za kwa Edo, wakati huo tunaishi kimara, nikaenda Yenu Bar Ubungo nikachukua chips nikarudi, yaani ile kuzifungua tu akasema siyo zenyewe, nilikoma, maana siku hiyo tulilala bila kusemeshana, mimi kwa Edo sijaenda na yeye kakataa kuzila zile nilizompelekea.
 
Jamani mi naomba mnifahamishe ni sehemu gani Dar hii hata nikienda saa nane usiku naweza kupata MISHKAKI maana jana niliagizwa MISHKAKI usiku saa nane sikwenda kutafuta, basi mpaka sahv nimekasirikiwa[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Siyo kila unachoagizwa unaenda kuchukua mkuu, sasa huo usiku ukivamiwa na vibaka yeye atafaidika na nini?

Sometimes unamwambia awe reasonable, au kama vipi yeye mwenyewe aseme wapi anajua hayo masaa kuna mishkaki mkachukue wote.
 
Sasa Mimi ilikuwa inaomba bunduki hapo ndio nilichoka kabisa yaani acha kabisa
 
Kununa kawaida yangu siku hizi tena ukinikuta ngumi na mateke vimechanganya huko ndani hata unisemeshe sikujibu nakuangalia tu yaani mpaka nimshike mikononi ntakuwa nimekoma maana hayo mateke na ngumi sijui huwa ana rukaruka tumbo lote linatikisika nikikaa na mtu karibu anaona hilo gwaride sijui kama maini yangu yako salama khaaaaa
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Umenichekesha hapo pa maini.
 
Habarini wadau,

Leo asubuhi niliamka nikiwa na mood mbaya ila wakati nakunywa chai nikajikuta naanza kucheka sana na kila nikikumbuka najikuta nacheka tu hata kimoyoni.

Ni hivi nina kaka yangu, ni mtu mzima tu na alishaoa na kuwa na mtoto mmoja na sasa mkewe ni mjamzito hivyo anatarajia mtoto wa pili.
Asubuhi nimempigia simu mama kumjulia hali, baada ya maongezi mafupi akaniambia kwa kilugha

"Hivi wewe huwezi kupiga nyumba rangi?"

Nikamwambia hapana mama, mara akaniambia

"sasa si ukaongee na kaka yako kuhusu huyo mpiga rangi?"

Akaongeza..."Nyie ni watu wazima sasa msinisumbue" akakata simu.

Ikabidi nimpigie kaka kujua kuna nini juu ya mpiga rangi.
Kumbe bana wiki mbili zilizopita alimleta mpiga rangi kwenye nyumba yake kwaajili ya kubadilisha rangi sebuleni kwake.

MAAJABU:
Mke wake (shemeji yangu) ambaye ni mjamzito aliipenda sana harufu ya ile rangi ya ukutani na kila mara alipenda kukaa sebuleni siku nzima tena karibu na ukuta kabla rangi haijakauka.

TATIZO LILIPOANZIA:

Mke wa brother alichukua namba ya simu ya fundi rangi kumbe akawa anamwambia mara kwa mara

"Fundi si uje kurudia rangi koti nyingine jamani" kwani nilikufukuza kwangu? Na alikuwa akimkumbusha mara kwa mara na mume wake akaja kuona messages ila hakumuuliza chochote.

Sasa mtoto wake kachafua ukuta kwa kuchora chora ndio kaka kaja juu kuwa mke wake ndio kachafua kwa makusudi ili nyumba ipigwe rangi na fundi yule yule. Jana alipomtembelea mama jana ndio akamwambia anahisi mke wake anamsaliti kwa kutembea na fundi rangi.

Sasa mama anachosema ni kwamba "mimba" yake ndio imependa hiyo harufu hivyo kaka aache kulia lia. Hivi Kweli mimba ya mwanamke inaweza kupenda harufu kali kama hiyo ya rangi na wakati inaletaga hadi mafua?
Najua mwanamke akiwa mjamzito anaweza kupenda harufu ya dagaa ama malimao.

Ila Rangi?
X
 
Back
Top Bottom