Maajabu ya mgunduzi wa umeme Duniani

Kuwite94

Member
Oct 10, 2016
16
117
Nikola Tesla alikua na akili kiasi cha watu kumuona ni mwendawazimu, lakin huyu ndo ameiwashia dunia umeme, ni mtu wa kwanza kugundua mawimbi ya radio, minara ya simu, wirelessly technology, leo hii maji/upepo/gas inageuka kuwa umeme, unasikiliza radio kutoka mbali, unapiga simu kwenda mbali ni miujiza iliyogeuzwa kuwa ya kweli, hizi modern technology unazoona sahiv ni maboresho tu ya zawad zake alizo ziachia dunia.

Lakin Tesla kwenye maisha yake hakua na Nyumba, mke wala mtoto, rafiki yake alikua ni njiwa tu, na kama angeendelea kuish kidogo bas alishaanza majaribio ya kuunganisha dunia kwa umeme usio tumia waya, Ila watu wenye tamaa ya pesa walichoma maabara yake na walimmaliza kabla hajakamilisha hilo kusudio lake, ubaya wa jamaa yeye alikua vitu anavyo vifikiria anakaa navyo kichwan tu na kuvifanyia kazi alikua anaandika Mara chache sana tena kidogo mno kiasi cha ukikuta ameandika kitu huwezi kuelewa kaandika nini,alafu hayo makaratasi yenyewe alikua anayatupatupa hovyo.

Africa yetu elimu tunayo pewa ni elimu iliyokua na mipaka mingi ambayo huruhusiwi wewe kuongeza mawazo yako, na akitokea mtu asie na cheti akaleta wazo tofaut anaonekana hana akili kumbe hata kina Tesla hawakua na vyeti na walipuuzwa mwanzo ila wakaibadilisha dunia, inawezekana ndo chanzo cha wenye elimu kuwa na uwezo mdogo wa kutatua changamoto kiasi cha wasio na elimu kuiona elimu haina thamani, maana asie na elimu inambidi atumie kiasi kikubwa cha uwezo wake wa kufikiri kutafuta solution hali ya kuwa mwenye elimu anatumia elimu aliyopewa darasani tu.

images.jpeg
 
Nikola Tesla pia ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa na uwezo wa kutumia mikono yote miwili (wa kushoto na wa kulia) kuandika kwa ufasaha.. pamoja na wanasayansi wengine kama Albert Einstein n.k.
Mbona hamuwaandiki wanasayansi weusi waliogundua Light Bulb kama lewis Latimer?

Unajua kwamba Kijana mweusi Ramarni Wilfred ame score IQ ya Juu zaidi ya 162 kupita Stephen Hawking, Albert Einstein na Bill gates?
 
Ndiyo na ndiyo Maana Elon Musk kwa heshima ya huyu mtu akaiita kampuni yake ya magari yakutumia umeme Tesla
Nope Tesla hajagundua umeme.., umeme ni phenomena iliyokuwepo tangia enzi na enzi ingawa kuna watu walioleta equations na laws of za umeme hao angalau tunaweza kuwaita wagunduzi wa umeme (laws za kwenye magnetism n.k.)

Tesla alikuwa an inventor na engineer, na baadhi ya vitu alivyotengeza kama Tesla Motor na alikuwa pioneer aliyewa-convice watu kutumia AC Current rather than DC Katika electric Distribution

Katika yote aliyofanya na ya kuongeza efficiency katika mambo mengi lakini hakugundua umeme...., Narudia Bora uwataje kina Maxwell na kina Faraday's waliochangia katika kuelewa laws zinazogovern umeme lakini sio Tesla....
 
Battle yake ya AC na ya Edison DC inayojulikama kama 'Current War' ni moja ya vitu vilivyomtambulisha kwenye tecknolojia,

Baada ya kumshinda Edison ambaye alikua anatumia njia za kikatili kuchafua umeme wa AC mfn kwa kupiga shoti tembo mpaka ikafikia hatau ya kugundua kiti cha umeme na hatimaye William Kemmler akawa binadamu wa kwanza kuuwawa kwa kiti cha umeme mwaka 1890 kuonesha madhaifu ya AC ya Tesla, lakini Tesla akashinda.

By the way hajagundua umeme huyu
 
Nikola Tesla alikua na akili kiasi cha watu kumuona ni mwendawazimu, lakin huyu ndo ameiwashia dunia umeme, ni mtu wa kwanza kugundua mawimbi ya radio, minara ya simu, wirelessly technology, leo hii maji/upepo/gas inageuka kuwa umeme, unasikiliza radio kutoka mbali, unapiga simu kwenda mbali ni miujiza iliyogeuzwa kuwa ya kweli, hizi modern technology unazoona sahiv ni maboresho tu ya zawad zake alizo ziachia dunia.

Lakin Tesla kwenye maisha yake hakua na Nyumba, mke wala mtoto, rafiki yake alikua ni njiwa tu, na kama angeendelea kuish kidogo bas alishaanza majaribio ya kuunganisha dunia kwa umeme usio tumia waya, Ila watu wenye tamaa ya pesa walichoma maabara yake na walimmaliza kabla hajakamilisha hilo kusudio lake, ubaya wa jamaa yeye alikua vitu anavyo vifikiria anakaa navyo kichwan tu na kuvifanyia kazi alikua anaandika Mara chache sana tena kidogo mno kiasi cha ukikuta ameandika kitu huwezi kuelewa kaandika nini,alafu hayo makaratasi yenyewe alikua anayatupatupa hovyo.

Africa yetu elimu tunayo pewa ni elimu iliyokua na mipaka mingi ambayo huruhusiwi wewe kuongeza mawazo yako, na akitokea mtu asie na cheti akaleta wazo tofaut anaonekana hana akili kumbe hata kina Tesla hawakua na vyeti na walipuuzwa mwanzo ila wakaibadilisha dunia, inawezekana ndo chanzo cha wenye elimu kuwa na uwezo mdogo wa kutatua changamoto kiasi cha wasio na elimu kuiona elimu haina thamani, maana asie na elimu inambidi atumie kiasi kikubwa cha uwezo wake wa kufikiri kutafuta solution hali ya kuwa mwenye elimu anatumia elimu aliyopewa darasani tu.

View attachment 2214062
Atakuja mtu atakwambia alisoma naye
 
Mbona hamuwaandiki wanasayansi weusi waliogundua Light Bulb kama lewis Latimer?

Unajua kwamba Kijana mweusi Ramarni Wilfred ame score IQ ya Juu zaidi ya 162 kupita Stephen Hawking, Albert Einstein na Bill gates?
Mimi binafsi nina 180 IQ
 
Back
Top Bottom