Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Unaweza pitia pia, kuna ambao wakibeba taabu wanapata wanaume.
Haswaa atoto, mke wa shemeji yangu akiwa mjamzito tabu zote anapata mumewe, mwanaume ataumwa vitu havieleweki, mara ajiskie kutapika, mara aanze kuchagua vyakula, Inashangaza but mwenyewe alishajijua. Anasemaga kabisa kuwa mkewe akiwa na mimba tabu zote anabeba yeye mpaka atakapojifungua, sijui hata kuna connection gani za kibaolojia.
 
Kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi....

Nimecheka mbele za watu mpaka wananishangaa.
hahahahhahahahhahahahhahha we acha tu!
namwangalia mwanangu huwa naishia kucheka!
nilikuwa nataka kupigana na kila mwanaume!
saaaaasa itokeee nimekaa mahali akaja mtu ajifanye kutaka kunitongoza !
aseeeee nitamwaga vinywaji,namkunja,tumbo liko hapa na manzese!
mara sijui mlinzi mmoja wa hospitali nilikokuwa nafanya clinic alinisemesha niiiini sijui!uuuuuuuwih!
hakiiiiiiiii but nilikuwa na wanaume nawapendaa!ila wengine including bwana mkubwa aseeee walijutaaaaaaaaaaaa!
 
Patience123 nikikaa kukuhadisia visanga vyangu hata mwenyewe huwa nakufa kucheka mpk nakaa chini!
we ushawahi fikiria mtu mwanamke unatafuta supu ya kichwa cha mbuzi saa moja asbh?
mimba inataka mpk kubet mechi za mpira wa miguu,hakiiii nahis walinirogamo!
 
Me nakula miwa mpaka usiku na nyama au maini ya kaangwe na kitunguu tu afu kisiive vizur naamka mpaka usiku sana kula na nalala na maji pembeni full ruti za toilet nalala nusu nusu unasikia tu mara teke mara ngumi ya kibofu lazima uamke tu nikishusha huyu kiumbe nitashukuru niko hoi kweli
Duh, we kiboko.
 
uyu wakwangu mimba ilipenda kula
yani matumizi ya msosi yalipanda kutoka 300k kwa mwez adi 500k daah..ilikua shoti balaa
nilikonda kabisaaa
 
Waheshimiwe wanawake wotee, Mimi nilikuwa napenda biscuit mama wee sehemu nilokuwa nafanya kazi asubuhi nikifika nakuta biscuit hizoo, now ana miezi Tisa nikifika utasikia biscuit zako hizoo looh!!!
 
mimi nilikuwa sipendi kuchelewa hata dakika moja ikizidi naanza kulia mpaka leo sielewi ilikuwa nini? nilikuwa nakula viporo vya ndizi nyama... ndizi ikipikwa leo siipendi lazima ilale asubuhi niamke nacho nishinde nacho na usiku nile hicho .. halafu usiku zipikwe zingine za kisho loh
Nimeshangaa hapa,huwa nahisi hauna mtoto.
 
Acha tu shost yangu... Mimba nyingine niliwapenda sana watu jamani... Kila mtu ninayemuona moyo wangu una cherish...


Nilijikuta naelewana na kupendana na kila mtu, sikutaka mtu aje halafu aondoke....
Nilijikuta nina marafiki kibaoo wake kwa waume..

The kid is now 9 years old...

Alivyo maarufu sasa...

Anavyopendwa na watu sasa... toka kakiwa kachanga.
Yaani kila mimba na mambo yake jamani, ndio hii ulokuwa unapenda harufu ya sabuni?
 
Hii
Haswaa atoto, mke wa shemeji yangu akiwa mjamzito tabu zote anapata mumewe, mwanaume ataumwa vitu havieleweki, mara ajiskie kutapika, mara aanze kuchagua vyakula, Inashangaza but mwenyewe alishajijua. Anasemaga kabisa kuwa mkewe akiwa na mimba tabu zote anabeba yeye mpaka atakapojifungua, sijui hata kuna connection gani za kibaolojia.

Hii hata mimi huwa sielewi inakuwaje, kuna mwl mwenzetu mkewe ni mjamzito yaani hadi chai anakamulia limao, kuna siku atatema mate kutwa nzima, mara asinzie ofisini yaani tunamtaniaga, alafu ndio mtoto wa kwanza.
 
Mimba kiboko jaman heshima kwa wanawake wote waliozaa kuna mshkaj jiran yetu yy lazma kila cku amsindikize mkewe sheli akanuse harufu ya petrol na diesel
Hahaaahuyo mtoto atakua kma mlevi mana petrol inalewesha kuliko pombe
 
Kuna dada mmoja alichukia deodorant za wanaume wote wa kazini kwao, kila siku akija ofisini tu anaanza kutapika. Sasa utawaambia watu waache kutumia deodorant? Ilibidi aende likizo ya ugonjwa.
Kuna mdada mmoja kazini kwetu ye alipokuwa mjamzito alikuwa anapenda harufu ya perfume yangu ninayojipulizia, kila mara kazini alikuwa yuko beneath na mimi, mumewe akija kumtembelea anamkuta yupo na mimi, kwenye chai anakwenda na mimi hadi nikajishtukia kwa mumewe, ilibidi nimnunulie mumewe pafyum kama yangu ndio kidogo ikawa afadhali yangu.
 
Mke wangu ye anapenda harufu ya jasho langu sana sana tsheti yangu nikirudi nyumbani toka mazoezi pale kabla jasho halijakauka mi nikivua ili nifue ye anachukua na kuvaa
 
Mke wangu mjamzito, ila sasa
Natapika Mimi,
Kichefu chefu mimi,
Nilipenda sana karanga, ila sasa nazichukia kuliko chochote.
Sipendi wali,
Napenda chakula cha ndimu nyingi.
Nalamba chumvi na ndimu kama chizi.
Imefikia hatua mke wangu kaniletea dawa za kurudisha humu ya Kula na kaniletea dawa za vitamini.
Nateseka sana. Sitaki sikia habari za mimba.
Ndio mjue tunayoyapitia wake zenu kipindi cha ujauzito, 'cause kuna baadhi ya wanaume wanaona kama tunajifanyisha.

Waheshimuni wake zenu, tunabeba mimba kwa tabu na tunazaa kwa uchungu...
 
Kununa kawaida yangu siku hizi tena ukinikuta ngumi na mateke vimechanganya huko ndani hata unisemeshe sikujibu nakuangalia tu yaani mpaka nimshike mikononi ntakuwa nimekoma maana hayo mateke na ngumi sijui huwa ana rukaruka tumbo lote linatikisika nikikaa na mtu karibu anaona hilo gwaride sijui kama maini yangu yako salama khaaaaa
 
Kuna mtu mimba yake ilikuwa inapenda mabarafu (maji yaliyoganda)

Breakfast barafu
Lunch barafu
Dinner barafu

Inaonekana mimba ina mambo ya ajabu sana

Nasubiri kuona yangu itapenda nini
itapenda dushe kila muda
 
Sitasahau siku niliamshwa saa tisa usiku nikamtafutie embe bichi, nikatoka room nikaenda kulala sebuleni. Asubuhi ndo balaa, akasema nisiende kazini anataka kushinda na mimi nimkumbatie tu. Hizi mimba hizi, sijawahi kuzielewa.
mimi niliwahi zungshwa mtaa mzma namtaftia maembe. yaan
 
Back
Top Bottom